Ilipoishia “Hayo ni majina ya Watu wa siri wa Mzee Dawson, Sande yupoย hai, moja ya kaburi hapo linaweza kuwa kaburi la Zola,ย fukueni haraka sana.” Ilisikika sauti ya John Brain, aliaminiย Dawson ni Mtu mwenye akili sana kwenye mambo yake.ย
Mengine yalionekana kuwa ya zamani sana lakini moja lilikuwaย bado jipya, wakalifukua hilo kwa kutumia chepe iliyo kwenyeย kona ya chumba hicho chenye makaburi. Kazi hii ilifanywa na Six aliyekuwa amebana rasta zake kwa nyuma. Jasho lilikuwaย likimtoka, harufu kidogo ilianza kutapakaa pale, haikuwazuiaย kufanya kazi yao. Endelea
SEHEMU YA KUMI
“Oooh Shit!” Alisema Six huku akitema mate, Malaika ilimbidiย asogee paleย
“Duuh! Kweli huyu jamaa alipitia mafunzo makubwa sana”ย Alisema Malaika, mwili huo ulikuwa umeharibiwa kwa kemikaliย maalum ambayo iliwafanya akina Six washindwe kuitambuwa suraย hiyo, wakati wanaendelea kushangaa tukio lile Malaika alionaย kitu kama redio Call hivi kando ya aliposimama tena ikiwaย imefukiwa kidogo, akaifuata na kuiokota akakuta redio hiyoย ikiwa inafanya kazi.ย
Haraka Malaika akakimbilia alipoliacha begi lake, akatoaย Laptop na baadhi ya vifaa fulani kisha akavaa Head Phone,ย akawasha kitu fulani kutoka katika Laptop yake akaona mawimbiย ya redio hiyo yakiwa yanatoka kando ya Bahari ya Hindi.ย
“Umefanikiwa kugundua chochote?” Aliuliza Six akiwaย ameshikilia chepeย
“Eneo ulipo mtambo wa redio hii ni kando ya Bahari ya Hindiย upande wa Mashariki”ย
“Inaweza kuwa mhusika wa andaki hili yupo huko, kama niย Dawson basi arobaini yake imefika” Alisema Six kisha kwaย pamoja wakapanda juu kutoka katika lile andaki wakijiandaaย kufuata mawimbi hayo. Walipotoka wakakutana na wauminiย waliokuwa wamesimama nje ya andaki hilo, walionekanaย kushangaaย
“Nani amechimba andaki hili hapa?” Aliuliza Malaika hukuย akiwa ameshatoa kitambulisho feki walichopewa na Rais iliย waonekane ni Watu wa Usalama wa Taifa. Macho ya watu haoย yalionekana kujawa na woga wakawa wanasakiziana kujibu, mmojaย akasikaka akisemaย
“Hatukuwahi kuona wala kuhisi uwepo wa shimo hilo, kwa miakaย mingi nimeishi hapa lakini hili shimo sijawahi kuliona”ย Alisema huku akitikisa kichwa chake, alionekana kuwa Mzeeย sana mwenye mvi nyeupe zisizo na matunzoย
“Kanisa hili limejengwa lini?” Aliuliza Sixย
“Miaka 15 iliyopita”
“Nani alihusika na ujenzi wake?” Six aliuliza tena,ย alichotaka kusikia ni jina la Mzee Dawson likitajwa ili waweย na uhakika wa wanachoenda kufanyaย
“Mfadhili alishafariki miaka mitatu baada ya kanisa hiliย kukamilika” Alijibu tena yule Mzee ambaye alijibebesha mzigoย wa kujibu maswali ya Sixย
Walipoona hawawezi kupata walichokuwa wanakitaka waliondokaย haraka eneo hilo ili kuanza safari ya kuelekea Kando yaย Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, upande huu ndiko ambakoย nyumba ya siri ya Marehemu Zola ilijengwa.ย
Kitendo cha Six na Malaika kuondoka kilimpa mwanya yule Mzeeย akawaacha wenzake wakiendelea kushangaa uwepo wa andakiย kanisani, akaenda nyuma kabisa ya kanisa hilo, alihakikishaย hakuna aliyemuona tena akionekana kuwa mwenye wasiwasiย Mkubwa.ย
