Ilipoishia “Sylvia akanyanyuka taratibu na kuuelekea Mlangoni ili aangalie ni nani alikuwa akigonga, laiti kama angelijuwa asingeliinuka akaenda mlangoni, Baba yake Robson alitumia maelekezo ya Robson kupajuwa walipo na alikuwa amesimama kuhakikisha anamuuwa Sylvia. Alipofungua mlango kwa kufikiri huwenda ni Mhudumu wa Hoteli alikutana na sura ya Baba Robson ikiwa kavu sana.”
Tuendelee
SEHEMU YA TISA-09
“Babaaaa!!!” Aliita Sylvia, Muda huo huo Baba Robson akafyatua Risasi mbili eneo la moyo wa Sylvia, alihitaji kummaliza ili kijana wake asiteseke tena na Mapenzi. Baada ya kumpiga risasi akakimbiaRobson akatoka haraka bafuni akamuona Sylvia akiwa anatapatapa Sakafuni, muda huo huo Walinzi wa Hoteli wakafika pale na kumsaidia Brahama kumpeleka Hospitalini Sylvia, akakimbizwa Muhimbili haraka ili kuona kama wanaweza kuokoa uhai wake.
Hakuna aliyekuwa akilifahamu hilo zaidi ya Brahama na Baba yake Sylvia
Damu zilikuwa zimetapakaa kwenye shati la Brahama, alikuwa akitetemeka na kujialaumu sana, akiwa hapo Robson alipiga simu. Ikawa ngumu kwa Brahama kuipokea sababu hakujuwa atamueleza nini akaeleweka.
Akaamuwa kuwapigia simu familia ya Sylvia kuwa Binti yao yupo mahututi Muhimbili,, haraka sana Mama Sylvia alifika hapo kumjulia hali Binti yake ambaye alikuwa akipigania uhai chumba cha wagonjwa Mahututi baada ya kupigwa risasi na Baba Robson
“Kimemkuta nini Binti yangu?” Aliuliza akiwa anahema juu juu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza anamuona Brahama ambaye aliifanya ndoa ya Sylvia kuwa Shaghalabaghala kwa siku chache tu
“Mama…Sylvia amepigwa risasi nikiwa Bafuni nikasikia akisema Baba” Mama Sylvia alishtuka sana akamwambia Brahama
“Siwezi kukuamini Mtu ambaye umevuruga kabisa Maisha ya Binti yangu, sikujui hunijui wewe Kijana hebu sema ukweli nini kimetokea kabla sijapiga simu polisi” Alisema, Bahati nzuri pembeni kulikuwa na mlinzi mmoja wa ile hoteli akadakia
“Mama anachokisema ni kweli japo kumjuwa mpigaji ni ngumu sana kwasababu hatukumwona Mtu yeyote pale zaidi ya huyu na Binti yako,” pale pale Mama Sylvia akamshika mishiko Brahama
“Umeniulia Mwanangu si ndiyo? Nakuuliza uneniulia Mwanangu…wewe ni shetani wewe Kijana” Alisema akaanza kumpiga Brahama kama Mtu aliyepandwa na kichaa, Mlinzi akaokoa
“Mama hauna haja ya kushuku kwa sasa kikubwa ni kuangalia afya ya Binti yako namna inavyoendelea vinginevyo utajikuta unapata presha, baada ya hapa kesi itafika kwenye dawati la jeshi la polisi, wao watafanya uchunguzi wao.” Alisema Mlinzi huyo ,
Mama Sylvia akakaa chini na kujiinamiaMuda huo Baba yake Robson alifika nyumbani kwake akiwa
anatokwa na jasho kama Mtu anayekimbizwa, damu kidogo ilimrukia kwenye Shati. Alikutana na Mke wake mlangoni akiwa anataka kuingia ndani
“Baba Robson hiyo damu ya nini?” aliuliza kwa mshtuko mkubwa sana
“Hebu pisha kwanza” AliSema akaingia ndani kwa kumsukuma Mama yake Robson
“Unachokijuwa kibakie kuwa siri yako, sitaki yeyote alijuwe hili tumeelewana? si Robson wala Mtu mwingine” Alisema kwa sauti iliyojaa msistizo sana huku Mama Robson akiwa katika hali ya kushangaa akamuuliza
“Ina maana umemuuwa kweli Sylvia?”
