Ilipoishia “
Robson alijawa na mshangao kumsikia Mama yake akisema kuwa anamjuwa aliyemuuwa Sylvia, alishusha munkari kisha akamuuliza Mama yake kwa utaratibu sana
“Unamjuwa aliyempiga risasi Sylvia?”
“Ndiyo Namjuwa, Robson Naona aibu siku nikifa na siri hii ambayo inaweza kuleta taharuki kubwa kwako Mwanangu” Alisema kwa sauti iliyojaa kilio
“Nani aliyempiga risasi Mke wangu?” Aliuliza Robson
“Nakuomba Robson nikikutajia kaa chini ufikirie nini ufanye lakini usikurupuke na hasira utafanya maamuzi magumu, nakuomba weka Bastola chini” Alisema
“Mama huwezi kuniondoa katika njia yangu, najuwa aliyempiga risasi Sylvia ni Brahama sababu yeye ndiye aliyekuwa na Mke wangu, hakuna Mwenye uadui na Mke wangu” Alisema
“Si Brahama….” Alisema Mama Robson akafuta chozi akamwambia Robson
Tuendelee:
SEHEMU YA KUMI -10 (SEHEMU YA MWISHO)
“Ni Baba yako…!!” Macho yalimtoka pima Robson, kusikia ni Baba yake kulizidi kumshangaza Robson
“Baba yangu?”
“Ndiyo Baba yako ndiye aliyesababisha kifo cha Mke wako na alifanya hivyo akiamini anakulinda wewe Robson” Alisema Mama yake, Robson alijikuta akikaa chini, nguvu zikamuisha, jinsiBaba yake aliavyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Sylivia anapatikana, alijiuliza ilikuwaje akamuuwa
“Robson! Baba yako aliona unateseka kwa ajili ya Sylvia akaona ni bora amuuwe ili upate kuwa salama, hakufanya kwa nia mbaya naomba unielewe”
“Kwahiyo Baba yangu ndiye aliyemuuwa Mke wangu, ndiye aliyenifanya namwaga chozi sasa hivi? Mama unajuwa nimeumia kiasi gani ndani ya moyo wangu? Furaha yangu imetoweka, nina thamani gani Mimi?” Aliuliza Robson.
“Thamani unayo Mwanangu, hebu tuifiche hii siri ili Baba yako awe salama” Alisema Mama Robson, kadiri alivyomuona Robson aliona ni wazi alikuwa amepowa sakafuni, akamsogelea akamwambia
“Sahau yote, muache yule Kijana aubebe mzigo wote ili Baba yako abakie kuwa salama” Aliongezea Mama Robson
“Vipi familia ya Brahama, umeifikiria? wakati unataka Baba awe salama umepima ni maumivu kiasi gani anayasikia Brahama? atafungwa kifungo cha Maisha kwa kosa ambalo hakutenda, siwezi kuendelea kuitazama Dunia ambayo kila kitu kimebadilika” AliSema Robson kisha akasimama kama mzimu.
Akamnyooshea Bastola Mama yake, akamuamrisha atulie kisha akamfungia ndani ya chumba hicho, akakimbilia nje akaingia kwenye gari akaondoka
Mama Robson alihangaika sana pale chumbani lakini hakuweza kufanikiwa kufungua, akaitafuta simu yake ili amwambie Mume wake kuwa Robson ameujuwa ukweli lakini bahati mbaya simu aliiacha jikoni. Brahama alikanyaga Mafuta kuelekea ofisini kwa Baba yake
Akaiacha gari nje ya ofisi akaingia haraka na kumkuta Baba yake akiwa anazunguka katika kiti, akashtuka kumwona Robson
“Robson kuna nini?” aliuliza Baba Robson
“Sylvia amekufa” Alijibu Robson
“Masikini pole sana Kijana wangu, sasa kwanini Mungu ameamua kukupa adhabu kali namna hii?” alisema Baba yake Robson, lakini akaiona Bastola kwenye kiuno cha Robson akajuwa tu Robson ameshajuwa kuwa yeye ndiye aliyempiga risasi Sylvia, akaitumia njia ya Kijeshi kutaka kuichukua Bastola kwa Robson, akawa anamsogelea taratibu huku akimsemesha Robson akashtuka lakini Baba yake alikuwa ameshamfikia lakini kabla hajachukua Bastola Robson aliiwahi akamnyooshea Baba yake
“Kwanini Umemuuwa Sylvia?” aliuliza Robson, Baba yake akaanza kutetemeka huku akisema
“Robson nimefanya kwa ajili ya kukuweka salama, nakuomba Mwanangu weka Bastola pembeni tuongee sisi ni familia moja”
Alisema Baba Robson akiwa anajaribu kusogea tena ili aichukue Bastola, Robson hakutaka maswali wala majibu kutoka kwa Baba yake
Akamtungua Baba yake Risasi ya kichwa, Baba yake akaangukia mezani kisha chini, harakaa Robson akakimbia, akaingia kwenye gari, akaondoa gari kwa kasi sana ili aondoke hapo lakini haraka yake haikuwa na Baraka, wakati anaingia Barabarani akakutana na roli lililobeba simenti, akagongwa ubavu ambao alikuwepo. Robson alifia pale pale.
