Ilipoishia “Nisamehe kwa yote yaliyotokea! Lakini hakutaharibika kitu! Najua unagopa Bibi atakutafuta! Ila nimewaambia umeenda chuoni utarudi jioni! Na leo utashinda chumbani kwangu halafu jioni nitakutoa naimani utakuwa sawa!”ย
Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINIย ย
Majira ya jioni Jolvin alifanya Kama walivyokubaliana na Gorii, alitazama mazingira ya pale Kama kupo salama Kisha alimtoa Gorii Chumbani kwake akampeleka ndani kwake!
Alirudi Chumbani kwake kisha alijitupia kitandani na kuchukua simu yake akimpigia Esau.
ย ย ย “” Yaani Kaka mkubwa! Leo najisikia kuwa na furaha Sana! Kale katoto bhana kana akili za juu juu ila kapo Safi! Unajua nataka tuanze vikao vya harusi mapema nataka nikamiliki mazima!””
“” Si nilikwambia unagopa bure tu! Vipi mama mideko unampeleka wapi!? Mama wa Jovii… Anakupenda yule!!?”
“” Ni Kama rafiki tu kwangu! Na sijawahi kuwa na Mawazo nae tofauti !”
“” Okay! Mimi nishaongea na Joely pamoja na Rich! Ajabu Rich nae anataka aoe siku hiyo hiyo amchukue Sophia!”
“” Bado mdogo bhana! Yaani yeye mwanaume lakini akili yake Kama ya Gorii Sasa huyo mke atammeneg Kweli?”
“” Baadae bhana ngoja nifanye kazi za maboss hapa! Wewe sahii si unasubili ajira tu! Halafu mbona hujaenda dukani kwa Bibi!? nikija huko nitaangalia ila kumbuka kuulizia usia wa Mama Gorii tujue imekaaje pale!”
“” Wewe si nimekwaambia nilikuwa na msala na Shemeji yako! Jioni nitamfata Bibi! Anajua nimetoka nafatilia mambo ya kazi.
Jolvin alikata simu huku akifikilia jukumu alilokabiziwa na Mama Gorii, alimpigia simu Mamake apate majibu lakini alimjibu yupo busy kwanza!
Mida ya jioni jioni wakiwa wamekaa pale sebuleni, alikuwa ni Jolvin akimuelekeza Gorii jinsi ya kutuma maombi ya kazi.
Ghafra mlango ulifunguliwa kwa kasi sana, walishituka wote kwa mshangao alikuwa ni Anelisa katia timu huku kashikilia picha zikimuonesha Gorii na Jolvin siku yenyewe wakiwa wamekaa sitaili za wapendanao, Alifika akazirusha mezani zikawa zimesambaa meza nzima, Alianza kupandisha sauti huku Gorii akibaki kutetemeka kwa woga!
ย ย ย “” Jovii… Kumbe umefanya yote kwa sababu ya Gorii! Kila mara nimejaribu kukuoneshea hisia zangu hutaki kuzisikia kabisa! Muda wote nimekaa kukusubili wewe lakini leo ndio umenifanyia ukatili kiasi hiki.. Jovii… Mbona lakini unaiaibisha familia yangu siku zote! Nmekataa wanaume wangapi wenye hadhi kukuzidi hata wewe, sababu yako tu nimekuganda! Ona leo unavyoenda kuurarua moyo wangu!ย
Anelisa alizidi kulia huku akimsogelea Jolvin Kisha alimkumbatia akizidi kumwaga machozi mgongoni kwake.
Gorii Alibaki akishangaa huku moyo ukianza kumuuma, aliamua aondoke angalau akalilie Chumbani ile anageuka tu Jolvin alimshika mkono, huku akimpatia ishara asiondoke lakini kwa Gorii akawa Kama kamchochea aongee japo pale alikuwa Kama anataka kujizuia asiseme kitu.
ย ย ย “” Kaka White… Siku zote huwa unachukulia simple simple tu! Nilikwambia Anelisa anakupenda wewe, wewe huwa husikii anavyolalamikaga muda wote ni Joviii.. Joviii wewe hujui anakupenda!?
Jolvin alimkata jicho lilimpa majibu abaki kimya Kisha alimshika mkono Anelisa akampeleka Chumbani kwake akafunga Mlango.