“Ishia hapo hapo, sitaki urudie tena. Sitaki kukusikia ukisema chochote hata Robson atakapofika. Nimefanya hivi ili kumlinda yeye asiharibu Maisha yake” Alisema Baba Robson.
“Umemkosea sana Kijana wako sababu anahangaika kuipata furaha ambayo uneiondoa kwa urahisi sana Baba Robson, Hujaacha Maisha ya kikatili uliyoyapata jeshini?”
“Mama Robson huu uamuzi una faida kubwa sana, hatutosumbuka hata sisi kwa ajili ya Robson tena, atapata Mwanamke mzuri mwenye mapenzi na Kijana wangu…”Alisema kisha akataka kupandisha ngazi kuelekea chumbani
“Itakuwaje kama Robson atapata Mwanamke kama Sylvia, naye utamuuwa?” aliuliza swali ambalo lilimfanya Baba Robson amtazame Mama Robson bila kutoa jibu lolote lile, akapandisha ngazi
Mama Robson akampigia simu Robson muda huo huo akamuuliza yupo wapi kisha akataka kujuwa kama amefanikiwa kujuwa alipo Sylvia, alifanya hivyo ili tu kudadisi kwa kina Kama Kijana wake amepata taarifa ya kutisha kuhusu Sylvia, majibu ya Robson yalimuonesha Mama huyo Robson hajui chochote.
Muda huo huo akampigia simu Mama Sylvia, hakutaka Robson azipate taarifa hizo wakati yupo Njiani kurudi Dar, akajifanya hajui lolote lakini kilio cha Mama Sylvia kilimfanya amuulize tatizo nini, akapewa taarifa hiyo nzito lakini bado hakukuwa na taarifa ya kifo cha Sylvia
“Nakuja lakini naomba Robson asilijuwe hili tafadhali, atachanganikiwa sana maana yupo Njiani anarudi Dar” Alisema Kisha haraka haraka akatoka akaelekea Muhimbili, akasimuliwa vizuri kilichotokea.
Moyoni alijuwa aliyefanya jaribio hilo ni Mume wake kwa ajili ya kumlinda Robson kama alivyosema
“Pole sana Mama Sylvia, laiti kama ningelijuwa haya yote yatatokea ningezuia ndoa ya Sylvia na Robson isifanyike, imeleta uchungu mwingi kwenye familia” Alisema Mama Robson.
Huku akizidi kuumia, akifikiria namna Robson atakavyo changanikiwa hakupata jibu
“Huyu Kijana ni Nani?” Alimuulizia Brahama ambaye alikuwa ameloa damu
“Huyo ndiye aliyekuwa na Sylvia kwa muda wote”
“Ina maana huyu ndiye akiyekuwa kizingiti cha mambo yote?”
“Ndiyo!!” Alisema Mama Sylvia akiwa anazidi kulia. Mama Robson alimtazama Brahama akatikisa kichwa chake sababu alishajuwa endapo Robson atakapokuwa amefika Dar balaa zito linaenda kuibuka
Brahama alikuwa ameketi kama Mtu aliyetengwa na kila Mtu,
Mara daktari alfika na kufanya wote wawe katika hali ya Kumsikiliza
“Tumefanya Upasuaji wa kuondoa risasi mbili ambazo zilikuwa upande wa kushoto, Bado yupo hai ila hajarudisha fahamu zake. Kwasasa jambo la Msingi ni Dua na sala” Alisema Daktari
“Tunaweza kumwona?” Aliuliza Mama Sylvia
“Kwasasa hapana mnaweza kurudi nyumbani sababu yupo katika chumba maalum kwa ajili ya uangalizi hadi pale hali yake itakavyoanza kuimarika” Alisema alafu akaondoka zake haraka.