Vilio vikatanda kwenye familia mbili ambazo ziliwapoteza wapendwa wao, Sylvia, Robson na Baba Robson wakazikwa siku iliyofuata. Mama Robson akasimama kizimbani kutoa ushahidi, Brahama akaachiwa kwasababu hakuwa na kesi ya kujibu.
MWISHO
Ahsante sana kwa kuisoma FUNGATE na mwisho wa Riwaya hii ni mwanzo wa Riwaya mpya hapa Kijiweni usibanduke kwani Mtaa Unaongea na Kaka Mkubwa anausikiliza
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz
FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04
36 Comments
Duuuh mbonaa imwisha haraka hivooo
Jaman nmeipenda, naomben muendlee kutupa mafunzo kupitia riwaya
Boñge moja la simulizi 🔥🔥🔥☑️ nimeenjoy sana😂😂😂
Apaaana sio sawa
Daaaah … Jmn ,…. Mm mbona nltaka iwe vingineee
Asanteee kaka tumejifunza Ving kupitia hii riwaya mung akupe uzima utunge nyingne 🙏🤗
Stor nzur inafunza pia
Funza umewaona😀😀
Daaaaaahhhhh huzuni kubwa sana wa2 wa 3 wanakufa kwa pamoja kiss mapenzi kweli mapenz sio ya kujalibiwa
Umetudanganya #ka mkubwa 😂😂😂😂
Tup muendlz bs ulivytak iwe
Riwaya nzuri ila imekuwa fupi sana jamani
Asante Mungu huyo baba kalipia makosa yake🙏🙏
daaah😢😢😢
Inayofuata ni nini admini??
Riwaya hii imetufunza🙂mengi Sana . Adimini tunaomba riwaya 😀nyingin nzury kuliko
Riwaya hii imetufunza🙂mengi Sana . Adimini tunaomba riwaya 😀nyingin nzury kuliko hii🥳
Mapema mno fungate 🙌😩But kaz nzur saaaana🥰Tunaenjoyy
Mhhhhhhhh!!!!!!!!!!!
Mbona haraka hiv
Funzo kuwa Kam ukifany ubaya kweny hii dunia bas na wewe utalipwa Kwa ubaya huo huo uliomfanyia mwenzako 🤟🤟pia kambla ya kufanya maamuzi ya kuoa watu wawili hao inabid wakae pamoja ili wajuane na waachane na watu wao wa zamani ili kuweza kupunguza migogoro katika familia Kwa ujumla .
ukitenda mema unalipwa mema na the same ukitena mabaya utalipwa mabaya
NB: MALIPO NI HAPA DUNIANI✔️✔️
Admin embu achana na fungate kidogo kuna jambo la kidunia jambo la kiafrika embu mlete Lookman tumuone na Atalanta yake tummwagie maua kijiweni leo tusifanye kazi yoyte zaidi ya Kumwongelea Lookman na Team iloshangaza wengi Atalanta
Admin embu achana na fungate kwanza walete Atalanta na Lookman wao, 😊 kule bayer Leverkusen na Xabi wao😂
pia atuletee na mamaake lookman maana ile hug ya bi mdashi imenikosha waxungu wamekoma..🤣🤣
Ukiwa unaandaa na simulizi za sauti itapendeza pia
Daaaah braham ndo sababu y matatizo yote n yy angeli pewa azab y kujifunz km umke w m2 sumu
Hii ndo maana halisi ya story haitakiwi kuwa nyepesi hata kidogo usimpe mtu nafasi ya ku guess nini kitafutia baada ya hatua moja kwenda nyingine
Alafu nina swali nimeona lipa namba ni kwaajili ya nini wakubwa
Ukitaka kumpa chochote kitu ADMIN
Riwaya ya KOTI JEUSI ndo ilikuwa nzuri sana kuliko hii FUNGATE hukutenda haki kutoimalizia aisee
KOTI JEUSI Iliisha Mbona?
Lete vitu hivyo
Daaaah imeisha kienyeji… Ila kazi nzuri sana admini 🥳🥳🥳🥳🥳🥳… Shusha chuma kingine
Adimin lete story nzuriii såñâä ifunze members kinomaa määñå mapenzi yanaleta conflicts såñâä 🤫🤫🤫🤫🤫🤫🤫🤫🤫🤫🤫🤫.
Mm kwangu story haijaisha naendelea kujisimulia mwenyew… utajua mwenyew admin🥺… story inaishaje hv me naendelea kujisimulia😂😂😂
Hasira hasara ona mama Robson anabaki mpweke 😭😭 msije kupendapenda jmn pendeni kiasi mbn wazuri wapo wengi t xiwezi kumng’ng’ania mtu ambae hanipendi never…
Bonge la story i appreciate it 👊🏽