Akawa anatafuta kitu ardhini kwa kukita mguu wake, alifanyaย hivyo kwa dakika kadhaa hadi alipokita mahali aliposikia kamaย kuna sauti inamuitikia, ilikuwa ni sauti iliyoashiria uwepoย wa kitu fulani sehemu hiyo, akafukua kwa kutumia mikono yakeย sababu eneo hilo lilikuwa limeloa kutokana na maji yaliyokuwaย yakimwagika kutoka katika tanki, akafanikiwa kufukua na kutoaย sanduku la rangi ya fedha, akapanda juu ya ukuta akiwa naย sanduku hilo dogo kisha akatokomea zake pasipo kuonwa naย yeyote yule.ย
Turudi kule kwenye Makazi ya siri ya Marehemu Zola, hali yaย kutafakari ilikuwa imechukua nafasi kubwa sana. Dawson haliย yake kiafya haikuwa nzuri hasa baada ya kupata mikiki ya hapaย na pale kwa zaidi ya masaa nane bila kutuliza akili yake,ย kifua kilikuwa kikimbana mno huku Kisko akimsaidia baadhi yaย dawa na huduma nyingineย
“Asante Kisko! Natamani sana siku moja niwaone mkitoka katikaย Maisha haya ambayo nahisi yanawapa mateso makubwa sana, hamnaย uhuru wa kufanya mambo yenu. Nimewalea kwa muda mrefu sana”ย Alisema Dawson huku akiangalia saa yake mkononi, kiskoย akamuulizaย
“Kwanini unaangalia saa hiyo kila wakati ilhali haioneshiย chochote?” Mzee Dawson akajilazimisha kucheka kidogoย
“Inaonekana kutokufanya kazi ndio lakini Je kama nikikwambiaย Hii saa ndiyo Mimi utaamini?” Kisko akacheka kisha akasema
“Hata Mtoto mdogo hawezi kuliamini hilo, Mtu anawezaje kuwaย saa?”ย
“Bahati mbaya au nzuri, nyie mna majina yenu. Majina ambayoย mlipewa huko mlipotoka, licha ya kupewa majina ya Kijeshiย lakini hayakuweza kubadili uhalisia kuwa wewe ni Kisko,ย wenzako ni Jesca na Chande” Akasema kisha akakohoa na kutoaย damu nzito sana, akapewa maji ya kusukutuaย
“Nawaza Jesca atakuwa wapi, ni masaa mengi yamepita bilaย kuwasiliana naye. Ulifanya kama nilivyo kwambia?” Alihojiย Dawsonย
“Ndio redio Call niliiacha kwenye kile chumba chenyeย makaburi” Alijibu Kisko huku akionekana kuwa mwnye kiu yaย kutaka kujuwa mengiย
“Hata wewe pia ni mwenye Bahati kama ni hivyo, una jina lakoย halisi Kama Dawson” Dawson akacheka tena kisha akasemaย
“Sababu Mimi ni Afsa wa juu katika Nchi hii ni lazima nitumieย jina halisi lakini kuna jambo lililo nyuma ya Pazia, utakujaย kuelewa siku moja endapo Mungu atanijalia uhai mrefu waย kuishi” Yalikuwa ni maongezi yaliyojaa mafumbo ambayoย hayakumshibisha Kisko, Muda huo Chande alikuwa kwenye chumbaย kimoja na Sande Olise wakiwa wanazungumzaย
“Tunasubiria nini?” Aliuliza Chande akiwa anamtazama Sandeย Olise aliyekuwa ameegesha nwili wake kwenye moja ya kioo naย kujipa fursa ya kutazama chini ya jengo hilo la kifahariย
“Hatuwezi kukurupuka! Tupo mawindoni Chande, kosa dogoย unaadhibiwa kifo. Nchi inatutambua kama waasi kutoka masaaย machache ya kujulikana kama Wazalendo wenye kulipiganiaย Taifa, Dunia wakati mwingine inaweza isikupe maana halisi yaย Binadamu”ย
“Ha!ha!ha!” Alicheka Chande, muda huo Kisko alikuja mbio naย kuwaambiaย
“Mzee Dawson hali yake ni mbaya sana” Taarifa ikazua taharukiย pale, wote wakaelekea chumbani kwa Dawson! Wakamkuta akiwaย ana pumua kwa shida sana.ย
“Inabidi tumsaidie!” Alisema Chande akionekana kuwa na wengeย la kutoshaย
“Tulia!! Hatuwezi kufanya hivyo kwa sasa, hatuweziย kuhatarisha Maisha yetu kirahisi hivyo!!” Alisema Sande kishaย alimgeukia Dawson
