Ilipoishia “Unatakiwa kuwa makini sana sababu kwa namna alivyo huyo MtuΒ si rahisi akamuamini Mtu kwa Mara ya kwanza, unapaswa piaΒ kujuwa kuwa ukibainika basi kila kitu kitaharibika. Zola niΒ Jasusi mbobezi, kabla hujampeleleza anakuwa tayariΒ amekupeleleza.” Alisema John Brain, kisha Malaika kasema
“Zola anatumika kama Mwanvuli wa Serikali katika kutekelezaΒ mipango ya siri, najiuliza aliwezaje kukwepa mtego wa Bomu” EndeleaΒ
SEHEMU YA TATUΒ
Yalikuwa ni maswali waliyoulizana, Muda huo Inspekta ZolaΒ alikuwa kwenye gari yake akiwa anaelekea nyumbani kwaΒ Marehemu Robert. Kichwani akiwa na mawazo lukuki akajikutaΒ akimfikiria Msichana aliyeuwa polisi katika kituo cha polisiΒ tena kwa Ustadi ambao hata Komando asingeliweza kufanya.Β Akatikisa kichwa chake kisha katabasamu tuuΒ
Akaanza kuvuta picha namna Msichana yule aliyejitambulishaΒ kama Judith alionekana, alikuwa mwembamba, mweupe na mwenyeΒ sura ya upole sana. Pasipo kujuwa kuwa picha aliyokuwaΒ akiiwaza Zola haikuwa halisi kwani, hakuitwa Judith baliΒ alikuwa akiitwa Malaika, sura ile haikuwa halisi.Β
Alikanyaga mafuta bila kujuwa alikuwa akiwindwa sana auawe,Β dakika Thelathini na tano baadae alikuwa akiegesha gari lakeΒ katika uwa wa nyumba ya Robert. Huzuni ilikuwa imetanda sana,Β Mama Robert alipomuona Zola alimtambua kama Polisi aliyekuwaΒ akifwafilia tukio la vifo vile, akamkimbilia na kumwambiaΒ
“Mnipe mwili wa Mwanangu nimzike, Mnipe mwili nawaomba sana”Β
“Mama hebu tulia, nimekuja kwa ajili ya kuzungumza na wewe.Β Hebu futa machozi Mama” Alisema Inspekta Zola akiwa amemshikaΒ mabega Mama RobertΒ
“Hebu tuongee vizuri” Zola akapepesa macho yake, kulikuwa naΒ Watu wengi pale Msibani akaona sehemu ambayo ilikuwa tulivuΒ bila Watu, akamsogeza Mama yake Robert hukoΒ
“Mama hebu nieleze vizuri tukio lilitokeaje? Kuna utata sanaΒ katika jambo hili” Alisema Zola huku akiwa makini kutakaΒ kusikia ambacho Mama Robert angesemaΒ
Mama Robert akajifuta chozi na kujituliza kidogo kabla yaΒ kumsimulia ZolaΒ
“Tulikuwa kanisani wakati tunasubiria ndoa iweze kufungwa,Β ili Mwanangu Robert amuowe Sandra. Nilishtuka kusikia mlio waΒ Risasi, nilipogeuka nikamuona Mwanangu akiwa ameshikiliaΒ Bastola huku miili miwili ya Bosco na Sandra ikiwa chini,Β katika hali ya taharuki kila mmoja akipiga kelele za woga,Β Robert aliubeba mwili wa Sandra na kuondoka nao akiwa analia”Β Mama Robert alianza kulia kwa uchungu hadi Inspekta ZolaΒ alijikuta akidondosha chozi lake kwa jinsi ambavyo MamaΒ Robert alikuwa akilia kwa uchungu.
