Ilipoishia ” Minnie ndo kwanza akawapita akisogea mezani nakuanza kumenya nanasi, wakazidi kumtizama jinsi ambavyo hana muda nao, Alexander ikabidi amsogelee karibu akisimama nyuma yake akimuongelea sikioni.
“” Please Minnie acha maigizo basi, Nyumbani wanakusubili wewe, kumbuka ahadi yetu Mimi na wewe niliahidi kutoivunja,, angalau kwa hili niamini turudi wote basii.”Ā Ā
EndeleaĀ
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Maina akaona kama Alexander anataka kujimaliza kwa Minnie iweje ambembeleze namna Ile kweli Kuna haja ya kuambatana nae? Akafanya kumshika mkono akimvuta.
Ā Ā Ā “” Alexander Baby! Muache kwanini unamlazimisha namna hiyo? Yeye haoneshi kuongozana na wewe basi twende.””
Muda huo huo Simu ya Alexander ikaita alikuwa ni Bibi kampigia simu, akawa kapokea huku akisogea pembeni akimsikiliza.
Ā Ā Ā “” Wewe upo wapi au Minnie kakugomea? Alex na Sandra wamefika Airport! Kama hakuelewi mpatie simu.”
Alexander akabaki kumtizama Minnie alichoamua ni kumpelekea simu, Minnie ikabidi asikilizie sauti.
Ā Ā Ā “” Minnie mjukuu wangu tafadhari usiniangushe huku mnasubiliwa nyie tu, halafu Alexander yupo na Maina..!?”
Minnie akamtolea jicho Maina akawaza aseme au akaushe tu ikabidi azungumze.
Ā Ā Ā “” Hapana nipo na Alexander,,, mh lakini sijajiandaa..!?”
Ā Ā Ā “” Aaa mjukuu,, kujiandaa gani hebu njoo hivyo hivyo!”
Ā Ā Ā “” Sawa Bibi.””
Minnie akampatia simu Alexander Kisha akaendelea kula nanasi.
Ā Ā Ā “” Maina karibu tule, huyo mchumba wako yeye amekula ndio maana ana nguvu hata za kupambana na Mimi?” Ni vile Minnie aligundua kabisa Maina anamezea mate Yale matunda.
“” Aaah… Nanasi lenyewe Chachu kweli nahisi ni kama wewe tu ulivyo.”
Minnie ikabidi acheke tu yaani yeye alifananishwa na uchachu wa nanasi Daah mbona alimuona hivyo lakini? Akafanya kuinuka huku akiingia chumbani.
Muda huo Alexander akakata Simu huku akimtizama Minnie jinsi anavyopandisha juu.
“” Bibi kasema tuondoke na Minnie.. !? Lakini Bibi nae yupoje huyu huoni ataenda kufanya jambo letu lisikamilike?”
Ā Maina akawahi kuongea.
Alexander hakuwa na chakuzungumza zaidi ya kumsogelea na kumkumbatia.
Ā Ā Ā “” Usijali kila kitu kitaenda sawa, kumbuka muoaji ni Mimi! Wazani naweza pigwa?”
Maina akahisi kufarijika kwa maneno ya Alexander ikabidi amkumbatie zaidi.
Minnie muda huo ndio anatoka chumbani akiwa na kibegi Cha mgongoni, Alexander akawahi kumuona huku akijiachia kwenye kumbato la Maina akimtizama mtoto mdogo mdogo mwenye urembo wake wa athili hakuwa na makolombezo mengi kama wewe ambavyo ungetaka kuonekana, baada ya kumtizama sana akawa anatizama mwili wake kwa ujumla Kisha alimuuliza…
Ā Ā Ā “” Vipi kuhusu mavazi yako ndio hayo utaingia nayo White House?”
Maina ndio akashituka ni kama akili yake ilikuwa mbali muda huo, ndio akamtizama Minnie, lakini akaona ngoja amuenjoy akadhalilike.
Ā Ā Ā “” Aaa Bwana Alexander mbona chicha tu,, Anaweza kuingia hivyo hivyo atabadili mavazi akifika white house ndani.””
Alexander hakulizika kabisa na mavazi ya Minnie kuingia white house, ikabidi aongoze njia huku Minnie akizitanguliza hizi couple mbili akizitathimini kwa muonekano wao akaishia kutabasamu tu huku akizungumza.
Ā Ā Ā “” Si umuoe tu Maina! Mimi nikiwa mfanyakazi wa White House itanifanya nifatilie mambo yangu haraka kuliko kusimama kwa ubini wa Mrs Alexander.”
Walifika kwenye gari Minnie hakutaka kuwasumbua zaidi ya kukaa nyuma akiendelea kuchezea simu, Alexander akawa anamtizama Minnie kupitia sait mirror alivyo busy na simu akaamua kuchukua simu yake na kumtumia Message.