ย ย ย “” Anelisa unajielewa kwelii.. lini Mimi niliwahi kukufungukia wewe kuwa nakupenda? Lini nimeijulisha familia yangu au yenu nikatangaza kuwa Mimi na wewe tuna mahusiano!? Please Anelisa hupaswi kuongea vile mbele ya Gorii kajisikia vibaya Sana! Isitoshe hata Gorii analitambua hilo kuwa wewe sio mtu mzuri kwangu pamoja na familia yako kwa ujumla! Siku ile ulipanga mipango gani pindi unaniomba nikuletee dawa chuoni! Si ulitaka nikifika uniwekee madawa ya kulevya nilewe ili nitembee nawe! Na asingekuwa Gorii kuleta maigizo yake kuwa anaumwa leo ningekuwa nimedumbukia kwenye shimo nisiloweza kutoka! Vipi kumtesa mtoto wa watu ukamlipa yule Askari amfanyie ukatiri? Huna hata huruma mtoto wa watu amebakiwa na alama kwasababu ya roho yako mbaya! Anee…ย Mbona unapenda maigizo Sana!?
Jolvin alimaliza kuongea mpaka mwili wake ukawa unatetemeka kwa hasira! Unaambiwa Omba Sana usikutane na mtu mpole akachukia siku hiyo itabaki mbaya kwako.
ย ย ย “” Lakini Joviii…..!!?”
ย ย ย “” No.. Anelisa nimechoka maigizo yako! Naomba ondoka kabla sijachukua maamuzi siyo!”
Jolvin alimshika mkono akamtoa nje Kisha alifunga mlango akaanza kujirusha rusha kitandani kwa hasira!
Huku Anelisa alifika sebuleni alimkuta Gorii kabebelea mabegi aondoke, baada ya kumuona Anelisa ilibidi asimame kwanza.
ย ย ย “” Anelisa.. tuondoke tu humu Ndani! Jolvin mwenyewe ndio haeleweki sijui anampenda Nani? Nisaidie kubeba begi zangu nitaenda kutafuta nyumba za kukaa nje!”
Anelisa Alibaki akimtizama Gorii akaona nae anamletea maigizo aliyapiga teke mabegi yote yakaanguka chini.ย
Jolvin alitoka kuangalia kinachoendelea pale ilibidi amshangae kwanza Anelisa Kisha alikaa kwenye kiti.
ย ย ย “” Nyie piganeni bhana! Mabegi yamekosea Nini hapo!?”
Gorii alimtizama Jolvin kwanza Kisha aling’ata midomo kwa hasira akamgeukia Jolvin amtwange ngumi ya pua, Jolvin akawahi kumdaka Kisha akaurudisha mkono.
ย ย ย “” Nipige huku naona sio kwa kuniibia ibia! Mimi sio muwindwaji!?”
Baada ya Anelisa kumaliza kusasambua pale Jolvin alimsogelea Kisha akamkamata mkono.
ย ย ย “” Nimekwaambia sitaki kukuona humu Ndani! Halafu sitaki ufike nyumbani uniletee Drama zako hukawii kuja na familia yako nyumbani.
Gorii Alibaki akimtizama Jolvin asiamini ni Kama anaweza kumtetea vile mbele yake! Anelisa aliondoka kwa hasira huku akipigiza miguu yake chini Kama kakosa nafasi ya kushindania umisi.
Jolvin Alibaki amemshikiliaย Gorii mkono! Alisimama akaanza kukusanya zile nguo huku wakiwa wanasaidiana kwa pamoja! Baadae walirudisha nguo ndani. Gorii alikuwa bado akimtizama Jolvin jinsi alivyobusy kukunja nguo, Jolvin nae anainua kichwa Kisha alitabasamu kwanza akaongea.
“” Mimi na wewe tuliandikiwa tuishi pamoja! Kama utakimbia mbali na mimi! Mimi sitaweza kuishi bila wewe!”
Gorii alitabasamu huku akiangalia pembeni, hutaamini katika kuongea kwake kote lakini wakiwa faragha na Jolvin huwa anashidwa kuongea kitu zaidi ya kutabasamu na kucheka.
Jolvin alimsogelea karibu Kisha alimuwekea mkono wake kwenye bega akimwegamia.
ย ย ย “” Najua unahamu ya kujua kuhusu maneno aliyoongea Mamako siku yenyewe ila leo majibu utayapata! Kazi hii nimemuachia mama, tayari kanitumia ujumbe kuwa anae majibu!
Gorii Alibaki ametoa jicho asiamini, aliamua kumkumbatia kwanza Jolvin, baada ya furaha kuisha ndio anakumbuka kumbe alizidisha mazoea na muda huo yupo mikononi kwa Jolvin! Aliijiengua haraka mpaka Jolvin akabaki kumcheka.
Usiku huo wakiwa mezani mama alianza kuelezea majibu aliyoyapata.
Mishoki alikuwa na rafiki yake Kama mnamfahamu Mr. Shejoh! Ni mfanyabiashara maarufu hapa Nchini! Miaka ya nyuma aliomba kuwekeza Shea katika kampuni yetu wakawa wameshindana na Mishoki akaamua kujiengua katika biashara!