“Naomba msaada wako niipate maiti ya Mwanangu Robert iliΒ nimzike Mimi”Β
“Sawa! Mwili wa Robert utaupata baada ya kumaliza uchunguziΒ ambao kwa asilimia kubwa naweza kusema Umeisha, nisaidieΒ namba ya Mama Sandra ili niweze kuzungumza nae”Β
Zola akapewa namba akaelekezwa anapoishi Mama Sandra,Β akamuaga Mama Robert kisha akaingia kwenye gari yake ambayoΒ ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kuzuia risasi kuingia, gariΒ hili lilinunuliwa na Mzee Dawson kwa ajili ya kazi zaΒ kipelelezi.Β
Mwendo wa dakika arobaini na nane, Zola alikuwa ameshafikaΒ alipoelekezwa, haikuhitaji sana ujuzi wa kutambuwa kuwa eneoΒ hilo lilikuwa na tatizo licha ya ukimya na uchache wa WatuΒ uliopo pale. Zola akajipenyesha hadi Ndani ambako Mama SandraΒ alikuwepo lakini kabla hajafika huko alikutana na Baba SandraΒ ambaye alimtambua Zola kabla hata hajajitambulisha.Β
“Umefanikiwa kujuwa chanzo cha kifo cha Binti yangu?”Β Aliuliza Baba yake Sandra ambaye alikuwa na umri sawa na ZolaΒ
“Ngoma ngumu lakini tutafikia tamati hivi karibuni”Β
“Tutashukuru sana ili tuweze kumpumzisha Sandra katika nyumbaΒ yake ya milele na hayo mengi tutayaachia jeshi la Polisi”Β
“Usijali! Nimekuja kuzungumza kidogo na Mama Sandra, hapanaΒ shaka yupo Kushoto chumba cha mwisho” Alisema Inspekta ZolaΒ huku akiachia tabasamu la kaziΒ
“Jicho lako la kipelelezi liko sahihi Afande, nenda tuuΒ kazungumze nae” Zola aliposikia kauli ya utii namna ileΒ aliona amtamzame Mzee huyo Usoni pake, akahisi jambo lakiniΒ akaliweka kiporo kichwani pake. Hata alipokaribia mlango waΒ chumba alichopo Mama Sandra aligeuka na kumuona Baba yakeΒ Sandra akiwa bado anamfwatilia Zola kisha alipoona ZolaΒ amegeuka akajifanya kuondoka pale. Zola akagundua jamboΒ fulani, akabisha hodi kisha akaruhusiwa kuingia chumbaniΒ
“Pole Mama! Samahani naomba wote mtoke ili nizungumze na MamaΒ Robert, Naitwa Inspekta Zola” Alisema kisha akatoaΒ kutambulisho, Watu walioko mle waliondoka taratibu huku ZolaΒ akipata nafasi ya kuangalia picha iliyopo Ukutani, ilikuwa niΒ picha ya Sandra akiwa shuleniΒ
“Hapana Shaka huyu ni Sandra katika umri wa ukuaji wake?”Β Alihoji Zola huku akiendelea kuiangalia, Mama SandraΒ akaitikia kwa masikitiko
“Ndio…Ameondoka nikiwa namuhitaji Mwanangu” AliposemaΒ alijikuta akianza kulia upya ni kama vile aliweka chumviΒ kwenye kidonda kibichi, Zola alisogea kisha aliketi chini kwaΒ mtindo wa kufunga miguu yake kama Waislam wakaavyo.Β
“Mwanao alipaswa kuolewa na Robert, lakini Huyo RobertΒ aliondowa uhai wake kabla hata ya harusi. Unafahamu nini katiΒ ya hawa Watu watatu yaani Bosco, Robert na Sandra Mwanao”Β
“Sandra alifahamiana na Robert muda mchache sana ndipoΒ akasema anataka kuolewa, lakini Robert na Bosco inasemekanaΒ ni marafiki wa muda mrefu sana”Β
“Vifo vyao unaweza ukahisi vinatokana na nini Mama?” MamaΒ Sandra alitikisa kichwa chake kisha akasemaΒ
“Ni ngumu sana kwa jinsi ambavyo walikuwa wakija hapa naΒ kuongea kwa furaha sana, sijui nini kimesababisha haya yote”Β
“Asante Mama! Hii ni namba yangu ukipata chochote nijuze,Β mtapewa mwili wa Sandra kwa ajili ya maziko huku uchunguziΒ mwingine ukiendelea” Zola alijizoa na kuondoka pale hukuΒ akili yake ikianza kumtafakari Baba yake Sandra kwaniniΒ alikuwa akimtazama sana?Β
Akiwa kwenye gari Zola alionelea aelekee Hospitali ambakoΒ miili ile ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi, alipofika alikutanaΒ na mtaalam wa Maabara kutoka katika kitengo cha MPA Cha MzeeΒ Dawson akamwambia kuwa ile miili miwili ipelekwe kwa wahusikaΒ kwasababu ni miili halali ya wahusikaΒ