Ā Ā Ā “” Ni kweli hauna mavazi mengine ya kubadilisha?Ā Kama hauna basi nipite dukani mara moja uchukue.””
Minnie akawa ameiona Ile message akaisoma Kisha akacheka tu, akiijibu. “” Kwani Kuna maungio umeona..?”
Alexander akasoma akipandisha pumnzi juu na kushusha akaona siyo mbaya kuingilia muonekano wa mtu ikabidi arejeshe simu yake mfukoni akiendelea kuongea na Maina.
Ā Ā Ā “” Unajua ni Miaka mitatu Alex aende jeshini halafu leo tunaonana tenaa, Sandra nae ana miaka mitatu vile vile huyu kuja kwake ni mpaka asikie Alex yupo. Nahisi kuwa na furaha sana Leo.””
Maina akatabasamu tu huku akijilaza begani kiuchookozi kabisa Nia ni kumuumiza Minnie tu.
Ā Ā Ā “” Hata Mimi nafuraha sana kwa vile nakuona Leo ni mwingi wa furaha yaani napenda siku zote uwe hivi, Sema Minnie anatuingilia tu.”
Alexander ikabidi acheke tu huku safari yao ikichukua nafasi kubwa ya kufurahia kwa maneno machache yenye furaha.
Mwisho kabisa walifika kwenye jengo kubwa la White House, Minnie akabaki kulitazama kwa hasira akisoma maneno yaliyoandikwa pale, WELCOME WHITE HOUSE HOLL” “” Ooh eti ukaribisho huku si kuzimu kabisa? Hapa inatakiwa nifunge kikoi Sasa, Najua Maina ulitaka Mimi niaibike lakini Mimi sio mjinga namna hiyo nilitaka kuwakela tu.”
Geti la White House likafunguliwa gari ikazama ndani Hadi sehemu ya kuegeshea magari, Minnie akafungua begi lake akavua raba na kuvaa sendo Kisha akachukua na kikoi akifanya kukifunga kiunoni kwake.Ā
Muda huo Alexander pamoja na Maina walikuwa wameshuka wakimsubili atoke, ndio anafungua mlango taratibu akishuka wote wakamshangaa inamaana alifunga kikoi?” Alexander furaha ikatawala usoni akaona hapo sawa hakusita kutembea kwa kibuli akionesha majigambo yake katika white house, taratibu kumbukumbu za kwao Minnie zikaanza kujengeka kichwani anakumbuka jinsi alivyomfanyia mauza uza akiwa ndani ya nyumba hiyo, anazidi kufikilia tenaa inamaana wakati ule amuwekee bastola kichwani yote ilikuwa ni kumtisha kisa yupo kwao? Na vipi kwa yeye akiwa White House labda alifaa kumfanya nini Binti huyu?”
Minnie wakati huo hana hili Wala lile kuwa Kawa kichwa Cha habari kwa Bwana Alexander, yeye alizidi kuingia ndani mwisho Bibi pamoja na Mirii( Miricka) wakafika kumpokea kwa furaha, Bibi akafanya kumshika kichwani kwanza.
Ā Ā Ā “” Afadhari umerudi Mimi Bibi yako na Amani Sasa.””
Ā Ā Ā “” Waoo ma’mdogo tulikumisi..” Mirii nae akaja kujaza ujazo pale.
Sauti nzito ya kiume ikasikika ikikohoa, Minnie ikabidi atizame inakotokea ndio anamuona Bright akimnyoshea mkono inamaana alitaka na yeye kumkalibisha kwa kumbatio? Minnie hakuwa na shida kwenda kumkumbatia.
Ā Ā Ā “” Ooh shemu mpo jamaniii..!”
Minnie akaongea huku akimuachia huku wakisogea wote kwa Bibi.
Ā Ā Ā “” Brighton, Mirii inabidi na nyie mjiandae Sasa make mmekuwa nje muda wote wewe na mwanao mkiweka mazingira safi, basi kajiandaeni sherehe inaanza muda si mrefu. Minnie kajiandae pia Kuna zawadi yako kitandani, halafu huyo Maina mwambie namuita huku.””
Minnie ilibidi aondoke kuelekea kwenye chumba chake alifika akagonga Mlango, sauti ya mziki uliokuwa mle ulikuwa mkubwa mtu kusikia ni ngumu, ikabidi Minnie aliunge hadi ndani anafungua Mlango anaona watu wapo kitandani wakitomasiana Minnie ikabidi akohoe ndipo wakasituka na kuinuka haraka huku Alexander akifanya kufunga visikizo vya shati lake.
“” Unaingia ingia ovyo, unazani hapa ni Bar? Utaingia nakutoka muda wote. Mbona huna adabu namna hiyo?”
Alexander akafoka huku akimsogelea Minnie huku jicho likiwa jekundu.
Ā Ā Ā ” Mi,,Ā mimi nilibisha hamkusikia.”