Brahama akainamia chini maana alijuwa baada ya mazungumzo hayo atakatakaye fuatia ni yeye
“Utasema nini kimemkuta Binti yangu Kijana, haiwezi kwisha katika hali kama unayoifikiria” Alisema Mama Sylvia, Ukweli alikuwa akiujuwa Mama Robson sababu Baba Robson ndiye aliyetaka Kumuua Sylvia
“Mama Sylvia!!” aliita Mama Robson
“Ndiyo ni lazima atasema, tena atasema mbele ya sheria” Mara wakaingia polisi wakamkamata Brahama, akawa anawaambia polisi kuwa hakumpiga risasi Sylvia
“Kama hukumpiga basi utakuwa unamjuwa aliyempiga risasi si mlikuwa wote, alafu kwanini ukae na Mke wa Mtu Hotelini? hilo ni kosa namba moja na ndiyo Mzizi wa hili linaloendelea” Alisema Askari polisi akiwa amemshikilia Brahama
“Tutakutana kituoni” Alisema Askari huyo kisha wakaondoka na Brahama kuelekea kituo cha polisi
“Una uhakika kuwa yule Kijana ndiye aliyemdhuru Binti yako Mama Sylvia?” alihoji Mama Robson huku akitamani sana amueleze ukweli Mama Sylvia ili Brahama asihukumiwe kwa kosa ambalo hakutenda lakini alijikuta akiwa mzito sana kusema chochote anachokijuwa
“Amekaa na Binti yangu Hotelini kwa siku zote hizo, amesababisha madhara kwenye familia yangu….na
yako…unawezaje kukosa kumhisi yeye?”
“Sina maana asihisiwe lakini mbona alishazungumza na Robson kuwa akirudi atamuacha Sylvia, inawezekana vipi ampige risasi alafu amlete Hospitali na akupigie simu wewe? aliweza kufanya unyama akamuacha Sylvia Hotelini” Alisema Mama Robson akiwa anaumia ndani ya moyo wake. Angalau Mama Sylvia maneno yalimuingia akakaa kimya
- โขโขโขโขโขโขโขโขโขโข
Saa tano Usiku, Jiji la Dar liliwapokea Mark na Robson wakiwa wamemshikilia Mage. Hakuna hata mmoja kati yao ambaye alikuwa na taarifa ya kilichomfika Sylvia, walienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Baba Robson, wakaingiza gari ndani.
Baba Robson alikuwa ameketi Sebleni akiwasubiria, Mara Mama Robson naye akaongezeka pale Sebleni baada ya kusikia ngurumo ya gari na purukushani za kufunga na kufungua geti, alitazamana na Mume wake, Kisha akamkimbilia Robson na kumkumbatia kwa uchungu.
“Mama Usijali kila kitu kitakaa sawa hivi karibuni, nimekuja na Mage” Alisema Robson, akaketi Usawa wa Baba yake
“Baba na Mama, poleni kwa kuwaingiza katika hili najuwa hamkustahili usumbufu huu” Alisema Robson, akamtazama Mark kidogo akaendelea
“Kesho ni siku ya kutamatisha kila kitu kwasababu Brahama yupo tayari kufanya makabidhiano, anipatie Sylvia ili nimpe Mage. Naamini kila jambo linaenda kukaa sawa” Alisema, Baba
yake akakohoa kidogo, alikuwa hana taarifa kuwa Sylvia bado anaishi kwani hata Mke wake hakunweleza chochote sababu alijuwa kufanya hivyo kunaweza kuzua taharuki zaidi.
“Hilo ni jambo ambalo tulikuwa tukilisubiria Mimi na Mama yako, tunaamini kesho itakuwa ni siku bora sana kwako Mwanangu” Alisema Baba Robson kama hakuna kilichotokea vile,
alifanya hivyo ili asiwe sehemu ya mshukiwa wa moja kwa moja, wakalala hadi kulipo pambazuka
Robson akampigia simu Mama yake Sylvia ili waambatane pamoja kuelekea Ocean view, lakini Mama Sylvia alianza kulia kama unavyojuwa Mwanamke hasa Mama ni ngumu kuvumilia maumivu ya Binti yake
“Mama unalia nini wakati leo tunaenda kumpata Binti yako?” aliuliza Robson, Mark akaingia akakuta Robson anaongea na simu
“Kwani Mama yako hajakwambia chochote Robson, Sylvia yupo Hospitalini tokea jana. hali yake siyo nzuri” Robson alishtuka sana, kwanza kujuwa kuwa Mama yake alimficha jambo pili alitaka kujuwa nini kimemsibu Sylvia Mwanamke ambaye anampenda sana.
