Ilipoishia ” Watu wote walipiga kelele huku wakifunga macho! Wasiamini tukio linaloenda kutokea! Ilisikika sauti ya break lakini kwa pembeni kuliruka damu Hadi kwenye gari! Kisha ukimia ukafata Kama dakika kumi kila mtu akiwa ametulia huku kainamisha kichwa chini haaamini kilichotokea.ย
Endeleaย
SEHEMU YA KUMI NA NANEย ย
Gorii ndio wa kwanza kuzinduka, alivuta mkono wake akahisi mzito! Ndio anageuka vizuri! Anakuta pembeni yake kunae Jolvin kaugandamiza ule mkono japo unatoka damu, alivyomtizama vizuri Jolvin alikuwa akimtizama Kisha alimuuliza.
ย ย ย “” Upo sawa Goryanah! Nimemuona mamako! Kweli mmefanana Sana kwa kila kitu! Ulivyomsifia ana nywele ndefu Kama zako kumbe hukuongopa!? Mtizame mama kwanza!”
Jolvin alimaliza kuongea vile Kisha alianza kukohoa huku akitoa Damu mdomoni! Gorii ndio anageuka upande wa pili ndio anamuona mamake sura yake ilikuwa imebadilika Sana hata ile rangi ya usoni ilikuwa haipo tenaa! Mwili wake ulikuwa umedhoofika kwa vidonda vingi!
Gorii alivyomuona alianza kulia upya Kisha alimkumbatia Mamake, unaambiwa Mama ni Mama hata watu wote wangemkataa ila kwako hubaki kuwa mama tu!.
ย ย ย “” Mama ulikuwa wapi lakini? Nilikutafuta muda mrefu sikukuona! Nilitoa Hadi yale matangazo! Lakini hukupatikana!? Uliishije huko ulikokuwa lakini!? Tayari ile nyumba yetu nishakujengea sahii tukitoka hapa tunaenda kuishi maisha mazuri! Hatutakuwa duni tena Kama hapo awali tunaenda kuishi maisha ya kati! Na wewe ulinikumbuka lakini huko ulipokuwa!?”
Mama alimkumbatia Binti yake ni Kama miaka minne imepita pasina kumuona leo anamuona! Alimfuta machozi Kisha alimuuliza.
ย ย ย “” Huyo kijana Ndie mmeo nilieambiwa kakuoa!?”
Gori alishituka kwanza huku akimtizama Jolvin ambae bado yupo chini! Aligeuka haraka akamfuta damu iliyokuwa ikimtoka puani.
ย ย ย “” Pole Kaka White lazima upone tu! Gorii amemuahidi Bibi anarudi Nyumbani ile furaha inaenda kurudi tenaa! tena itakuwa mara mbili yake Mamangu umemuona lakini! Ila atakaa vizuri sahivi amechakaa na Dunia lazima nimfanye Mamangu awe binti tenaa!?”
Jolvin alibaki kutabasamu japo alikuwa na maumivu hakutaka kumvunja moyo Gorii! Alimtizama mamake kwanza, aliona ana khari mbaya hata hapo anajikaza tu!
Mamake Gorii” alisogea hadi alipo Jolvin Kisha alimshika mkono akimuunganisha na Gorii Kisha aliwatamkia.
ย ย ย “” Naamini nyie ni mke na mme! Kijana naomba umfanye Binti yangu awe na furaha siku zote! Kwaajili yako leo binti yangu umemfanya akutane na Mimi! Kama usingetokea binti yangu asingeniona Tena! Kwasababu yako nimewaona wote naomba mbaki na furaha siku zote! Nina ombi kwako.. najua umeumia Sana hata Gorii” kaumia ila ni vile ana furaha kukutana na Mimi hahisi maumivu!ย Ukipona naomba umtafute mtu anaeitwa Mishoki Kuna mfanyabiashara mmoja waliwahi kuunganisha Shea zao kwa pamoja lakini walikuja kutaharukiana akatoa Shea zake…
Kabla Mama hajamaliza kuongea alianza kukohoa mwisho kabisa alikohoa damu!