Maina akasogea karibu akainua mkono kumuwasha kofi, Minnie akadaka nakuukunja huku akimsogeza mlangoni.
Ā Ā Ā “” Minnie hayupo hivyo unavyofikilia wewe! Hebu kuwa na mipaka yako Maina, kingine Bibi anakuita huko nje.””
Ā Ā Ā “” Weee muache tafadhari, unathubutu vipi kumnyanyulia mkono.”
Alexander alifoka Maina ndio akaona kapata nafasi ya kudeka akafanya kumkumbatia Alexander eti katendewa ubaya?”
Ā Ā Ā Ā “” Okay, Maina usijali nitamuonya! Naomba kaongee na Bibi halafu kajiandae mapema tuna nusu saa sherehe inaanza.”
Maina akafanya kumbusu shavuni hakutaka kuondoka mkavu mkavu namna Ile.
Minnie yeye akajiweka busy na mambo yake hata hivyo hayamhusu, alitizama gauni aliyoandaliwa kuvaa kwanza kweli ilionekana ni nadhifu sana! Ilibidi achukue begi aliokuja nae ndio lilikuwa na baadhi ya mafuta yake ambayo angeyatumia baada ya kuoga, alifanya kuyaweka Dressing table Ili aingie bafuni kujiandaa kwanza.
Alexander ndio akarudisha Mlango huku akimtizama Minnie anavyofikilia kukaa kwenye chumba hicho na yeye labda angejiandaa vipi akiwa nae, Alexander ikabidi aingie bafuni kuoga kwanza Kisha alirudi akiwa na taulo tu ambavyo siyo kawaida yake mara nyingi huvalia bafuni.
Minnie akawa anamtizama kwa kuibia mwisho akaamua bora kujilaza kwanza asimtizame.
Ā Ā Ā “” Kajiandae haraka, Nisije beba lawama nimekuchelewesha.”
Ā Ā Ā “” Kwani ushavaa…!!?”
Alexander akahisi kucheka tu inamaana alimuogopa kumuona yupo wazi.
Ā Ā Ā Ā “” Lakini wewe si mkewangu..? Kuna uhusiano gani wa kuuliza hivyo?”
Minnie hakutaka kuendelea kuuliza tena zaidi ya kuinuka asitizame upande mwingine alichukua gauni lake lilokuwa kitandani Kisha akaingia nalo Moja kwa moja bafuni.
Ā Ā Ā “” Ahaa!! Kweli naishi na mwendawazimu humu ndani, ngoja tuone hatima itatimia vipi Mimi na huyu Bandit girl, Leo kwakuwa tunasherehe nisingetaka nikwaruzane na wewe ndugu zangu wakanichukulia tofauti, nipo radhi kuepukana na kelele zako.”Ā
Alexander alimaliza kujiandaa huku akitana nywele zake vizuri, vazi la suit lilikaa vizuri kwenye mwili wake hata yeye alivyojitizama kwenye kioo aliona ni Prince katika White House, kwanza alijiona ni kama Suleiman kwa mvuto wake katika vitabu vya dini bilashaka hata tembea yake alifaa atembee ki Prince.
Mlango wa bafuni ukafunguliwa alikuwa ni Minnie kavalia gauni lake refu lenye rangi ya blue bahari lililoonesha kuushep vizuri mwili wake, alipiga hatua kwa wasiwasi akitizama chumba chote kama Alexander yupo pale lakini alijihakikisha hayupo ikabidi asogee kwenye dressing table yake akianza kufunga vizuri nywele yake, lakini ndio akakumbuka hata zipu ya gauni lake Alishindwa kuifunga vizuri ilibidi aachane na nywele kwanza akasimama akielekea kunako kioo Cha kabati la nguo hiki kilitosha kuonesha mwili wake vizuri, alihitaji kufunga lakini ikawa ngumu akaona msaada uliopo ni kumtafuta Mama Mirii huyu ndie anaonekana kuwa karibu yake.
Alitoka nje kuchungulia haoni mtu akaona hapa ni kutafuta namna nyingine ya kufunga zipu! Alichukua enka ya nguo akijaribu kuvuta zipu lakini haikusaidia, Ghafla alihisi Kuna mtu kama kamsimamia nyuma yake alishituka na kumuona Alexander akiinua mikono yake na kushika Ile zipu akawahi kujitoa.
Ā Ā Ā “” Acha nitafanya mwenyewe, uliona nimeshidwa…?””
Alexander hakutaka kumjibu zaidi ya kumshika mikono yake na kumfungia Ile zipu baada ya kumaliza alitoka.
Ā Ā Ā Ā “” Sasa mbona unatoka, wameanza hizo sherehe zenu, make hapa White House hamuishi kukuza jambo, kwani Kuna ulazima wa kufanya sherehe kuwakaribisha wao…?”