Zola aliondoka Hospitali na kuelekea katika makazi yake yaΒ siri ambayo Watu wengi walikuwa hawayafahamu, wakati anafikaΒ akakumbuka kuwa ujumbe wa picha ulikuwa umeshatumwa, akaingiaΒ chumba cha siri kwa ajili ya kufanya alichokusudia, alihitajiΒ kujuwa ule mwili bandia ni wa nani. Akaingiza picha katikaΒ mashine yake ya Kazi akapata majibu yaliyomfanya afungeΒ safari nyingine kuelekea Chuo Kikuu cha Sayansi ya Mifupa.Β
“Namuulizia Anastanzia Nyange” Aliuliza Zola akiwa ameketiΒ mbele ya Mkuu wa Chuo hicho ambaye macho yake yalikuwaΒ yametua kwenye sura ya ZolaΒ
“Anastanzia Nyange?” Aliuliza Mkuu wa Chuo ambaye alikuwa naΒ kitambiΒ
“Ndio, picha yake hii hapa” alimuonesha picha
“Ameenda Field na wanachuo Wenzake Kaskazimi Mashariki mwaΒ Mkoa jirani”Β
“Ok asante” Zola aliondoka pale, nyuma yule Mkuu wa ChuoΒ akanyanyua simu ya mezani akapiga sehemu akaisikilizia hadiΒ ilipopokelewa kisha akasemaΒ
“Amekuja hapa muda sio mrefu anamuulizia Anastanzia Nyange”Β Aliposema hivyo hakuhitaji kusikiliza sauti kutoka upande waΒ pili akakata simu kisha akaweka mikono yake juu ya meza hukuΒ akionekana kuzama katika tafakari nzito sana.Β
Zola kabla hajaondoka pale Chuoni alikutana na MwanachuoΒ mmoja akamuuliza kama anamfahamu Anastanzia, yule MwanachuoΒ akamwambia Zola kuwa anamfahamu Anastanzia lakini hakuonekanaΒ hapo chuoni kwa siku saba. Zola akajitambulisha kuwa niΒ polisi akamuomba Yule Mwanachuo amueleze mahali ambapoΒ Anastanzia alikuwa akiishiΒ
“Anaishi na Rafiki yake sio mbali sana ni nyuma ya HoteliΒ mpya ya Sub Marine, ukifika utaona jengo la Njano lina vigaeΒ ndio hapo hapo”Β
“Asante sana” Zola alifunga safari nyingine ya kuelekea hukoΒ alipoelekezwa, alitumia dakika ishirini pekee kufikaΒ akakutana na Mtu nje ya nyumba hiyo hapana shaka alionekanaΒ kuwa mwenyeji hapo, Zola akamuulizaΒ
“Nimemkuta Anastanzia?”Β
“Salimia kwanza, waungwana husalimia sasa unapouliza tu HataΒ hujui unayemuuliza kama ni Mzima au la” alifoka Mtu huyoΒ ambaye alikuwa ni Msichana wa Makamo tuu.Β
“Samahani! Namuulizia Anastanzia”Β
“Chumba chake kile pale” alioneshwa kisha Zola akashukaΒ kwenye gari na kuelekea kubisha hodi.Β
Kiatu cheusi cha Zola kilikuwa kinang’aa na kumfanya msichanaΒ huyo kujuwa kuwa Mwanaume huyo alikuwa na pesa sana, kishaΒ akapeleka macho yake kwenye gari ya Zola kisha akaingiaΒ chumbani kwake.Β
Muda huo zola alikuwa akibisha Hodi huku macho yake yaΒ Kijasusi yakiangaza huku na kule, ukimya uliomuitikia ulimpaΒ wazo la kujaribu kufungua pale ili aweze kuchunguza vizuri,Β akarudi kwenye gari yake kisha akafungua begi dogo akatoaΒ rundo la funguo za Bandia, akachagua ambayo iliendana naΒ kitasa cha pale Mlangoni. Akarudi mlangoni na kufunguaΒ taratibu sana bila hata sauti ya kufungua kusikika, sekundeΒ chache akajikuta amefanikiwa kuingia ndani. Alikuwa makiniΒ sana, sehemu hiyo ilikuwa na chumba na sebule.Β
Muda huu alikuwa pale sebleni, palionekana kuwa tulivu sanaΒ huku feni ikiwa inaendelea kupepea, ilimfanya aamini kuwaΒ kulikuwa na Mtu aliyekuwa akiishi pale, akili yakeΒ ikayakumbuka maneno ya yule mwanachuo kuwa Anastanzia alikuwaΒ akiishi na rafiki yake, Zola alimuhitaji zaidi huyo rafikiΒ yake sababu alishafanikiwa kujuwa kuwa Anastanzia amekufaΒ katika lile tukio kule kanisani, akanyata taratibu aliposikiaΒ mlio wa simu ukilia kutokea chumbani, akapinda mkonoΒ akachomoa Bastola yake yenye kiwambo cha kupoza sauti yaΒ risasi itokapo.Β