Muda huo watu wote walikuwa wakishangaa kinachoendelea baada ya kuona Mama anakohoa sana! Gorii nae alianza kulia ile anataka kusimama ndio anagundua mguu wake haujiwezi Tena! Hapo hapo Ambulance ilifika pale kuwachukua.
Walikimbizwa hospitali kwa emergence rooms! Matibabu ya haraka yalianza kutolewa!ย
Upande wa Mama ile wanataka kumtundikia Dreep ya maji! Wakati Madaktari wanamtafutia mshipa! Kila wakichoma sindano mshipa unafeli walikuja kumtizama vizuri tayari kapoteza maisha! Walifanya kuufunikia mwili Kisha wakampeleka Mochwari.
Huku kwa Jolvin muda ule alivokuja kumsaidia Gorii! Kwa bahati mbaya ile anamvuta aliteleza mguu wake ukawa umepigizwa na gari akaanguka, muda huo alikuwa tayari kumsaidia Gorii lakini na yeye alienda kuangukia chuma akawa amevunjika nyonga!
Matibabu yaliendelea kwa watu wawili Gorii yeye alikuwa akijitambua, alianza kuwasumbua anamtaka Mamaa mpaka wakaamua kumchoma sindano ya usungizi!”
Ile anakuja kuzinduka anashangaa chumba kizima kimejaa watu. Alitazama vizuri ndio anamuona, Rich, Esau, Joely ,Bibi, Mama Rich, Mama Doreen na Doreen. Alishusha pumzi kwanza kisha aliongea.
ย ย ย “” Hivi hatujafa tu!?”
Ilikuwa ni ile dawa ya usingizi inamletea mawenge!
Wote walisikitika ilikuwa ni Yale majibu ya Doctor! Kuwa Mamake katangulia! Jolvin anaendelea vizuri lakini atatembelea magongo kwa muda ila atakuwa sawa! Kwa Gorii pia atatembelea magongo lakini kaumia Sana nyonga kwenye kuzaa itakuwa ngumu, japo atazaa lakini ni kwa Operation.
Bibi alisogea karibu Kisha akamshika mkononi make alikuwa kaumia anae bandage!
ย ย “” Bibi! Umemuona lakini Mamangu! Mbona simuoni yeye anaendeleaje!?”
Bibi alishidwa kujibu akaekiti kikohozi kimembana alianza kukohoa huku akitoka nje! Ma Doreen akawa amechukua nafasi ile.
ย ย ย “” Yupo sawa! Jali afya yako kwanza!”
ย ย “” Kaka white yeye Yuko wapi!! Kama vile na yeye aliumia! Damu zilimtoka puani!”
Wakati ule Esau, Joely na Rich walifika! Ile kuwatizama tu Gorii alijawa furaha aliwamisi pia!
Mama pamoja na Bibi walitoka nje ili wazungumze jinsi msiba utakapokuwa walikubaliana wafanyie kijijini kwao na Gorii, kazi ikabaki ni kumjulisha Gorii kuhusu kumpoteza Mamake.
Waliingia chumbani kwa Jolvin alikokuwa amelazwa walimkuta bado ana usingizi! Mama alikaa huku akimtizama Jolvin baadae ndio anaamka taratibu akipepesa macho.
ย ย ย “” Maama! Gorii anaendeleaje!? Vipi kuhusu mamake?”
ย ย ย “” Anaendelea vizuri ila kaumia nyonga! Na Doctor anadai kaumia Sana hata kuzaa itakuwa ni kwa Operation!”
“” Hapana! Operation tenaa!? Itakuwa kakosea vipimo! Mwambie arudie! Na vipi kuhusu Mamake?”