Alexander muda huo alikuwa kafika mlangoni ilibidi asimame kwanza aking’ata midomo yake kwa hasira anajiuliza huyu mwanamke mbona ni muongeaji vile na sio kama Maina? Ikabidi aondoke tu.
Huku kwa Minnie alimaliza kujiandaa Kisha alivalia necklace iliofanania na hereni pamoja na blaclet yenye madini ya Shaba, Kisha alichomeka mguu wake kwenye kiatu kirefu wengi wao wavaapo kiatu hiki hata motion hubadilika, huonekana ni kama miss Tanzania yupo jukwaani kuonesha umaridadi wake mbele ya hadhara, labda watu wote wavutiwe na motion yake, Mimi sijuiš.
Huku kunako Sherehe sauti ya vigelegele ilisikika namuda huo Alex pamoja na Sandra walikuwa wakipokewa pale kwa furaha sana, Bibi ilibidi awafuate wajukuu zake wawili akiwakumbatia kwa pamoja hakutaka maneno mengi zaidi ya wao wakajiandae waingie kwenye sherehe.
Sauti za shagwe zilisikika Hadi chumbani kwa Minnie ilibidi afungue dirisha akibaki kutazama nje na kuwaona wageni waliotarajiwa wapo pale, Minnie akawa na shauku sana ya kuwaona lakini watu waliokuwa pale walizidi kumziba kwa kumsalimia muda wote akaona sio mbaya hata hivyo anae wakati mzuri wa kuonana nao leo.
Huku chumbani kwa Mama Mirii alikuwa akijiandaa vizuri huku akiwa na shauku ya kumpokea huyo Alex kwani ndie Mmewe sasa.
Mlango ukafunguliwa, Mashallah! alimuona mmewake kipenzi hakusita kujirusha kwenye kifua kipana Cha mwanaume huyu huku akitulia kwa sekunde akizidi kuvuta manukato yalivyojaa kwenye mwili huo, baadae alijiengua taratibu akirudisha uso wake amkague vizuri, machozi ya furaha yalitiririka, Alex nae akafanya kumfuta tu Kisha alimbusu kwenye paji la uso na kumkumbatia teenaa.
Ā Ā Ā “” Nilikumisi sana mkewangu kipenzi, ilikuwa ni ngumu sana usiku waku kukamilika pasina kuiona sura yako, Nilishidwa kujizuia kutizama picha yako na ya mwanangu angalau tu nipate usingizi,, unajua Nini mama Mirii.. Nakupenda sana yaani. I loved!”
Alex aliamua kujimaliza kabisa angeshidwa vipi kutamka maneno Yale kwa Mkewangu wake kipenzi wakati yupo nae bilashaka wakati huo asingemaliza maneno yake yasiyoishwa hamu kuyatamka muda huo, Sauti ya Mlango iliwashitua na kubaki wote wametoa macho kuangalia mlangoni ndipo wanamuona mtoto wao Mirii aliachiwa tabasamu zito huku asisite kumwambia Baba’ke”” I miss you my Daddy” Aweeee…. Alex hakusita kumnyanyua princess wake juu juu huku akimbusu katika Mashavu yake huku akimkalisha kitandani.. “” Baba’ko anae suprise kwako a you already?” Mirii akawa katikisa kichwa akimtizama Baba’ke akifungua begi na kutoa gauni zuri akimpatia.Ā “” Leo utavaa hii.””Ā
Ma Mirii yeye bado haishi kumtizama mmewake ni kama alikuwa mgeni mpaka Alex akajishitukia akamtizama mkewe wakawa wametabasamu pamoja.
Ā Ā Ā “” Unahisi nimekusahau…? Ninayo zawadi yako nzuri hakika leo inabidi Mimi pamoja na vipenzi vyangu tufananie kwa mavazi haya.”
Akatoa gauni zuri akampatia, gauni refu lenye rangi ya pink lilifanania kidogo na la Mirii, Mama Mirii hakusita kumkumbatia mmewe akimshukuru kwa zawadi Ile.
Huku chumbani kwa Minnie alikuwa akizunguka akisubili kufatwa make asingeweza kutoka mwenyewe!Ā
Alexander akawa amefika Minnie ndio akabaki kumtizama vizuri hakika alipendeza sana, Alexander nae akawa akimtizama vile vile kwa sekunde chache lakini hakupaza sauti yake kumsifia zaidi ya Kila mtu kumsifia mwenzake kimya kimya akisema “” umependeza sana kwa vazi Hilo”Ā
Minnie ndio akawahi kujishutukia akiangalia pembeni ni kama eti alikuwa akitizama picha ukutani.
Ā Ā Ā “” Upo tayari twende..? Kingine sitaki tabia za ubandit kwenye sherehe naomba ukae kwa kutulia halafu sijasahau ulichonifanyia nyumbani kwenu, kwasasa kumbuka upo nyumbani kwetu hutanizuia kufanya kitu chochote nitachotaka.”
