Hivi sasa mchezo wa mpira wa miguu ni moja ya michezo maarufu duniani na umekuwa ukiteka hisia za watu mbalimbali na wa rika zote.
Soka ndiyo mchezo unaopendwa zaidi duniani na unachezwa kwa kufuata sheria Zilizotungwa ma Bodi ya Kimataifa ya Sheria za soka maarufu kama “International Football Board Association IFBA” chini ya usimamizi wa Shirikisho la Soka duniani FIFA.
Soka au mpira wa miguu ni mchezo unaochezwa na wachezaji 22 uwanjani kwa timu mbili tofauti ikiwa na idadi sawa ya wachezaji 11 kila upande/timu.
Sasa kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Duniani “Federationale Internationale de Football Association” FIFA wametunga sheria zinazoongoza mchezo huo pale unapochezwa kiwanjani na sheria hizo kwa ujumla wake ziko 17 zenye vipengele vyake.
Sheria hizo ni mpira, uwanja, vifaa vya wachezaji, mwamuzi, waamuzi wasaidizi, muda wa mchezo, kuanza na kuanzishwa tena kwa mchezo, mpira mchezoni na mpira kutokuwa mchezoni, kuamua matokeo ya mchezo, kuotea, rafu na utovu wa nidhamu, mapigo huru, pigo la penalti, mpira wa kurusha, pigo la goli na pigo la kona. Zote hizo ni sheria zinazoendesha mpira wa miguu ndani ya kiwanja.
Mchezo unapochezwa kwa dakika 90 uwanjani matukio mbalimbali na makosa pia hutokea kati ya hayo baadhi hushindwa kutafsiriwa vizuri na waamuzi au maamuzi yatolewayo uleta utata kwa mashabiki wa timu fulani japo kuwa huwa ni maamuzi sahihi yaliyotolewa, Sheria namba 11 ni moja ya sheria ambayo maamuzi yake huleta utata katikati ya mashabiki na wapenda soka.
Sheria namba 11 “Kuotea/offiside “
Sheria hii ina vipengele vinne vyenye kuleta maamuzi sahihi uwanjani navyo ni kipengele cha kwanza nafasi ya kuotea, kipengele cha pili kosa la kuotea, kipengele cha tatu Sio kosa na kipengele cha nne Makosa na Adhabu.
Kipengele cha kwanza “Nafasi ya kuotea “ sheria inasema Mchezaji atakuwa kwenye nafasi ya kuotea endapo sehemu yeyote ya kichwa mwili au mguu wake utakuwa kwenye nusu ya kiwanja cha timu pinzani au kuwa karibu zaidi na goli la timu pinzani. Mikono na viganja vya wachezaji wote havihusishwi kwenye kosa la kuotea.
Zaidi mchezaji hatokuwa kwenye nafasi ya kuotea endapo atakuwa sambaba na mpinzani wa pili wa mwisho au wapinzani wawili wa mwisho.
Kipengele cha pili “Kosa la kuotea “ kipengele hiki kinaelezea kosa la kuotea baada ya Mchezaji kuwa kwenye nafasi ya kuotea. Mchezaji atahukumiwa kuwa ameotea endapo ataingilia mchezo kwa kupasiwa na Mchezaji wake au kumuingilia mpinzani kwa kuucheza au kuzuia nafasi ya mpinzani kuona mpira.
Pia atahukumiwa kuotea kwa kugombania mpira na mpinzani, kucheza mpira uliogonga mwamba au mpinzani huku yeye akiwa kwenye nafasi ya kuotea au akitokea kwenye nafasi ya kuotea.
Kipengele cha tatu “Sio Kosa “ Mchezaji hatohukumiwa kuwa ameotea endapo sehemu yake ya mkono pekee itakuwa imezidi mpinzani wake au atapokea mpira moja kwa moja kutokana na pigo la goli maarufu kama “free kick “, mpira wa kurusha (thrown in)au pigo la kona.
Kipengele cha nne “Makosa na adhabu “ Kipengele hiki kinaeleza kuwa endapo Mchezaji atakutwa au kuadhibiwa kwa kosa la kuotea mwamuzi atatoa maamuzi ya pigo huru lisilo la moja kwa moja “Indirect free kick” na litapigwa kutokea mahali ambapo kosa limetendeka ikiwa ni ndani ya eneo la nusu ya kiwanja cha mpinzani.
Mchezaji aliye kwenye nafasi ya kuotea anaweza kujitoa kwenye nafasi ya kuotea pale timu yake itapokuwa inashambulia kwa kutojihusisha kuucheza au kutojaribu kuingia mchezo. Ikitokea Mchezaji huyo ameingilia mchezo huo bhasi mwamuzi ataamuru kuwa ameotea.
Ikitokea Mchezaji wa timu inayooshambulia yuko kwenye nafasi ya kuotea na atabaki wima pale mpira uliyopigwa na Mchezaji wa timu yake utakuwa unaelekea golini na kuingia bhasi goli litakubaliwa. Isipokuwa, endapo mpira huo kabla yakupigwa kuingia golini Mchezaji huyo alicheza faulo au kuonyesha utovu wowote ule wa kinidhamu ikiwemo kumpiga mpinzani kwa kiwiko au ngumi bhasi atahukumiwa kama sheria namba 12 inavyosema ya faulo na utovu wa nidhamu.
SOMA PIA: Takwimu Na Rekodi Za CBE SA Wapinzani Wa Yanga Ligi Ya Mabingwa Afrika
2 Comments
Pingback: Huu Ndio Wakati Wa Wazawa Kuwa Bora
Pingback: Fahamu Yote Kuhusu Muundo Mpya Wa Ligi Ya Mabingwa Ulaya