“Yupo sahihi! Rais anajuwa Mimi naumwa kwa muda mrefuย simalizagi wiki mbili kabla ya kupelekwa JNI Hospital kwaย matibabu ya ugonjwa wangu sababu wao ndio speshelist waย tatizo hili, huu ni mtego mtakamatwa wote. Ni bora mniacheย nife nyie mbaki kuwa hai” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaaย maumivu mnoย
“Baba usiseme hivyo unayo nafasi ya kuendelea kuishi, semaย unataka nifanye nini Baba” Chande alisema kwa uchungu hukuย macho yake yakibubujika chozi laini lililolowesha mashavuย yake madogo, Mzee Dawson kwao alikuwa ndiye Baba yao sababuย aliwatoa kwenye kituo cha kulea Watoto yatima miaka mingi,ย akawapeleka mafunzoni, wakapata mafunzo ya kijeshi naย kijasusiย
“Chande anayejuwa mwisho wangu atawapa tumaini endapoย atanichukua” Alisema Dawson huku hali yake ikizidi kuwaย mbaya!! Sande Olise akahisi jambo, haraka akaelekea kwenyeย kioo kutazama chini akaona gari nyeusi ikiwa imesimama nje yaย uzio wa jumba hilo la siri, walikuwa ni Malaika na Six ambaoย walikuwa wakifuatilia mawimbi ya Redio Call kutoka kanisaniย hadi Ufukweni, kifaa chao kiliwaambia kuwa walikuwa wamefikaย eneo husika.ย
“Kuwa makini!” Alisema Six kisha akampatia Bastola Malaika.ย Sande akarudi kwenye kile chumba akawapa taarifa kuwa Kunaย hali ya hatari wanapaswa kuokoa Maisha yao harakaย iwezekanavyo, muda huo Mzee Dawson alikuwa katika hali mbayaย ya kuumwa.ย
Ndani ya msitu mmoja ulio kando na Jiji hili, alionekana Mtuย mmoja Mzee Akikimbia, mkononi alikuwa ameshikilia sandukuย lenye kutu, alikuwa ni yule Mzee aliyefukua Sanduku kuleย kanisani. Alikuwa amechoka baada ya kukimbia kwa muda mrefu,ย mikono yake ilikuwa ikitetemeka. Akaingiza mkono mfunoniย akatoa funguo kisha akasimma chini ya Mti mmoja mkubwa,ย akalifungua sanduku hilo.ย
Ndani ya sanduku kulikuwa na kifaa kimoja kilichoonekana kuwaย cha zamani sana, akakiangalia kisha chozi likawa linamtoka.ย Akabonyeza kitufe cha kuwasha, kikawaka.ย
Kifaa kile kilikuwa kimeunganishwa na vifaa vinne ambavyoย vilikuwa kwa Watu wanne, Mtu wa kwanza kupata ishara alikuwaย ni John Brain, Mtu wa pili ni Mzee Dawson, wa tatu ni Malaikaย na Wanne ni Six ambaye alikuwa akitembea kuelekea kwenyeย jengo lingine kama kawaida yake kutafuta eneo zuri la kulengaย shabaha, kitendo cha kuwashwa kile kifaa na yule Mzee kuleย msituni kilimfanya Six aanguke na kuhisi baridi kali sana,ย vivo hivyo kwa Malaika ambaye alikuwa ameshafika kwenye getiย la kuingia katika jumba la siri ambalo Mzee Dawson na vijanaย wake walikuwemo, kwa Mzee Dawson iliwaka ile saa ambayo Kiskoย alimuuliza Dawson kwanini alikuwa akiiangalia mara kwa maraย lakini wakati inawaka Mzee Dawson alikuwa ameshapoteza Fahamuย zake, wote walishangaa kuona saa ya Dawson imewaka ghafla naย kutoa mwanga wa kijani, katika saa hiyo kulikuwa na kitu kamaย ramani iliyokuwa ikizunguka ndani yake.ย
John Brain alishtuka sana baada kupata ishara kutoka katikaย moja ya saa yake ndogo ambayo mara nyingi alikuwa akitembeaย nayo, saa hiyo ilikuwa ikifanana sana na saa aliyokuwaย akiivaa Mzee Dawson! Akasimama na kutabasamu kisha akajikutaย mwenye furaha isiyo kifani.ย
“Baada ya miaka mingi hatimaye umeonekana, niliweka Maishaย yangu rehani kwa muda mrefu kukutafuta” Alisema John Brain.ย