Minnie hakumjibu zaidi ya kumkazia jicho huku akimfata nyuma nyuma.
Ā Ā Ā “” Wewe tangu lini mwanaume akatangulia, Aya nikuone mbele yangu.”
Ā Ā Ā “” Ushaanza kuninyanyasa kisiasa.” ” nikisema kabisa hapa ni kuzimu sikukosea.”
Ā Ā Ā “‘ Wewe mbona unazungumza kimya kimya? Halafu tembea Gani hiyo au mavazi haya hukuzoea… Binti Mzobe..!? Ahaa,, inafurahisha! olewako uanguke hadhara bora uangukie hapa, nilikuona mle ndani kumbe ulikuwa ukifanya mazoezi ya kutembea …..?”
Minnie akaona asimame ni vile kakumbuka mizunguko aliyoifanya ndani kumbe alikuwa akitizamwa? Alexander akawa kamfikia na kumshika mkono lakini Minnie akamtoa.
“” Sijawa gari bovu la kuwekewa sapoti ya kutembea, naweza kwakuwa sifananii na vile wataka.”
“” Okay vizuri twende.”
Muda huo huo Alex pamoja na mkewe na wao wanatoka wakawa wamekutana Kona, Alexander ikabidi awahi kwa Kaka’ke akimshika mkono, Mirii yeye akawahi kwa Minnie akimkumbatia.
Ā Ā Ā “” Waoo ma’mdogo you looking so good.”
Minnie akatabasamu tu huku akimtizama Mama Miricka wakawa wamecheka wote, Sauti ya kipaza sauti ikasikika ikiwaomba wafike kwenye sherehe haraka.
Ā Ā Ā “” Lakini Alexander nilitaka nimuone shemeji yangu kwa ukaribu umeniwahisha kunitoa pale hata sijamuona ujue.”
Ā Ā Ā “” Aaa utamuona tu hata hivyo tunahitajika.”
Ā Ā Ā “” Vipi Maina hakusumbui lakini.?”
Ā Ā Ā “” Wewe acha tu, hii leo sijui mambo yatakuwaje, ila nimepanga nitangaze Ndoa na yeye..”
Alex ikabidi asimame kwanza anafikilia huenda utani.
Ā Ā Ā “” Hivi upo sawa kweli wewe? Na mkeo vipi au ulimuoa kwa kutompenda? Unaona Mimi nilivyochaguliwa mke na Baba! Sikumlizia kabisa awe wangu lakini kadili nilivyozidi kuishi nae tayari nishampenda sana sana tu, hata wewe utampenda,, nataka nimuone kwanza shemeji yangu nijue anafeli wapi?”
Ā Ā Ā “” Kakaa! Hivi si unakumbuka ujumbe niliowahi kukutumia nahisi Minnie sio mtu mzuri kwangu, kingine anaonekana anatabia za ubandit na hapa white house ni kama kaolewa na Mimi kutafuta kitu fulani.”
Ā Ā Ā “” Acha zako ni kwakuwa humpendi ndio maana unamchukulia tofauti.”
Ā Ā Ā “” Nielewe basi Alex.”
Ā Ā Ā “” Naweza kuelewa hilo lakini sio wewe kumuoa Maina, na ole wako nisikie.”
Huku chumba Cha pili kulisikika harufu nzuri ya perfume ikishamili chumba hicho, Katika kunako kioo midomo milaini iliyojazwa rangi ya lipstick ya piki ilinona huku kope ndefu pamoja na nyusi nyingi zilionekana katika sura ya mwanadada aitwae Sandra, Alimaliza kujipodoa huku akichukua simu yake iphone macho matatu alibofya kwa kucha zake bandia ndefu za wastani Kisha aliweka sikioni akiongea.
Ā Ā Ā “” Ooh wifi yangu mzuri, umesema nafasi uliyokuwa ukiwaniwa imechukuliwa na Binti mpori-pori!? Nikuombe kitu kimoja katika sherehe najua hautakuwa na sehemu ya kuegamia hebu njoo ukae karibu yangu naimani kaka’ngu lazima ang’ake kwako.”
Mazungumzo haya yaliishia hapo huku Sandra mwanamke mwenye umbo la wastani alisimama huku akipindua kiuno chake kushoto na kulia na hii ilikuwa ni kutizama mkao wa nguo yake kwa nyuma unavyoonekana. Baada ya kujihakikia alitoka na hio motion yake viatu pekee viliitikia mtembeo wake huku kiuno chake chembamba misri ya nyigu kilipata shida kulazimika kufanya mazoezi ilihali haikuwa wakati wake.
“” Ooh Sandra queen, umependeza sana! Halafu umekuwa mrembo zaidi hakika ulaya sio uhayani.