Mama alitikisa kichwa Kisha aliinama chini, Jolvin akawa ameelewa alimshika mkono mamake Kisha aliongea:
ย ย ย “” Gorii atajisikia vibaya Sana! Mpaka khari yake ikamrudie Kama awali inatakiwa nguvu nyingi! Wakati ule nipo na mamake chini! Aliongea maneno mengi Sana! Yeye anajua Mimi na Gorii ni mke na Mme! Alitushikisha mikono huku akiniomba nimuahidi kuwa nitamfanya Gorii awe na furaha!? Wazani mama Mimi nitaweza kweli kwa khari hii!? Nilitamani muda huo nimueleweshe kuwa hatuna Mahusiano kwa khari aliyokuwa nayo sikuweza kumkatisha! Lakini ombi la mwisho kaniomba nikipona nimtafute mfanyabiashara aliewekeza na Mishoki Shea zake kwenye kampuni nikimpata hakumalizia hata kuongea khari yake ikabadilika! Mpaka nawaza nitakamilisha vipi wakati hakumalizia sentesi yake.
Mama Alibaki akishangaa Mishoki family Tena! Ni familia yao au tofauti na hiyoo?”
Muda huo Joely alifika! Mama alipomuona ilibidi awapishe make alijua huwa hawapatani! Aliwaachia nafasi!
Joely alikaa kitandani Kisha aliushika mkono wa Jolvin huku akiupapasa akitizama ile mishipa ilivyosimama alimuonea huruma Sana! Make yeye alikuwa mkubwa kwake na Jolvin alimfatia Kisha Rich! Esau yeye alikuwa ni mtoto wa Ba Mkubwa.
“” Nakuombea kwa Mungu upate afya tenaa! Najua unapitia wakati mgumu sio Wewe tu! Hata moyo wako unamaumivu ya Gorii! Naimani mtakaa sawa!”
Jolvin alibaki akimtizama Joely alionesha ana huzuni Sana siku hiyo ndio alimuita kwa mara ya kwanza “Kaka” Joely hakuamini aligeuza shingo amtizame Jolvin vizuri Kama ndie yeye kweli kaongea, Alirudia tena baada ya kuona haamini.
“” Kaka naomba umuombee Gorii asiwe mnyonge! Ikiwezekana kaa nae karibu mmufariji! Khari yangu Kama unavyoniona sizani hata msibani nitaenda!”
Joely alihisi furaha Sana! Siyo kwamba hapendi ukaribu wa yeye na Jolvin! Ni vile Jolvin huwa anamkaziaga! Aliamua kumkumbatia palepale Kisha alimnong’oneza sikioni.
ย ย ย “” Vipi kuhusu Msamaha…!!?”
ย ย ย “” Nishakusamehe! Unazani ningekupatia nafasi ya kukaa karibu na Gorii tena, Kama hapo nyuma ilivyotokea!?”
Jolvin alimaliza kuongea huku akicheka, kumbe ugomvi wao ni Joely alimchukulia msichana wake ndio wakapishana! Wakati wanacheka pale Esau, Rich nao waliingia walishangaa wawili hao leo wanashea furaha ya pamoja!
Joely baada ya kuwaona aliwakimbilia akawakumbatia kwa pamoja Kisha aliwanong’oneza.
ย ย ย “” Kwaajili ya Gorii! Jolvin kafungua moyo kanisamehe! Kwasasa tunarudi Kama hapo awali!!”
Muda si mrefu Gorii aliletwa akiwa kwenye wheelchair akisukumwa na Mama Doreen huku Doreen kabebelea baadhi ya nguo huku akiwa analia Mama Rich ndio kamshikilia! huku Bibi nae kashikilia pia Wheelchair wakisaidiana kumwangalia Gorii, walielekea chumbani kwa Jolvin!
Jolvin baada ya kumuona Gorii alianza kuhangaika akae, angalau amtizame vizuri. Joely ndio alikuwa wa kwanza kumuweka sawa mpaka Mama na Bibi walishangaa.
Gori alibaki akimtizama Jolvin kwa sekunde kadhaa, machozi yalianza kudondoka kikifatiwa na kilio! Alijitahidi kujikaza lakini aliishia kuongea.