“Sylvia amepigwa risasi akiwa Hotelini” Macho yakamtoka Robson, akadondosha saa aliyokuwa anataka kuivaa
“Amepigwa risasi? yupo hai kweli?” Alihoji akiwa na wasiwasi huwenda Sylvia akawa amekufa. Chozi likawa linamvuja taratibuu
“Robson! nimechanganikiwa sana sijui nifanye nini, Sylvia yupo hai lakini mahututi hajitambui”
“Brahama ndiye aliyempiga risasi, Okay!! yupo Hospitali gani?” Aliuliza Robson, akaambiwa ni Muhimbili, akakata simu akataka kutoka lakini Mark alimzuia
“Kuna nini Robson?”
“Sylvia amepigwa risasi na Brahama yupo Hospitalini” Alisema Robson
“Unamaanisha?..”
“Hivyo ndivyo ilivyo amekiuka makubaliano, nakwapia Mark kama Sylvia kitamkuta kibaya namuuwa Brahama” Alisema kisha akamsukuma Mark akatoka, akapita sebleni akamkuta Mage akiwa hapo
Robson akasimama na Kumtazama kwa hasira huku akiwa anavuja mchozi, Mara Mama yake Robson akaingia Sebleni na kumkuta Robson akimtazama Mage kwa hasira huku akivuja mchozi
“Robson!” akaita Mama
“Unataka kusema nini Mama?” Aliuliza Robson
“Kuna nini? si mmekubaliana kila kitu kwanini unalia sasa…”
“Nalia kwasababu Mama yangu ni mnafiki, Muongo na mficha siri…Hivi Mama ulikaa kimya wakati Sylivia yupo Hoi Muhimbili akipigania uhai wake, kulikuwa na sababu gani kunificha jambo lenye maana kubwa kwangu?”
Mama Robson akainamia chini huku Robson akizidi kuzungumza kwa hisia kali sana, ndipo Mage aliposhtuka na kumuuliza Robson
“Sylvia yupo Muhimbili? kimemkuta nini?” alihoji kwa Mshangao mkubwa akiwa anasimama
“Unashamgaa nini, unafikiria naweza nikakuamini tena Mage? Wewe na Brahama ni kitu kimoja alafu unajifanya hujui si ndiyo….Brahama amempiga risasi Mke wangu wakati tulikubaliana, kama Sylvia kitamkuta kibaya Nakuuwa wewe”
Alisema Robson kisha alitoka kwa hasira akaingia kwenye prado akaondoka hapo akaelekea Muhimbili ambako Sylvia alikuwa akipigania uhai wake.
Akampigia simu Mama yake Sylvia kisha akaelekezwa mahali ambapo Mama huyo alikuwepo, Kwa mwendo wa Haraka sana Alisogea hapo akaonana na Mama Sylvia
“Mama,, Sylvia anaendeleaje?” alihoji
“Hali yake bado haijakaa sawa hatuwezi hata kumuona tangu jana Robson” Alisema Mama sylvia kisha chozi likamdondoka
“Brahama yupo wapi?”
“Amekamatwa na Polisi jana, yupo kituoni”
“Kwanini amempiga risasi Sylvia wakati tulikubaliana kilakitu kiishe leo?”
“Hata Mimi nimeshindwa kupata jibu Robson, nimejiuliza kwa muda mrefu hadi akili imechoka. Brahama anasema hakumpiga risasi Sylvia bali alisikia Sylvia akiita Baba kabla ya kusikia mlio wa Risasi, inakuwa ngumu kumwamini sababu yeye ndiye chanzo cha matatizo yote haya” Alieleza Mama Sylvia
Akamshika Robson ili waketi wazungumze
“Ilipofikia Robson sioni kama unaweza ukamfurahia Binti yangu, Baba yake pia hataki kumwona Sylvia. Hata alivyosikia alisema ni bora afe tu” Alisema Mama Sylvia wakiwa wameketi
“Mama Mimi naamini Sylvia alitereza mahali, bado ananipenda sababu Mimi ni Mume wake hawezi kulisahau hilo….na kuhusu Baba yake nafikiri ni hasira tu sababu ya maumivu ya Mguu”
“Sidhani Robson, Hata familia yako haiwezi kumpenda tena Sylvia. Nikushauri tu achana na Sylvia..” Alieleza kwa uchungu sanaa Mama Sylvia, Robson akamwambia Mama Sylvia
“Wakati nafanya maamuzi ya kuwa na Binti yako ilikuwa ni Mimi na moyo wangu, sitajali hata kama Familia itanisusia” Alisema Robson, Mara akaingia Daktari ambaye tangia jana alikuwa akimtibia Sylvia
Wote walisimama kumsikiliza, akavua Gloves kisha akawaambia.