Dada mrembo aitwae Getu alimsifia Sandra mara tu baada ya kumuona na huyu alikuwa ni rafiki yake kipenzi kabisa.
“” Ahsante msweet wangu, Nilijua utaniangusha Leo, lakini Aneth atakuwa wapi au Ndoa tamu mwezetu?”
Sandra aliongea huku macho yake yakiangaza kumtizama huyo mke wa Kaka’ke ambae kampindua wifi yake Maina ambae alimtaraji ataolewa nae hivi punde. Kwani alikuwa na kitu gani cha kumzidi Maina wake?
Minnie muda huo baada ya kuona watu wapo busy alichomoka na kwenda bustanini bilashaka Kuna kitu alitaka kuongea na Mlinzi wa siku Ile.
Alifika bustanini anashangaa kunako bustani siku Ile aliona Kuna Kaburi kama tatu, Moja ya Kaburi aliona kunae kijana alivalia mkoti wa Dark blue kapiga magoti kwenye Moja ya Kaburi akifanya Sala, akawa hamuelewi vile anatizama vizuri ndio anagundua ndie Mme wa Mama Mirii, inamaana shemeji yake, yaani Alex, akawa anamshangaa kwenye lile Kaburi alielala pale atakuwa na uhusiano gani na yeye..?”Ā
Kuna mkono wa kiume ulimshika na kumvutia katika mti mpana na kufanya umzuie kutizama mbele tenaa, Minnie akashituka kwa woga huku akiinua uso wake akimtizama mtu yule usoni ndipo anatahamaki baada ya kugundua ni Mlinzi.
Ā Ā Ā “” Umeijia Nini tena huku? Eti Mrs Alexander Kuna kitu wakagua kwenye hii bustani? Siku Ile nilikuonya usije huku na Leo tenaa, hapana Leo nitakushitaki kwa Bwana Alexander bilashaka utanifukuzisha kazi kama nitalikalia kimya jambo hili.”
Ā Ā Ā “” A a a , Mi Mimi.. ham na! Nilikuwa nimemfata huyo kaka anahitajika huko.
Minnie akapata wazo la kusingizia mapema, Mlinzi akawa kamuamini.
Ā Ā Ā “” Ooh hapo sawa nikajua na Leo umekuja kufukunyua jambo tenaa? Make unaonekana kwenye nyumba hii ni kama Kuna kitu ulifuata.””
Minnie akajichekesha kwa roho Mbaya ashajua huyu Mlinzi ashaanza kumtililia shaka tena.
Ā Ā Ā “” Kwahiyo alikuja kumuombea marehemu?” Akawahi kujiulizisha.
Ā Ā Ā “” Huwa ni kawaida yake, mara tu baada ya kutua White House huja kuomba Dua kwenye mwili wa Mama’ke ulipolazwa, yaani alimpenda sana Mama’ke.”
Ā Ā Ā “” Ooh Mama’ke ndo huyu Mama’ke na Alexander aliyelala pale…!!?”
Ā Ā Ā “” Ee ni Mama’ke japo wao walichangia Baba, huyo ndo Mama’ke wa pekee.”
Minnie akawa ameduwaa kidogo lakini moyoni akahisi ushindi ni kama Kuna kitu kaongeza kwa siku hiyo akawa kagundua kumbe Alexander na Alex wao walishea Baba akatoka kwa furaha akiruka Mlinzi akawa hamuelewi akawahi kumsimamisha.
Ā Ā Ā “” Vipi mbona unamuacha mwenzako. Msubili anakuita.”
Minnie akaona sio mbaya hata hivyo alisikia kuitwa kitendo Cha kumgojea na kuambatana nae sio mbaya.
Ā Ā Ā “” Aaa Bwana Alex! Binti huyu alikufuata wewe nilishidwa kumzuia.”
Mlinzi akaongea mara baada ya Alex kumfikia.
Ā Ā Ā “” Haina shida ni shemeji yangu hata hivyo nilifaa nimuone karibu, imekuwa vyema sana yeye kunifuata.”
Alex akawa amepiga hatua kwenda mbele akawa amemfika Minnie ambae alikuwa akifuta tope kiatu chake katika Bomba lililotiririsha maji kuelekea bombani, Mara nyingi maji yake yalitumika kunyunyuzia bustani.
Ā Ā Ā “” Mhuu Shem lake…!!”
Ā Alex alimuita kwa furaha kweli ni alimaanisha kabisa.
Minnie ndio akamalizia kuvaa viatu vyake huku akiinua uso kumtizama Alex, ndipo wote wakamtizama kwa pamoja Ile kuonana tu kila mtu akasituka huku akitizama pembeni kwanza kwa wakati mmoja huku akivuta taswira ni kama waliwahi kuonana.
Ā Ā Ā “” Aaa wewee,, Ni kama niliwahi kukuona sehemu…!!!!!!”