ย ย ย ย “” Yote haya ni kwasababu yangu! Nisingemkimbilia Mama kwenye Gari wala asingepoteza maisha! Na Kaka White asingekuja kunikimbilia Mimi matokeo yake na yeye kaumia kwaajili yangu!”
Gorii alizidi kulia, mpaka na wale wengine walianza kulia! Ilibidi Doctor aje kuwatoa pale! Kilichofuata ni kilio pale!ย
Jolvin Yale maneno yalimuumiza sana! Kila akikumbuka maneno ya Mamake aliahidi hata yeye lazima ahudhulie mazishi make wameshaunganishwa mwili mmoja na ni ahadi ya Marehemu.
Alimtizamaย Esau pamoja na Joely walikuwa wakimtizama, alimwagiza Joely amwambie Mamake hata yeye ataenda kumsitiri Mamake mkwe wa kiapo.
Joely alienda kumwambia Mamake! Ilibidi afanye utaratibu wa kuongea na Madoctor! Baadae alirudi nao wakaomba wamfanyizie zoezi Kama ataweza kukaa kwenye Wheelchair ataruhusiwa kwenda kustili mwili! Jolvin alikuwa akiumia lakini alijikaza nia na malengo nikukamilisha ahadi yake tu!
Siku ya kesho yake walifanikiwa kuanza Safari majira ya jioni walifika! Walikuta wanakijiji wamekaa kwa huzuni wakisubili mwili wa Marehemu!
Mama Muddy ndio alikuwa Kama ndie familia yake na Gorii! Bahati nzuri Gorii ile hela aliyoituma Nyumbani kukarabati nyumba ilisaidia Sana! Tayari nyumba ilikuwa imekamilika ilikuwa ni mjengo mzuriย wa kisasa! Ilipigwa lip na rangi ya kutosha pamoja Na Tails chini! Ni Kama alimwandalia mamake sehemu ya kupumnzikia akisubili apelekwe malaloni.
Upande wa Jolvin nae alikuwa haamini! Kipindi kile walipokuja waliishia kwa Mama Muddy japo na penyewe kulikuwa kumejengwa nyumba nzuri hizi zote ni juhudi za Goryanah!”
Muda huo Gorii aliachiwa abaki na wanakijiji wenzake ili wazidi kumfariji! Mama Muddy ndie alikuwa ni Kama Mamake mzazi alichukua nafasi hiyo! Waliongea mambo mengi Sana! Alimwelezea jinsi alivyoonana na mamake kwa muda mfupi hatimae kampoteza kwa huo huo muda mfupi! Pasina kumwambia wapi alipokuwa!?”
Mama Muddy alisikitika Sana, alimwambia pia kuhusu Mzee Rajab nae wamemzika Kama mwezi mmoja umepita kwa ugonjwa ule ule wa upungufu wa Kinga Mwilini!
Sitori nyingi ziliendelea ili kumfanya Gorii awe na amani! Lakini akili yake ilikuwa mbali Sana japo alijitahidi kujikaza!ย
Huku kwa Jolvin khari yake haikuwa nzuri ukiangalia kajilazimisha tu kufika! Ilibidi avumilie hivyo hivyo huku akiendelea na matibabu! Make walikuja na Doctor wao.
Siku ya kesho ndio ilikuwa ni siku ya kusitiri mwili! Zoezi lilimalizika lakini Gorii Alibaki amekaa pale pale malaloni akibaki kukumbuka mambo mengi aliyoyafanya na mamake leo hii hayupo tena! Ilibidi wamuache kwanza pale akiwa amekaa kwenye Wheelchair!ย
Jolvin alikuwaa amekaa mbali akiangalia! Alimuomba Rich amsaidie kufika pale! Ukiangalia jua lilikuwa linachoma Sana ilibidi amfuate! Na yeye ndie alikuwa akijulikana Kama mme tangu kizaazaa Cha Hammad na Gorii wakamini vile.ย
Gorii alimtizama Jolvin baada ya kuhisi yupo pale! Kisha aliongea.