Muda huo yule Mzee ambaye hakujulikana ni nani na ametokeaย wapi, alichukua kifaa kingine ndani ya sanduku, kifaa ambachoย kilikuwa kama simu hivi kisha akapiga mahali. Simu iliitaย ndani ya Ikulu, ilikuwa ni katika ofisi ya Raisย
“Mimi ni P55 Mbaga” ilikuwa ni sauti komavu kutoka kwa Mzeeย huyo, Rais alishtuka sana kusikia jina hilo yaani P55 Mbaga,ย akakata simu haraka sana baada ya kusikia hivyo kishaย akanyanyua simu kumpigia John Brain ambaye alikuwa katikaย hali ya furaha sanaย
“Mimi ni mfu John!!” Alisema Rais kwa sauti iliyooneshaย alikuwa kwenye butwaaaย
“Kivipi?” Alihoji Brainย
“P55 Mbaga amejitokeza!!”ย
“Imarisha ulinzi haraka, Naingia kazini kupambana naye”ย Alisema John huku tabasamu likiwa limeimarika katika suraย yake.ย
Muda huo yule Mzee ambaye ni P55 Mbaga alikuwa akitoka kuleย Msituni na kufunga safari ya kufuata uelekeo wa saa ya Mzeeย Dawson, alikuwa na kifaa chake alichokiamini sana, alionekanaย kuwa mtaalam wa kifaa hicho, Dakika tano baada ya vifaaย vilivyofungwa katika miili ya Six na Malaika kuwaka,ย iliwafanya wabadili maamuzi yao. Mpango ulikuwa ni kuwauwaย Sande na Mzee Dawson, haraka wakaingia kwenye gari naย kuondoka eneo lile, huku maswali yakiwa mengi vichwani mwao.
Yule Mzee alifika hadi eneo la Mashariki ya Bahari ya Hindi,ย kifaa kikamwambia kuwa alikuwa amefika eneo ambalo saa hiyoย ilikuwepo, muda huo Mzee Dawson alikuwa akirejea kwenyeย fahamu zake!! Alipoamka alishangaa kuona saa yake imewaka,ย akashtuka kisha akaulizaย
“Imeweka saa ngapi?” Aliwatumbulia macho vijana wake ambaoย walikuwa wamesimama mbele yake, alikuwepo Kisko na Chandeย
“Nusu saa iliyopita” alijibu Chande huku akimtazama Mzeeย Dawson aliyekuwa kitandaniย
“Na Sande yupo wapi?”ย
“Nafikiri yupo kwenye korido, unamuhitaji?”ย
“Hapana!! Nipe Maji ya kunywa” Alisema tena Mzee Dawson kishaย alikohoa na kutoa damu.ย
“Baba kwanini hii saa ni muhimu sana kwako umeamka hujaliย afya yako unauliza kuhusu saa?” Alihoji Kiskoย
“Nilikwambia hii saa ndiyo Maisha yangu, Mimi ni hii saa,ย niliisibiria kwa miaka mingi na jambo hili lilibakia kuwaย siri ambayo sina budi kuwaeleza mkiwa pamoja” Muda huo Chandeย alirejea akiwa na glasi yenye maji ya vuguvugu ambayo maraย nyingi Mzee Dawson alikuwa akiyatumia. Ghafla, Sande aliingiaย chumbani bahati nzuri Dawson alikuwa ameshapata fahamuย akasemaย
“Kuna Mtu anakuja upande huu, anaonekana kuwa anafuatiliaย jambo maana yupo bize na kitu mkononi, nafikiri ana GPS”ย Alisema Sande, Mzee Dawson akanyanyuka na kwenda kuangalia,ย alipofika dirishani alimuona Yule Mzee ambaye mara nyingiย alikuwa akishinda kule kanisani akajiuliza alikuwa amefuataย nini paleย
“Unamfahamu?” Aliuliza Sandeย
“Ndio….huyu Ni Miongoni mwa Wazee wa kanisa letu, najiulizaย amepajuaje hapa” Akajibu Mzee Dawson huku akionekana kujawaย na mshangaoย
“Niachie Mimi” Sande alisema kisha akashusha ngazi kuelekeaย chini, akafungua mlango kisha akatoka. Akakutana yule Mzeeย
“Wewe ni nani?” Alihoji Sande lakini kwa tahadhari sababuย Mzee huyo alikuwa makini kumtazama Sande na jinsiย alivyomtazama Sande aligundua Mzee huyo alikuwa na machoย makini kuliko maelezo.