Wakazungumza kwa pamoja huku wakizidi kukaguana.
Lakini Alex akafanya Kucheka tu huku Minnie bado anavuta taswira ni wapi alimuona.
“” Aaa hapana sio yeye huenda nilichanganya tu.”
“” Shem,,, Alex akamuita huku akimshika begani…
“” No ni utani tu Nilitania huenda nakufananisha tu, basi tuondoke.”
Ikabidi waongozane kwa pamoja japo Kila mtu alikuwa anafikilia sura ya mwenzake ni wapi aliiona.
“” Vipi lakini Shem! Naona unamtunza kaka’ngu vizuri anazidi kushamili tu.”
Alex akaongea huku wakipiga hatua wakizidi kuongea.
Ā Ā Ā “” Aaa yaani bora huyo Alex angekuwa kama wewe! Yaani mkalimkali tu.”
Ā Ā Ā “” Mhuu Minnie, Alex tenaa.. !? Huyo anaitwa Alexander ukisema Alex umenizungumzia Mimi.”
Minnie ikabidi acheke tu, maneno ya Alex yalimkumbusha mbali sana anakumbuka Alexander aliwahi kumwambia kuwa yeye sio Alex ila ni Alexander na kama atamzungumzia Alex atakuwa kazungumzia mtu mwingine.
Ā Ā Ā “” Ooh!! Mimi ni mjinga kumbe hakika wakati ule nilipotaja Alex kumbe nilikuzungumzia wewe! Anisamehe tu.”
Alex yeye akabaki kutabasamu tu Kisha alimuuliza.
Ā Ā Ā “” Inamaana ndugu yangu ulimuita Alex..!?”
Ā Ā Ā “” Ndio Mimi nikajua ni jina lile lile, Sema alinikazia sana! Naona angalau sahii naanza kuzoea kumuita Alexander.””
“” Ututofautishe bhana! Kama utamuita yeye Alex na Mimi nikiwa karibu yake basi nitaitika Mimi na sio Alexander.”
Kwa ujumla wote walibaki Kucheka kwa furaha kwa utani wao uliojenga ukaribu mzuri kwa sekunde chache walijikuta kuzoeana sana.
Huku kwenye sherehe alipo Alexander anamuangaza Minnie Kila Kona anajua tayari kaenda kufanya ubandit. Hakusita kumfikia Shemeji yake kumuulizia.
Ā Ā Ā “” Shem! Umemuona Minnie hapa..!?”
Ā Ā Ā “” Aaa sijamuona, lakini Mimi pia namtafuta Alex.”
Ā Ā Ā “” Bora Alex atakuwa kwenye ibaada zake lakini huyu Bandit sijui kaenda kuspy Nini huko aliko.””
Sandra muda huo alikuwa na Maina na wao walimtafuta Minnie, muda huo Alexander akawafikia.
Ā Ā Ā “” Vipi! Mbona mnatoa macho Kuna kitu mwatafuta? Eti Minnie mmemuona?”
Alexander akauliza huku akimtupia Maina jicho.
“” Ooh unaniangalia Nini..!? Kwamba nimemteka huyo mpori-pori wako?”
Alexander akamkata jicho huku akipandisha juu lakini alisikika akiitwa na Alex.
“” Ooh Nini tena Alexander najua unanitafuta? Nipo na Malkia wako hapa yaani ni charming girl.”
Minnie yeye akamtizama tu Alexander atasema Nini lakini alitabasamu tu huku akishuka na kwenda upande wa Minnie akafanya kumshika mkono huku akimbinya kwa nguvu, Minnie ikabidi ajikaze tu.
Mama Miricka nae akawa amefika kwa Mmewe akashika mkono huku akimtizama usoni na kuongea.
Ā Ā Ā “” Ulinitia hofu sana! Wakati mwingine jaribu kuniondolea hofu Mimi mkeo bhana.”
Alex alitabasamu tu huku akimshika nywele mkewe aliziweka sawa.
Ā Ā Ā “” Nikiwa hapa siwezi nikakuacha kamwe! Nilienda kumsalimia mama mara moja.””
Wote ilibidi wagawane wawili wawili, Alexander akawa amepata muda wa kuongea na Minnie.
Ā Ā Ā “” Mikono yako inaloa jasho, bilashaka ulienda kufanya madhambi yako tenaa! Eti Leo tenaa ulienda bustanini?”
Minnie akahisi presha akitaka kuutoa mkono wake lakini Alexander akamzuia.
Ā Ā Ā “” Mhuu wazani sahii nitakupa nafasi ya wewe kukaa mbali na Mimi? Leo itabidi tuambatane tu.””
Ā Ā Ā “” Aaa lakini unaniumiza!! Mikono yako migumu.”
Alexander ikabidi acheke tu kwamba yeye ana mikono migumu au alitaka kuachiwa tu..?Ā
Ā Muda huo Sandra akawa amefika mbele Yao.