“” Kaka White! Tayari Mama ameshatangulia mbele za haki! Njia hii hii Kuna siku na sisi tutairudia! Ila kifo ni fumbo…!”
Gorii aliweka kituo huku akiomba msaada wa kutoka pale Doreen alifika kutoa msaada! Ikawa wanasukumwa taratibu kwenye wheelchair mpaka wakafika kwenye umati uliokuwa ukiwazunguka, kwa mbali Gorii ndio akamuona Hammad kabebelea mtoto alijua kabisa atakuwa ni mwanae alimuta kupitia kidole akawa kafika, alimshika Yule mtoto shavu Kisha alimwangalia Hammad akamwambia.
ย ย ย “” Kitu nilichokuwa nakikataa katika maisha yangu kuwa na Wewe hatimae nilifanikiwa lakini Nilitegemea siku moja uje uwe na familia nzuri utakayoishi nayo kwa upendo Kama hivi leo! Nafurahi imekuwa hivyo! Ungelazimisha kuwa na Mimi usingepata familia nzuri Kama hii! Nakushukuru kwakuwa umekuja kumstiri Mamangu angalau hata kwa kumwandalia nyumba yake ya kulala umeshilikiana na vijana wenzako! Hongera kwa hilo!”
Gorii alimaliza kuongea Kisha alimuaga Hammad wakisogea mbele! Umati wa watu uliwafuata pia kupata chakula make ilikuwa ni wakati wenyewe.
Baadae kabisa Muddy ndio alipata muda wa kuongea na Gorii” Alimshukuru Sana Gorii kwa mchango alioufanya Nyumbani kwao! Bado kamfungulia duka kubwa la bidhaa anauza kwahiyo maisha kwao kwasasa yapo vizuri!
ย ย ย “” Gorii! Nakuomba uendelee kuwa na moyo huo! Halafu nimegundua kweli Jolvin anakupenda Sana Kama alikimbia kuja kukusaidia wewe bila kujali ataenda kuumizwa lakini aliachilia mbali naomba ukae nae karibu”
Gorii alitabasamu tu! Huku akiamini ni kitu hakiwezekani Kafanya Kama wajibu isitoshe ni mwanafamilia, hii haikumuingia kichwani.
Siku ya kesho yake watu walianza kusambaa wakielekea makwao! Gorii yeye hakutaka kurudi mjini make alienda kule kumtafuta Mamake na Kama kampata haina haja ya kurudi tenaa! Taarifa zilifika kwa Jolvin zilimuumiza Sana ukiangalia ndie jukumu lake kakabidhiwa inatakiwa arudi nae kivyovyote vile.
Mamake Rich ilibidi akaongee na Mama Muddy! Mwisho kabisa aliamua kufunguka jukumu aliloachiwa Jolvin na Marehemu! Mama Muddy ilibidi amuite Gorii aongee nae lakini Gorii alirudisha.
“” Huwa ni kawaida tu kuongea vilee! Mama alipata hofu baada ya kushuhudia ile ajari, Mimi naweza kujilinda mbona!?”
“” Gorii Mwanangu! Semi ya mwisho ya Marehemu huwa inasikilizwa kuliko kitu chochote! Unavyokataa Roho ya Mamako inahangaisha huko haitulii! Pia itakuwa inamsumbua Jolvin muda wote hajakamilisha ahadi yake!”
Gorii alikuwa bado haelewi ilibidi aitiwe wale wabibi wenye umri umeenda kidogo mwisho akawaelewa kidogo ila kuunganishwa kuolewa alikataa! Alikubali Kama ni kukaa karibu yake ili Mamake asiteseke hapo sawa! Na swala la pili ni kwaajili ya matibabu tu.