Sitori yake ya maisha anae familia yake inakaa nje ya nchi huku alikuja kibiashara tu! Alifikia kwenye hotel moja kipindi hicho akiwa bado ni kijana katika kutembea tembea ndio alikutana na Mama Gorii yeye akiwa bado ni binti mdogo walianzisha urafiki baadae yakazaliwa mahusiano ndani yao, mwisho kabisa alimbebesha mimba ya Gorii. Muda huo Mama Gorii alikuwa kachukuliwa na familia moja iliyokuwa ni rafiki wa familia yake kumsomesha kutoka kijijini.
Wazazi wake baada ya kugundua hilo walimkemea vibaya asirudi nyumbani tena! Alimtafuta Mr. Shejoh akawa ameikataa ile mimba! Lakini aliondoka huku akisema “” Naamini hii mimba nimembeba mtoto wa kike hata akizaliwa nitamuita Goryanah atakuwa ni mpambanaji siku zote daima atauchukia umaskini, nitakaa mbali na familia yako hata yeye nitamtenga mbali na wewe hautakuja kumuona kamwe labda mtoto ndie akutafute na sio Mimi” aliweka Ni Kama kiapo.
Mama Goryanah aliamua kujitenga na ile familia ndipo alipohamia kijijini ambako alikokuwa akikaa mpaka Sasa, aliamua kubadilisha mfumo wa maisha akaanza maisha ya kawaida Sana kwa kujichanganya na kile Kijiji, alimlea mwanae mpaka akakua na hakuwahi kumwambia kitu chochote kuhusu maisha yake ya nyuma! Aliamua kufutilia mbali familia yake pamoja na mzazi mwenzake na ndio maisha aliyomlelea binti yake!
Mama alimaliza kuongea huku kila mtu alikuwa kimya akimuonea huruma Mama Gorii kwa maisha aliyoyapitia ila kila mtu alibaki kushangaa maamuzi yake aliyoyachukua.
Gori yeye Alibaki akilia kumbe Mamake alipitia maisha magumu kiasi kile, Jolvin alimuuliza mama kuhusu Mr. Shejoh watampata vipi?”
Gorii alikohoa kwanza Kisha alifuta machozi akaongea..
ย ย ย “” Mamangu hakutaka Mimi nijue familia yangu! Kuhusu Baba hakutaka kabisa amsikie! Kama angekuwa ni Baba anataka amuone binti yake angenitafuta? Hapa inaonesha hata huyo Mr. Shejoh hakutaka kusikia kuhusu Mamangu pamoja na mwanae! Mimi naona iwe hivyo daima! Sitaitafuta ile familia iliyomkana Mamangu wala familia ya Mamangu.
ย ย ย Siku zote watu unaoishi nao vizuri hao ndio familia yako ya Baadae! Naamini katika hili familia yangu itakuwa ni Mishoki Family nami nitasimama kwa niaba ya Naina katika nyumba hii kamwe sitaikimbia, nitabaki na Kaka white nitampambania pia kufikisha malengo yake! Namimi nitapambania Duka la Bibi, Daima nitatoa Ushirikiano kama mwanafamilia tenaย nitasimama Kama mkamwana wa hii familia!
Gorii alimaliza kuongea Kisha aliwahi kumkumbatia Mamake huku akilia kutoa maumivu ya nyuma na, kuanzisha familia mpya ndani ya moyo wake! Alienda kumkumbatia Bibi tena kwa furaha huku akimuahidi hatomuacha tenaa.
Alimaliza akamgeukia Jolvin ambae alikuwa ametulia akizani amesahaulika, aliishia kutabasamu tu asifanye chochote! Jolvin akawa amejiongeza alifanya kumkumbatia huku akimuachia asikie neno kutoka kwake make kila mtu aliongea nae!”
Gorii alimtizama huku akiwa anamuonea aibu alimuita kwanza.
ย ย ย “” Kaka White.. Mjukuu wa Bibi. Siku ile ulivoingia ndani nilianza kukuita haya majina kabla hata sijakuona! Ila umeendana nayo kweli make wewe ni msafi wa moyo Hadi nguo zako ni nyeupe nahisi hata unae moyo wenye rangi nyeupe!”
ย ย ย “” Kwahiyo..ย
ย Jolvin alimhoji.
ย ย ย “” Kwahiyo Nini tenaa..? Maswali uliyokuwa ukiniuliza siku ile twacheza yalinitoa jasho Kweli!! Ila leo nayajibu kumbe nilitakiwa kusema ” ndio” namaanisha nipo tayari kuolewa na wewe!”
