Ilipoishia “Minnie hakujua kama Siri yake imevuja baada ya kumkosa Kaka’ke ilibidi alale tu hana mtu wa kuongea nae sahii.
Huku kwa Alexander baada kupata ujumbe alimwambia shemeji yake asiwambie familia ila wao watawafanyia suprise ila mpaka wazungumze kwanza.
“” Sasa nataka nicheze na akili za Minnie kama hataniambia anaona basi nitamfanyia vitimbwi vya ajabu mpaka akili mwenyewe anaona! Huwa namjua Bandit wangu anakuwaga na akili nyingi na ukute ni siku nyingi anaona ila kaniigizia tu, au na muda ule kitandani ashituke huenda alikuwa akiniona ee..!!? Ngoja nipite hospitali kwanza Daktari atanipa majibu.
EndeleaĀ
SEHEMU YA KUMI NA NANE
Abdul akafanya kumshika mkono akiurudisha chini.
“” Ooh mke wako..? Kwa Mme yupi labda..? Mwanaume huwezi mhandle mkeo mpaka anapata ajali, ulikuwa wapi mpaka anaumia namna hii? Tenaaa akipatwa matatizo utawajibika.”
Alexander akabaki kumtizama tu jinsi alivyomshika mkono akafanya kuutoa huku akimtizama usoni.
“” Wewe unanizuia kumlisha mkewangu kama nani..? Sawa alikuwa mpenzi wako lakini kwangu ni mke na kingine Naomba tuliza mihemko yako upo kwangu.”
Abdul alishidwa kujizuia alijikuta akimvaa Alexander wakiendelea kuvutana wakionesha umwamba wao.
“” Sawa umemuoa lakini Minnie hakupendi wewe na hana Mapenzi na wewe, na hii Ndoa basi tu muda si mrefu atarudi kwangu.”
“” Mhuu arudi kwako kwa vigezo vipi…? Minnie ni mkewangu na atabakia kuwa mkewangu siku zote za maisha yangu, haijalishi yeye ni Spy lakini ndio nishampenda hivyo.”
Minnie alikuwa akiwasikiliza tu mwisho alichoshwa na kelele zao akasukuma stuli iliyokuwa na chakula baadhi ya bakuri zikavunjika ndipo wakaachana.
“” Inatoshaaa!! Mnanipigia kelele tu mpaka kichwa kinauma Kwanini mnakuwa hivyo lakini..?”
Ikabidi wote watulie wakirejea kwenye kitanda alichokuwa kakaa Minnie Kila mtu akabaki kushika kichwa na kuinamisha kichwa chini wakifiklia vitu vingi kichwani.
Upande wa Mzee Mzobe alikuwa akiongea na White House.
“” Ooh Kamanda Mzobe! Najua Bado unakisasi na Mimi! Huenda kila kinachotokea hapa unahisi kuumia kwa Minnie ni mojawapo ya ugomvi wetu lakini sivyo.”
White House aliongea .
“” Ni vile hukuwafunza watoto wako kwaajili ya kijana wako mwanangu Leo haoni tenaa, kumbuka ulinifuata mwenyewe ukiomba kijana wako amuoe binti yako kwa makubaliano ya kibiashara! Sasa biashara gani hiyo inavuka mipaka mwanangu sikukupa adhurike kwa tabia mbaya za kijana wako.”
Mzee Mzobe akaongea kwa hasira huku akizidi kukagua chumba Cha White House.
“” Vijana wetu huwa wanakosea hata ukiwaelekeza hufanya kinyume na matakwa yetu, nitamuonya kijana wangu kuhusu tabia hiyo nitamrekebisha.””
“” Utamrekebisha wapi wakati Binti yangu kaumia,,haoni sahiii.”
Mzee Mzobe alizidi kuonesha maumivu yake hata hivyo alikuwa na hasira nae tu ilionesha kabisa ugomvi wa miaka ishirini haukuisha.
Upande mwingine alionekana ni Brighton akiwa barabarani akielekea kwao Maina. Alifika getini akapiga honi kwa nguvu Mlinzi akawa amefungua geti. Brighton alipaki gari yake kwenye parking ya nyumba Ile Kisha alishuka akielekea kwenye lango kuu akizidi kumuita Maina kwa sauti…. “” Mainaaa!!! Mainaaaah!!!”
Maina ndio akatoka akiwa na wasiwasi anashangaa kumuona Brighton yupo pale.
“” Aaa Shem mbona kelele hivyo nyumbani kwetu, kunashida labda…!?”
Bright alifanya kumshika mkono akimvuta kuelekea kwenye gari lake akiongea nae.
“”” Unauliza shida iliyotokea inamaana umesahau? ” Leo utaenda kujibu kituoni.””
Ghafla akasikia sauti iliyomfanya atulie kwanza huku akimtizama Maina ambae hapigi hatua tenaa.
“” Hapaswi kwenda sehemu yoyote huyo…!?”
Ikabidi ageuke kutizama aliemsimamisha hakuwa mwingine zaidi ya Baba’ke na Maina yaani Mzee Saud( Sudi) alifanya kumsogelea kwanza azungumze nae.
“” Baba unajua lakini mwanao kakosea Leo? Upofu wake wa Mapenzi leo Binti wa watu anatumia mti kuongoza njia assumed ndio Binti yako kafanywa hivyo ungefanyaje?. lazima aadhibiwe huyu.””
Maina akafanya kujitoa kwa Brighton akisogea pembeni na Baba’ke akimshika mkono asikie anavyomtetea ashaona dalili za kwenda getezani umewadia.