Walikubaliana na Safari ikaendelea! Jioni yake walifika, Jolvin alikuwa na khari mbaya ilibidi arudishwe hospitali! Na siku iliyofuata Gorii alikuwa akijaribu mazoezi ya kusimama pekee! Akili yake ilimtuma Kama atapona haraka atarudi Nyumbani kwao mapema! Siku hiyo ikawa mbaya kwake alianguka vibaya bahati nzuri walinzi walimuona wakawa wamemsaidia akapelekwa hospitali matibabu yakaanza upya.
Zilipita Kama wiki mbili Gorii alikuwa ni wa kitandani! Alikuwa ni wa kuamshwa kujisaidia make alikuwa kawekewa vyuma kwenye nyonga ili akae vizuri. Jolvin yeye alikuwa akiendelea vizuri alikuwa akitembelea magongo na mara nyingi alifika kumuona Gorii.
Siku hiyo alikuja kumuona Gorii alikuwa ametulia kitandani, Jolvin alifika pale akakaa make walizoea kupiga visitori vya hapa na pale, Gori alianza…..
“” Kaka White.. Afadhari umeugua Anelisa hayupo, make hapa hospitali ingekuwa Jovi… Unaendeleaje, Jovii.. nikuletee Nini?,ย Jovii… Umekula, Jovii… Sipendi kukuona unakuwa hivi, Jovii… Nikuletee mihogo… Yaani humu ndaniย tusingepumua..
Jolvin alicheka tu, Kisha akamuuliza.
ย ย “” Kumbe hupendi ukaribu wangu na Anelisa.. !?””
ย ย ย “” Sio Sipendi… Yaani napenda mpaka basii!! Huoni namisi.. hizo Joviii…ย
ย ย “Huwa zinakufurahisha Sana ee!?”
ย ย ย “” Achana nae tu! Na bora napumua make hapa ningekuwa nimebanwa balaa.. “
ย ย ย “” Huyo anakufaa bhana! Hivi kwanini nimecheka nilipokuona.. Ani ulivyoingia na hizo gongo unavohangaika kuingia.. umeviligisha kiuno Kama unacheza sidimba ndio ukakaa… Halafu eti Mama kasema Gorii, Jolvin” waje kuwa mme na mke… Viwete wote?.. Si nilikwambia alikuwa na Mawazo haukunielewa tu”
Jolvin alikuna kichwa kwanza huku akimsogelea Gorii akawa amekaa kitandani, Kisha alimtizama.
“” Kwahiyo Wewe hapo hauwezi kukili uzima!? Utakuwa wa kindani maisha yako yote!?”
“” Aaa Kaka White! Nishakukataza kunisogelea Sana! Mpaka huwa naogopa kukujibu!ย ” Sawa Wewe unazani mi nikiamka hapa si nitakaa kwenye Wheelchair muda wote Kama ile siku nilivyokaa!?”
Jolvin aling’ata midomo kwanza ni tabia yake alikuwa nayo Kisha alinyanyua mkono wake wa kushoto akamshika kichwani.
“” Mimi nakuombea upone! Ukaendelee na Duka lako! Kumbuka niliwaahidi msimu wa Sikukuu duka litakuwa wazi na Wewe utakuwepo! natamani iwe hivyo! Siku ya kesho utaelekea India kuchekiwa naimani ukirudi utakuwa haupo kwenye khari hii Tena!”
Jolvin alimtia moyo Kisha alisimama kuondoka! Lakini Gorii alimshika mkono, ilibidi ageuke kumtizama.
ย ย ย “” Ile siku nilipokaa kitandani kwako uliniambia nitandike! Na wewe umetandua shuka! Tandika!”
Jolvin ilibidi atandike kwa kutumia mkono mmoja! Kisha alimwaga aondoke.
ย ย ย “” Usiku mwema Goryanah! Kabla kesho hujaondoka nitakuja kukuona!”
Siku iliyofuata Gorii alichukuliwa akawa amepelekwa India kwa matibabu! Jolvin yeye alikuwa akiendelea vizuri baada ya wiki moja kuisha alikuwa akitembea bila magongo japo ni kwa hatua moja moja! Na hii ilidhihilisha anaendelea vizuri.