Punde ikasikika sauti ya Dawson ikisemaย
“Mruhusu aje ndani” alipogeuka alikutana na macho ya Dawson,ย Mzee huyo akaruhusiwa kuingia ndani lakini tayari kila mmojaย alikuwa na umakini mno. Tembea ya Mzee huyo bado ilikuwaย makini sana, alionekana kutafuta kitu lakini alipoingia humoย kifaa chake chenye GPS kilizimika sababu nyumba hiyo ilikuwaย maalum kwa ajili ya kazi za kipelelezi hivyo ilikuwa ni ngumuย kwa baadhi ya vifaa kupenyeza.ย
Alipewa kiti akakaa kisha akaulizwaย
“Umefikaje hapa?” Aliuliza Mzee Dawson, yule Mzee akawatazamaย kisha akasema bila kujibu swali la Dawsonย
“Nimekuja kwa ishara yako Dawson, nimetoka mbali, nimesubiriย kwa miaka mingi kukuambia kuwa Dunia ilikuwa ikikutafuta kwaย miaka hiyo, nilikuficha kwa muda mrefu sana” Alisema Mzeeย huyoย
“Wewe ni nani hasa?”ย
“P55 Mbaga” Alijibu Mzee huyo na kusababisha mshangao kwaย Mzee Dawson ambaye alionekana kulifahamu jambo hiloย
“Haiwezekani, wewe ni Mzee wa kanisa umeijuaje siri hiyoย niliyoificha kwa muda mrefu!”ย
“Hukuificha siri hiyo, siri hii inajulikana ila kuwaka kwaย saa hiyo ni ishara kuwa mapambano yanaanza upya! Mapambano yaย kung’oa mizizi ya utawala huu wa Mabavu”ย
“Una maana gani?”ย
Mzee huyo alisimama kisha akasemaย
“Naitwa Mbaga, nilikuwa rafiki mkubwa wa Baba yako japoย alinizidi umri lakini alinipenda sana. Baba yako alikuwa niย miongoni mwa Askari wa ngazi ya juu, wakati huo, akatoroka naย nyaraka za siri ambazo alianza kuzisambaza kuhusu Urais waย Nchii namna unavyo rithishwa, uozo na ufedhuli uliokuwaย umejaa serikalini, aliishia kuuawa huku Taifa likiambiwa kuwaย Baba yako alikuwa ni muasi” Alimeza mate kisha akaendeleaย Mzee Mbagaย
“Kabla ya kuuawa kwake alinipa kifaa maalum, akaniambiaย unatakiwa kuvaa saa mkononi mwako na wakati wa ukomboziย utakapofika mimi nitakuja kukusaidia. Teknolojia hiiย iligunduliwa huko Ujerumani, mmoja wa Watu wa siri wa Baba yako walimwambia Rais juu ya Mpango wetu Mimi na Baba yako,ย nilitafutwa kila kona bila mafanikio yoyote yale, ndipo Babaย yako akapiga simu ukiwa masomoni ukabadilishwa Ubin wako iliย usitambulike, akakuandaa ukawa Mwanajeshi lakini Alipouawaย ulikuwa bado hujamaliza Mafunzo ya Kijeshi Nchini Cuba, Baadaย ya Teknolojia kugundulika wao wakatengeneza ya kwao iliย kujuwa muda na mahala ambapo nitawasha kifaa nilichopewa naย Baba yako kama ishara ya uhuru na ukombozi” Aliendelea kusemaย Mzee Mbaga na kuwaacha akina Dawson kinywa waziย
Machozi yalimtoka Dawson akakumbuka jinsi Mama yakeย alivyomwambia mpango huo, kuanzia kipindi hicho aliivaa saaย hiyo katika Maisha yake yote hadi anafikia uzee wa Makamo,ย alimkumbatia Mzee Mbaga. Taarifa hii ilikuwa ni ajendaa kuuย kwa kila Rais aliyetokea katika ukoo wa kurithi nafasi yaย Urais, alitafutwa sana Mbaga bila mafanikio na Marais Kadhaaย waliopita.ย
Comments ziwe nyingi apa KESHO itoke EPISODE NDEFU YA 11
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAย USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xxย
ย ย
15 Comments
Daah kitu inazidi kuwa pana kama vle inaisha kumbe nd kwanza inaanza
Admin unazid kunfurahisha
Kwisha kwisha ka mkubwaa
Mambo yanazidi kunoga
Hii kitu noma sana lete ingine
Hatar
Aaha jamaa anakatisha yan utamu
๐ฅ
โค๏ธ
Mambo yanazidi kua moto
Yes hadithi ni tamu sana
Yes hadithi ni tamu sana acha moto uwake
hiz ndo Hadith sasa
So nice story
Mambo yanzidi kunoga
Tupe. Ya. 11 Admin wetu