“Poleni sana, Bahati mbaya muda mchache uliopita Sylvia amefariki” Alisema Daktari huyo, Mama Sylvia akaanguka palepale. Robson akamdaka huku chozi likiwa linambubujika
“Dokta Sylvia amekufa?” alliuliza akiwa anatokwa na mchozi
“Pole sana Kaka kazi ya Mungu haina makosa” Alisema Daktari huyo kisha aliwaita manesi kwa ajili ya kumsaidia Mama Sylvia ambaye alikuwa ameishiwa nguvu, Manesi walimchukua MamaSylvia hadi kwenye wodi kwa ajili ya matibabu
Mlango wa chumba alichotokea Daktari ulikuwa wazi, macho ya Robson yalikita huko, akajkuta ananyanyuka hadi ndani ya wodi hiyo ya uangalizi maalum, akakuta mwili ukiwa umefunikwa juu ya kitanda, akaufunua taratibu akamuona Sylvia akiwa amelala hapo, nguvu zilimuisha Robson hakuamini kama kweli Sylvia alikuwa amekufa, chozi la maumivu lilimbubujika akasema
“Haikuwa njia nzuri ya kuniaga Sylvia, nilipambana kukurudisha, nimefanya vyote…..Nawe umenilipa Kifo si ndiyo!” Maneno haya yaliwaumiza hadi manesi waliopo kwenye chumba hicho, pete ya ndoa ilikuwa kidoleni kwa Sylvia
Wale manesi walimuondoa Robson kwa nguvu pale wodini sababu maumivu aliyokuwa nayo yasingeliweza kupoa haraka na pengine yangemletea maumivu zaidi.
“Niacheni nikakae na Mke wangu Mimi” Alisema Robson kwa uchungu lakini Manesi walihakikisha wanamtoa kabisa hadi nje, wakamuacha akiwa emekaa kwenye korido
Kama kuna siku Robson aliumia, alilia basi ni siku hiyo. Alilia sana kama Mtoto mdogo akitokwa na makamasi, kila alivyokumbuka namna alivyohangaikaa Mwanza kwa ajili ya Sylvia alizidi kulia, dakika chache baadaye kilio kilikoma, hasira zikajaa kwenye kifua cha Robson, Kichwani akawa na jina moja tu la kulifanyia kazi, si lingine bali Brahama, aliamini Brahama alikuwa amempiga risasi na kusababisha kifo cha Sylvia.
Akanyanyuka na kukimbilia kwenye gari, akawasha kisha akaelekea nyumbani kwao. Akamkuta Mama yake akiwa nje, akampita mbio hadi chumbani kwa Baba yake, akavuta droo na kutoa Bastola ya Baba yake ambayo laiti kama angelijuwa kuwa ndiyo iliyotumika kuondoa uhai wa Sylvia sijui ingekuwaje?
Mama yake akamzuia Robson akamuulzia
“Una kichaa Robson, unaenda wapi?” alihoji Mama Robson, kwakuwa alikuwa mwanaye tu ndiyo maana aliweza kukaa karibu naye lakini jinsi alivyo na hasira ilikuwa inatisha sana.
“Ndiyo nina kichaa kwasababu ua langu limenyauka mbele yamacho yangu, aliye nifanya nikakosa raha katika Maisha yangu ndiye atakayelipa gharama ya maumivu yangu” Alisema Robson
“Robsson kuna nini hasa?”
“Sylvia amekufa Mama, nina raha gani kwasasa, nina thamani gani? siwezi kumwacha Brahama”
“Una hakika ndiye aliyempiga risasi Sylvia, Robson mbona unataka kuniacha na Mimi? nilikwambia mwisho utakuwa mbaya”
“Brahama atalipa gharama ya damu aliyoimwaga kwa Sylvia Mama nipishe….” Maneno haya yalimfanya Mama Robson ashindwe kuvumilia, alifikiria anachoenda kukofanya Robson kinaweza kuleta matatizo zaidi sababu Brahama yupo polisi, na kama ataenda polisi basi atauawa na polisi kabla ya kumfikia Brahama
“Robson Mimi namjuwa aliyempiga risasi Sylvia lakini siyo Brahama” Ilibidi aseme Mama Robson huku akimwaga chozi la haja
Robson alijawa na mshangao kumsikia Mama yake akisema kuwa anamjuwa aliyemuuwa Sylvia, alishusha munkari kisha akamuuliza Mama yake kwa utaratibu sana
“Unamjuwa aliyempiga risasi Sylvia?”