Ā Ā Ā “” Ooh! Namuona wifi Mrembo kweli, kumbuka kaka hukunitambulisha! Basi nakupa faini,, niache niongozane nae angalau tuzungumze nae.”
Alexander akamtizama Minnie kwanza akaona sio mbaya kumkabidhisha kwa Dada’ke hata hivyo anamjua vizuri Sandra vile angemganda.”
Ā Ā Ā “” Kaka jamaniii hutakii…!! Niachie wifi yangu jamaniii.”
Ā Ā Ā “” Sawa,, hakikisha unamtizama muda wote asikupoteee! Usinifanye nimtafute tenaa..”
Ā Ā Ā “” Kaka jamanii Najua unampenda sana! Basi namtizama.”
Minnie muda huo yeye macho yake makavu yametua kwa Alexander aliyaelewa vizuri maneno yale ilikuwa ni onyo kwake kwa mtu mwingine ilikuwa ni ngumu kumuelewa. Alexander alivyojua kumhadaa hakusita kumpiga busu kwenye paji la uso eti alifanya kumuaga.
Minnie ikabidi ajivute mdogo mdogo akitamani kulifuta busu lile, lakini haikuwa na maana kwamba litaacha Alama moyoni alimfuata Sandra mpaka alipoenda kusimama, baada ya kufika tu Maina akawa amefika pale na kuanza kutoa maneno yake ya karaha.
Ā Ā Ā “” Ooh! Mrs Alexander naona Leo umependeza sana kwa vazi zuri la heshima, najua haikuwa ndoto yako kuvaa gauni hili ila ni White House pekee ndipo ungelipata, Vipi lakini Ndoa yako Inae furaha najua siku zote kuiba moyo wa mtu uhamishike kwako ni ngumu ndomaana hata mmeo ameshidwa kukupatia Haki yako ya Ndoa kama ulivyofikilia, si kweli..?””
Maina aliweka kituo huku akimtizama usoni vile kachachafyika kwa maneno yake, Minnie alihisi ni kama wanamnyima pumnzi tu yeye alitaka kufikilia mambo yake na sio maneno ya mwanamke huyo, kingine aligundua kabisa huyo wifi yake alimchukua pale makusudi akatambua ni wale wale akaona awapishe.
“” Aaa wifi wapi tenaaa..? Achana na Maina maneno mengi, kaka amesemaa nisikufanye akutafute tenaa.”
Minnie ikabidi arudi na kusimama pembeni yake, kwa mbali kabisa alimuona Brighton akawaza ni wakati sahihi ya yeye kuwa kule, akatoka kimya kimya huku wamejisahau wakipiga picha.
Ā Ā Ā “” Ooh shemela umependeza sana, umekuwa kama Malkia kwenye utawala wa kifalme.”
Bright akachombeza baada ya kumuona.
Ā Ā Ā “” Basi wewe ndio Mfalme wangu. Karibu kwenye himaya yangu.”
Minnie akazidi kuonesha furaha kwa shemeji yake, Bright akawa kamchukua huku wakipiga hatua.
Ā Ā Ā “” Leo twende ukamuone Dadako najua hujawahi muona hata mkapiga stori nae. Nifuate.”
Muda huo Alexander kwa mbali ndio anamuona Minnie akiwa na Bright ikabidi amtizame kwanza Dada’ke aliempatia kazi ndipo anamuona yupo busy na Rafiki zake wakipiga picha akabaki kulalama kimya kimya.
Ā Ā Ā “” Hamna kazi niliyoifanya hapa, Mimi pekee ndio nafaa kuwa karibu nae! Na hapo hatochelewa kuwatoroka.”Ā
Nini Kitaendelea?Ā Usikose SEHEMU YA KUMI NA MBILI YA KISASI CHANGU
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMĀ Ā
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAĀ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAĀ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIĀ
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoĀ kijiweni.co.tzĀ unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiĀ editor@kijiweni.co.tzĀ Ā Ā
KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU
8 Comments
Mwandishi me nikajua utafidia utatuma mbili kumbe moja tuu na ya Jana iko wapi?
We acha tu hata mimi nilijua zitakuwa mbili kumbe ni moja na alivyosema ni ndefu kumbe ya kawaida tu
Duuuuuh admin …matukio yanachanganyaaa
Story inazidi kunogaš
Well done
Habari boss, samahani
naitwa Enliq nipo dar nina project lakini nimechungua kupata mawasiliano na wewe sijaona ndo maana nacomment hapa. naomba nicheki whatsapp number 0678250925.
nina project ya site na kuna mfumo wa forum nimeupenda na nataka kama inawezekana unisaidie kuset kwa gharama yoyote
Aaaise ni tamu naona minnie alivojasiri jamani kuna vitu ananifundisha
Ni nzuri sana jamam unachelewa