Akageuka nyuma kuhakiki kuwa hakukuwa na Mtu pale sebleni,Β kisha akaanza kuelekea chumbani ambako ile sauti ya simuΒ kuita ilikuwa ikiendelea kusikika. Akameza mate taratibu hukuΒ kijasho cha umakini kikiendelea kutiririka katika paji lakeΒ la Uso, Kisha kwa mwendo wa haraka akaingia chumbani hukuΒ akiangaza Bastola yake huku na kule, kitandani aliona MtuΒ akiwa amelala huku sura ya huyo Mtu ikiwa inatazama ukutaniΒ na kumpa wakati mgumu Zola kujuwa ni nani aliyelala pale,Β taswira ilionesha ni Mwanamke kisha akili na moyo wa ZolaΒ ukajipa tumaini la kumpata rafiki wa Anastanzia ambayeΒ anaweza kuwa Mwangaza wa kumpa mwanga Zola kuhusu kesi ile yaΒ Utata sana iliyoibua taswira ya nani alihusika na kifo chaΒ Makam wa Rais..Β
Bastola ikiwa mbele Zola alionekana kuwa makini huku akizidiΒ kusogea karibu na Mtu huyo ambaye hakumtambua hadi muda huo,Β alipomfikia akamgeuza kwa kutumia bastola yake, mambo hayaΒ aliyafanya akiwa na unri wa miaka zaidi ya 50 sijui alipokuwaΒ kijana Zola alikuwa hatari kiasi gani kwenye upelelezi wake,Β akashusha miwani na Bastola yake taratibu akapelekea kidoleΒ eneo la shingo kisha kwenye pua, ubaridi wa Mtu huyoΒ ulionesha kuwa alikuwa amekufa muda mrefu sana, povuΒ ililikuwa likimtoka puani, alipomchunguza vizuri aliona ileΒ alama ya vidole kwenye paja la Marehemu.Β
“Shit!” Alisema huku akili yake ikimpa majibu kuwaΒ waliohusika na matukio ya kikatili, waliomuuwa Makam wa RaisΒ ndio waliosababisha kifo kile, haraka Zola akachukua simuΒ yake na kumpigia Mzee Dawson ambaye alimpa kazi ile iliyojaaΒ utata sana, Simu hiyo ilipokuwa ikiita Mzee Dawson alikuwaΒ akistarehe na Msichana mmoja nyumbani kwake, alipoona simu yaΒ Zola akaacha kisha akamwambia Msichana huyo avae aondokeΒ haraka. Mzee Dawson akajitupa kitandani akiwa hoi kishaΒ kapokea simu ya Zola
“Unasemaje Zola?” Aliitika Mzee Dawson kwa sauti ya uchovuΒ sanaΒ
“Unapaswa nawe kuingia kazini, vinginevyo mambo yanawezaΒ kuharibika kabisa. Nilikuwa nafuatilia kuhusu vifo vya utataΒ vilivyotokea kanisani, mmoja wa Watu ambao wangeliweza kunipaΒ Mwangaza wa kesi hii nimemkuta akiwa amekufa nyumbani kwake,Β Watu hawa wapo macho na wananifuatilia”Β
“Nilikueleza kuhusu hilo Zola, nilikupa pia msaidizi iliΒ akusaidie lakini cha ajabu hutaki kuwasiliana naye kabisa,Β unataka niingie kwenye majukumu hayo?”Β
“Dawson unajua fika huwa simuamini Mtu katika mambo yangu,Β napenda kufanya kazi mwenyewe lakini hili linahitaji utulivuΒ zaidi kitu ambacho maadui zetu hawataki kunipa”Β
“Aaaah Zola” ilisikika sauti upande wa Mzee Dawson, ikioneshaΒ alikuwa akijigeuza.Β
“Hebu fanya taratibu tuonane ana kwa ana Mzee Dawson, nahisiΒ kuchanganikiwa sasa” Zola alikata simu bila kusikiliza sautiΒ ya Mzee Dawson, baada ya hapo akapiga simu sehemu nyingineΒ ndani ya kitengo cha siri cha Mzee Dawson kinachoitwa MPA,Β akaomba madaktari waweze kufika eneo la tukio, akawapa RamaniΒ kamili lilipo eneo hilo.Β Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNEΒ USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Β Β
14 Comments
Mimi wa kwanza kusoma kazi nzur sana
βοΈβοΈ
Nzuri
Ngoma ngumuβοΈβοΈβοΈ
Kama nimeielewa ivi
Bonge moja la kazi
Kazi Iko poa japo mmmmh
Iko poa sanaaaaa
Noma sana
Kali sana
kama mimi tu navurugwa na mkasa huu je huyo zolaπ, hapo kijiwen niπ₯π₯π₯π―π―
Hatari sana
Akakunja miguu kama wakaavyo Waislam π
No!aaa sana