Jolvin alimpigia makofi, Mama na Bibi nao wakafatia wakifanya vilevile. Gorii Alibaki kuwashangaa nae akaliunga kufanya vilevile, mwisho kabisa Jolvin aliongea.
ย ย ย “” Daima Gorii huwa anajipongeza kila mara akifanya vizuri katika Jambo lake, Nasi leo twaungana kufanya vilevile Gorii huwa anafanya baada ya kushinda! Na mwezi kesho tayari kwa Ndoa make kila kitu tumeshakiweka sawa! Ndoto ya Mama Jolvin kumuoa Gorii Sasa inaenda timia na hakutakuwa na mbambamba tena. Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yakoย ย
ย ย ย ย ย ยถยถยถยถยถ MWISHOยถยถยถยถยถย
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Stori Nyingine Kwa Kumtumia Chochoteย
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoย kijiweni.co.tzย unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiย editor@kijiweni.co.tzย ย
Ulipitwa naย SIMULIZI NYINGINE?ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
41 Comments
Imeisha km bado inaedelea
Nzur sana
Hello ndugu admin tunaomba goryanah basi na sisi tuendeleze mzigo Kila nikichungulia kijiweni nakuta mikeka TU me haipandi jamani
Nzurii Sana Mungu abarik kazi ya mikono yak๐
Admin anelisa amejinyonga au …?
๐๐๐๐
Cjawai soma stry zako ila ndugu una stry kali xna ww umetisha mungu akupe nguvu za kuleta simuliz nzr
Mbona kama bado inaendelea vileee au kuna season two……ni nzuri sana
Iwepo tu
โค๏ธโค๏ธโค๏ธโค๏ธโค๏ธ 100%๐
Ndugu mwandishi umetuacha hewani, tafadhali iendelee kidogo ๐
Ndugu muandishi hii mbon km inaendelea malizia na sherehe kidogo jmn nimeipenda bure ๐ฉธโค๏ธโค๏ธโค๏ธ๐ฅฐ๐ฅฐ๐
Mwenyewe Mungu akubariki Sanaa asantee Kwa kutupa burudani isiyokifani
Daah.. nakoss cha kuandika ila ni mwandishi… be blessed ๐
Adimin story unatunga mwenyew mana watu mda wote tunachungulia kuna k2 gan kpya mana kila story nzur
utan kama utan ikawa kwel jmn๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
mwandishi unajua ety
Ndugu admin, leta Goryana part II, umetuacha hewani hatujashuhudia kama huyo jamaa aliyeshea na Mishoki biashara kama walimpata, hatujashuhudia pia ndoa ya Gorii na jovii, na bado hatima ya anelisa hatujaiona. ๐๐
Nzuri Sana natamani isinge Isha ila lililo na mwanzo basi mwisho ni njia ifatayo.
Admini tunasubiri nyingne tupe na beading…โ
Tamu mpaka kumoyo hongera ndugu mtunzi hakika una kipaji
Adimin una baya
Namuona Anelisa anachukua maamuzi magumu
Adimin story unatowaga wap mana unafnya mda wote tupo online kusubilia story mana una story mby yan ikiwezeka leo tuanze na nyengine
Oooooh jaman ata ingeendelea tumuone na mtoto wa Kaka White na Goryanah ๐๐
Hongera Kwa kazi nzr na Kwa kutufunza pia hongera sana upewe ๐น yako
nzuri
Tumpe ADMIN Maua yake hajawahi kosea ๐๐ฝ๐
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
Tunataka part 2
Aisee natamani kujua maisha baada ya ndoa Goriyannah na kaka white yalikuwaje walipata mtoto kwa operation au Anne je
Ni tamu story ๐
Story nzuri sana.
Admin upewe mua yako kazi nzuri sana.๐
Story nzuri Sana..
Ila anelisa Sasa
Alaf Gorii alibadilika akaacha akil za juu juu au,,,, ,
Hii bado ina muendelezo
Sema imeshia katikati.
Waoooow kama vile naitazama yaan
Ilinifanya nikiwa board naenjoy sana๐ค๐๐น๐ฟ
next mbona kama haijaisha hivi
Mwandishi hongera kwa kazi yako ni nzuri sana
Jaman mi nilitaka iendelee Jaman nzuri sana hadi chozi limenitoka
The story wร s so fantastic and life lesson container
Jamaniii imeisha ishaje ndo kwanza inanoga
Duuuh story nzuri sana hii
Kumb every good time has a sorrow moment inside it
Kwwli naamin,
It’s very interesting ๐๐๐๐๐๐๐
Story nzuriiii,tunaomb bc hata muendelezo make inaonekana kama vile bado inaendeleaa