Yapata mwezi mmoja kuisha Gorii ndio alirejea Tena akiwa mzima! Siku hiyo Mishoki family walikuja kumpokea Airport! Kwa pamoja walimpokea kwa furaha huku kila mtu asiaminiย kumuona yupo sawa sema kilichobadilika ni ile speed ya kutembea haraka ilikuwa imepungua.
Mwanzoni walifikili labda ni kwa muda tu! Hata walipofika nyumbani! Mwendo ni ule ule! Wengine waliogopa kumuuliza lakini Rich akaliwasha!
ย ย ย “” Gorii hivi ni Mimi tu sikuelewi! Inaonekana ulivoenda kutibiwa Kuna ile nati moja ilikuwa imelegea sahii imeenda kukazwa, naona sahiiย hupamii viti, milango na sofa!?”
Ilibidi wote wacheke ndio wakachangia maada kweli, Kweli!
ย ย ย “” Yaani mlivyocheka hata Mimi nilicheka hivyo hivyo! Baada ya kumaliza kufanyanyiwa matibabu nilijaribu kutembea nikaona huu mwendo sio wangu! Ikabidi niangalie miguu huenda nimebadilishiwa! Aaa! kumbe ni yangu ila huku kwenye kiuno sijui wameweka Nini tu nashidwa kutembea vizuri!”
Wote waliangua kicheko tena! Gorii alizunguka kwanza, akatazama watu wote Baadae akaona kunae watu wawili wamepelea.
ย ย ย “” Macho yangu tu au!!? Kaka white Yuko wapi? Au na yeye tumepishana India kimatibabu! Na huyu J mkubwa yuko wapi!?”
Mama alisogea pale Kisha alimkumbatia kwa furaha.
ย ย ย “” Leo ni sherehe yenu! Tumewaandalia part kubwa ya kufurahia afya zenu! Ingia chumbani kwako ujiandae kila kitu utakachokikuta utakitumia! Halafu ndio utaenda kumuona huyo Kaka White! Na yeye katoka kwenye matibabu Pamoja na wengineo ambao hawapo hapa!”ย ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya 19
Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yakoย
Ulipitwa naย SIMULIZI NYINGINE?ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoย kijiweni.co.tzย unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiย editor@kijiweni.co.tzย ย
ย
20 Comments
Wakwanzaa kuisoma
leo umecheza kaka pele
Jamnii gorr tenaa furahaa imerudii upyaa bado ndoa tyu hahhaha
Neeeeeeext
Sehemu ya kumi na Saba ipo wapo
Ila admin unatusahau Sana mbn ulikwa unatoa mbili kwa siku Sasa imekwaje. Seema watu was michezo saiv ndo wanaenjoy Sana ๐ค๐ค๐ค๐ค
Leta 19 admin, tunaingoja Kwa hamu.
Dah!! Naona gorii na jov mambo yao yanaenda kua mazur sasa mambo ni๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Hii sehemu mbona inahuzunisha
Taarifa mheshimiwa…………..naomba mwendelezo wake kesho saa moja asubuhi.
Uwiii sitamani kuikosa aseee naiwaza kabisaa
Daaaaah unbelievable hope atakuwa sawa gorii
Apo leo unyama sasa๐
Delicious story
Good Story
๐คธ๐คธ๐คธ๐คธ๐ฏ๐ฏ๐โ๏ธ๐๏ธ๐ง๐๐๐ am enjoying the story for sure
Kwa kauli ya mama goryanah kabla hajafa inaniweka nnjia panda ukute goryanah baba yake ni …….embu admin tufanyie wepesi wa muendelezo maana sio kwa utamu huu
Ingawa Leo naona kama imekua ndefu au ni Mimi tu
Apo sawa umeshusha
Presha ila nasubiria
Ile kauri ya mm familia ya mishoki_______???
So good so mwaaa
รaaaah mara pa Goryanah ni damu ya mishoki ๐๐