Namna timu zote mbili yaani Yanga pamoja na Simba zilivyoingia uwanjani na kucheza ni jambo ambalo wengi walitarajia na imetokea hivyo na tofauti ya mchezo wao wa mwisho kukutana na hii ni ndogo sana, Yanga SC alimuachia Simba SC kumiliki mpira kwa dakika 20 za mwanzo na dakika zilizobaki alizichukua na kumiliki mchezo kwa kasi kubwa.
Kasi Ya kushambulia kwa timu zote ilikuwa juu kwa dakika za mwanzo na timu zote mbili zilitengeneza nafasi za magoli, Simba SC wakitengeneza nafasi nzuri za kufunga na zote zilikuwa kwa Sadio Kanoute ila walishindwa kutumia, ubora wa Yanga SC ulikuwa kwenye matumizi ya nafasi chache za kufunga walizopata na wamezitumia vizuri.
Tatizo lilikuwa wapi kwa timu zote mbili ? Simba SC waliacha mianya au nafasi sana hususa kwenye eneo lao la kati na mikimbio mingi waliyoamua kuanzisha Yanga SC kuelekea mbele ilikuwa ikipitia katikati. Yanga SC kwao ilikuwa rahisi kuzuia mashambulizi ya Simba SC kwani walikuwa haraka sana kureact kukava mianya yao.
Kipindi cha pili kilibadilika sana na Simba SC, walikubali kuwa chini kidogo na kuhepusha kupishana sana na Yanga SC wakiwa kwenye 4-2-2-2 na Yanga SC waliamua kuwa chini kuufanya mchezo uwe taratibu na hiyo ilisababishwa na ubora waliyonao na matokeo walishakuwa nayo kwa muda mrefu hata hivyo wakati ambao waliamua kuondoka taratibu na kushambulia walikuwa sahihi ila kuna wakati maamuzi hayakuwa sahihi.
Kuna wakati Simba SC ilikuwa inashindwa kueleweka wafanye โpressโ au wazibe mianya kwanini ? Kubwa ni walikuwa wanapanda sana na wakati mwingine walikuwa wachezaji wawili hadi watatu kwenye mpira jambo lililofanya mpira ukiamishwa basi mianya kuonekana.
Magoli yote mawili waliyofungwa Simba SC yalikuwa na makosa ya wachezaji wao, goli la kwanza kosa lilikuwa kwa Hussein Kazi kushindwa kufanya maamuzi ya haraka na kupelekea presha โpressโ kuongezeka kutoka kwa Aziz Ki na kupelekea kufanya kosa, goli la pili uharaka wa Joseph Guede na pasi ya Khalid Aucho ilikuwa bora ila kwa kosa alilofanya Mohamed Hussein ni lazima upate adhabu na adhabu hiyo ni kufungwa goli, kwa upande wa Simba SC umakini mdogo wa mabeki wa Yanga SC ndiyo uliyowapa adhabu ya kuruhusu goli wachezaji 3 dhidi ya Mmoja na bado waliruhusu goli Mchezaji pekee aliyeonyesha kutaka kufanya maamuzi haraka ni Ibrahim Bacca pekee.
Sadio Kanoute nafasi mbili za kufunga goli ila anashindwa kufunga jambo linalompa nafasi mpinzani wako kukuadhibu kwa nafasi chache alizopata. Kibu Denis kasi nguvu na kujituma kwake hakuna shida ila eneo lake la mwisho bado linahitaji maboresho zaidi, Stephane Aziz Ki amekuwa na msimu bora sana namna anamiliki na kuondoka na mpira zaidi amekuwa hatari sana kwenye kupiga pasi mara nyingi pasi zake alizopiga zilikuwa zinafika na hatari sana, Clatous Chama kuna kitu ameongeza kwenye uchezaji wake amekuwa akishuka chini kuchukua mipira na kukaba pia amekuwa ndiyo msingi mkubwa wa kuanzisha mashambulizi kwa Simba SC msimu huu hususa kwenye raundi hii ya pili.
Mchezo wa leo ulikuwa wa kimbinu zaidi kwa pande zote mbili Simba SC na Yanga SC na ulifanya kuwa wa tofauti na matarajio ya wengi.
SOMA ZAIDI: Tabiri Sasa Matokeo Ya Dabi Ya Kariakoo Hapa Kijiweni
11 Comments
Kwanza kabisaa simba waboreshe timu yao maan mpira wanaocheza sahiv ni wa kiwango cha chini pili simba wanakosa sana nafasi tatu kumiliki sana mpira sio kupata matokeo approach ya gamondi ilikua best for today
Simba inatakiwa kufanya maboresha sahihi kuanzia kwenye uongozi ndipo uje kwenye wachezaji. Wachezaji wengi wa simba sc waliokuwepo hawana quality ya kuitumikia club hiyo ๐ฆ๐ฆ
Uongozi wa simba ajiuzuru!!!!!!
Yani Simba sijui tifanyaje kwa Mimi navyoona bora hata ijishushe daraja Ili haanze upya kabisa ๐ค๐ค
Sio kwa mpira wa simba๐๐๐. Hata hilo goli lao basi tu nondo kaona awape maana hizo skendo zake za kwenda Simba zishavuma .
Ningepemda wasajili wafungaji wapya hao waliopo wanajigonga gonga tu golini ๐๐๐sisi wananchi hatuoni challenge tunataka challenge .
Simba sc inahitaji maboresho makubwa hasa eneo la ulinzi simba sc imeruhusu bao 21 .za kufungwa .. ikiwa imefunga goal 41 hii ni mbaya sana .. pili Eneo la kiungo hatuna kiungo mkabaji mithili ya Gerson Fraga Tadeo lwanga au Khalid Aucho .. Tunahitaji left winger na right winger wenye kasi pia Eneo la ushambuliaji tunahitaji striker katili mithili ya fiston kalala mayele … KIKUBWA UONGOZI ULIOPO UPISHE WENGINE .. WAITUMIKIE SIMBA SC KWA WELEDI MKUBWA
Actually kwa sasa young Africans wapewe maua yao iko wazi n team bora kwa sasa simba inabid ogumili we upya kuanzia uongozi na usajil wa wachezaj bora
Simba mbovu tu
Wafukuze kocha
Ni vyema kwanza baadhi ya viongozi muhimu waachie nafasi zao zimilikiwe na wengine . Hata mwenyekiti wa bodi pia nivyema akang’atuka tu. Watu unaowaongoza pia hawajutaki sasa unaforce vp siutoke ?๐
Lakini pia wachezaji wasioweza kutumika ndani ya dk 90 wapewe nafasi chache said maana wanamchango ktk metch but hawawezi kucheza dk zote 90.
After that sasa tuhamie kwenye kroo nzima ya wachezaji Stoke yupi na yupi abaki. “kuanza upya sio ujinga lakini kukumbatia maji kama jiwe huo Ni ujinga”
Shida ni kuwa Simba haijapata wabadili wa kiwango cha wakati ule. Kwa mfano Kagere aliewahi kufunga magoli 23, na mara mbili mfululizo alikuwa mfungaji bora, Boko, Nyoni, Mkude na yule beki wa kati wa Ivory coast na wengineo