“Ndiyo Namjuwa, Robson Naona aibu siku nikifa na siri hii ambayo inaweza kuleta taharuki kubwa kwako Mwanangu” Alisema kwa sauti iliyojaa kilio
“Nani aliyempiga risasi Mke wangu?” Aliuliza Robson
“Nakuomba Robson nikikutajia kaa chini ufikirie nini ufanye lakini usikurupuke na hasira utafanya maamuzi magumu, nakuomba weka Bastola chini” Alisema
“Mama huwezi kuniondoa katika njia yangu, najuwa aliyempiga risasi Sylvia ni Brahama sababu yeye ndiye aliyekuwa na Mke wangu, hakuna Mwenye uadui na Mke wangu” Alisema
“Si Brahama….” Alisema Mama Robson akafuta chozi akamwambia Robson
Nini Kiliendelea? Robson atamuua baba yake? ย Usikose Sehemu Ya Kumi Mchangie Kaka Mkubwa Ya Bando Kwa
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoย kijiweni.co.tzย unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiย editor@kijiweni.co.tzย ย
FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04
ย
21 Comments
Hakuna siri ya wawil ๐๐, wanaphys… Watusaidie force ya mapenz unaicoolije na formula kabs hii ni hatar ๐
Duh mamb yanazd kua mamb
Duuh mamb si mamb tena maskini robson haelew kitu,wanawak mungu atusaidie tutafik mbinguni tumechok๐๐๐
Hahahahaa tena tumechoka sanaaa
We admin acha uchoyo leta vitu mbn unakata radhA leta Cha 10 ๐ค๐ค๐ค
Duuuh pagumu hapo Baba kafanya maamuzi magumu San kama mwanae sijuh atakavyo ambiwa sijuh atafany mini๐๐
Aah jamniiiii mbon ctor inahuzunisha tn
Ni motoo
sio kweli bhn adimin unaktisha utamuโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅ
Kumekucha haswaaaa,itakuaje robi akijua ni bba yake katenda unyama huo? Na je brahm ataachuwa hulu? ๐ฒ๐ฒ๐ฒ๐ฒ๐ฒadmn umeniacha njia panda bola ungeweka na inayo fata hata asubh tuu๐๐๐
๐๐๐ wuuuh hii ndo ile ukija bila guard nagawa wastani kwa idadi ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Huyu mama nae anzngua… Anamchomeshaje mmewe …. Angekaushaaaaa … Wangelua msiba basiiii
Mama Robson apewe maua yake kama atasema ukweli kwa mwanae ,na hata ningekuwa mimi nisingekaa na siri mbaya kama hii hasa kwa mwanangu wa pekee,na kina baba wa aina ya baba Robson hawafai kabisa katika maisha haya,waache kuingilia mapenzi ya watoto wao ili hali wakijua watasababisha maumivu makali mioyoni mwa watu wasiokuwa na hatia,I HATE DADDY’S ROBSON!!! I HATE HIM ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ yaani ingekuwa mume wangu nisingemuacha aishi hata kama mwanajeshi,uanajeshi wake apeleke huko kwenye dustbin ๐ ๐ ๐ ๐
Mama Robsaon anataka kuchana mkeka
Hahahaha ๐ ๐
Mzee wa Rob hajakosea saaaanah,,,๐ค๐ค kiMovie-movie hajakosea saaaanah,,,
Maana Sylivia mwenyew ndo hovyo kabisa,, umeona alichofny kw baba yake lkn๐
Dah! Ya moto sana,, yani kama na mimi ni muhisika vile!!!
Kama nawaona Liiiiiiiiive bila chenga,,,
Admin โ๏ธโ๏ธโ๏ธ๐๐๐๐๐๐
Ni hatari na nusu
Mama rob anazinguaa angesubir hat msiba upite kwanza
Kweli hii kali mzee kauwa kutetea moyo wa mwanae ilihali mwanae anapagawa kwajili ya huo mwanamke
Inamfanya atake kufanya vitu ambavyo vinaweza ata kugharimu maisha yake pia
Admn uwe unaweka vipande viwil kwa siku maan story n ๐ฅ๐ฅ
Duuuh kazi IPO