“” Sawa najua kosa alilolifanya Binti yangu,,, lakini tushalimaliza Maada hiyo kitambo, Minnie atatibiwa mpaka atakapokuwa sawa.”
“” Kilaini namna hiyo? Na vipi kuhusu tabia yake yakung’ang’aniza mahusiano ya Mme wa mtu anapaswa aendelee..!?”
Mzee Sudi akamgeukia Binti yake alimuomba aingie ndani kwanza Ili wazungumze kiume wakamilishe swala hili.
“” Brighton najua unavyojisikia lakini Mdogo wako mwenyewe alikuja kumchumbia Maina, kinachoendelea hapa ni vile Maina aliaminishwa, nikuombe kitu nenda kaongee na Alexander azungumze na Maina wayaweke sawa Ili kuepusha kelele zisizo na msingi, kwa tukio alilolifanya hata Mimi limenipunguzia nyazifa kwenye kazi zangu ndiomaana nimemfungia ndani asitoke humu, vinginevyo ni aibu tu.””
Brighton hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuondoka japo hasira yake kwa Maina haikuisha akaamua akaimalizie kwa Alexander.
Muda huo Mzee Mzobe ndio anamaliza kuongea na White House kilichoendelea ndani ilikuwa ni tafurani mtupu kwani Mzee Mzobe hakumpa muda wa kumsikiliza White House zaidi ya tuhuma tu, ilibidi amchukue Abdul waondoke japo wote Kila mtu aliondoka kwa malalamiko si kwa Mzee Mzobe Wala kwa Abdul.
Muda huo Brighton akawa amepishana na Mzee Mzobe pamoja na Abdul hakuwa na hiyana kuwaaga. Alinyoka Moja kwa Moja chumbani kwa Alexander alimkuta akimalizia kukusanya puje za bakuli zilizoanguka kwa kuziokota, Minnie muda huo alikuwa kakaa kitandani katulia tu hana kazi ya kufanya.. ama kweli kwa wakati huu asingeweza kufanya kitu chochote kwa hari ambayo hakuizoea katika maisha yake alijihisi ni mpweke kweli.
Brighton akawa amefika akiwa na hasira alifika akamfurumsha Alexander akimsukuma kwa nguvu akawa ameangukia vile vipande vya bakuli vikamuumiza mkononi akabaki kulalamika kwa maumivu makali. Minnie alibaki kusikilizia tu hata hivyo kelele za vijana wa hii nyumba vilimchosha.
“” Unaona ujinga uliofanya lakini? Muda wote wamng’ang’ania Maina Bado Baba’ke mwenyewe anamkingia kifua kumbe ulimchumbia Maina? Basi kamuoe Sasa umlete ndani.. na kuhusu Minnie mrudishe kwao. Haya karatasi ya taraka hii hapa usaini Kisha mpatie na Minnie angalau awe huru tu.””
Alexander ndio akasimama akitizama Ile karatasi aihakiki kweli ni karatasi ya taraka alifanya kuisoma kwanza baada ya hapo aliichana-chana vipande.
“” Nimechosha na nyumba hii! Kila siku mnaniandama mnaona Mimi ndie mkosefu sana! Kwani wewe hukuwahi kukosea mbona ulimcheat mkeo ukatembea na mama Miricka si ulisamehewa..? Iweje kwangu mnanituhumu namna hiyo nitabadilika na nitalekebisha Kila kitu kitakaa sawa Mimi na familia yangu.””
Minnie kazi aliyokuwa nayo ni kusikiliza tu japo habari ya Brighton kutembea na mke wa Alex ilimshangaza sana anashidwa kuwaelewa vizuri vijana wa white house wanatabia Gani?
“” Nakwambia badilisha mambo yako unaleta habari za miaka mingi kupita! Nitasimamia Haki ya Minnie kwahizo tabia zako mbovu sitataka zijirudie tena kwenye nyumba hii, halafu kumbuka unaongea na Kaka’ko.”
Minnie akahisi kuchoka mpaka masikio aliyasikia yakipiga kelele ni kama Kuna kipenga kilipulizwa.
“” Naombeni mniache mwenyewe enyi watoto wa white house, kelele kelelee hivi hamuwazi kama mnamgonjwa..?”
Brighton akaishia kumtizama Alexander kwa hasira Kisha aliondoka. Ilibidi Alexander amalizie kufanya usafi wake baada ya kumaliza alichukua dawa akapakaa kwenye mikono yake make aliumia kwa vipande vya bakuli alibaki kujitibia huku Minnie kalala ni kama anatumia taswira ya picha baada ya kusikia harufu ya dawa akajua Alexander ndio anaitumia.
Alexander baada ya kumaliza kupakaa dawa alijitupia kitandani huku akilala Chali, Minnie akawa kajishitukia akasogea pembeni.
“” Tulia bhana! Unajua sahii naweza kufanya kitu chochote kwako! Au nikwambie hapo ulipo nguo yako imefunuka.”
Minnie akawahi kujifunika akifikili anavua, Alexander akacheka tu huku akimtizama usoni.
“” Wewe hapo… upo vizuri! Lakini Kuna kitu nahitaji kwako,,, ni msamaha tu.”
“” Msamaha gani si unampenda Maina! Wewe tengeneza mazingira mazuri umuoe huyo mwanamke kabla hajaniua.”
“” Ahaa! Eti akuue..? Na vipi nikisema nampenda mkewangu wa Ndoa…!?”’
“” Una mje kumbe …!?”
Alexander ikabidi acheke huku akijiongelesha mwenyewe.
“” Eti Minnie…,,, ndo nimekosa namna hii hadi wanizonge familia nzima? Aaa!! Nahisi kuchoka tu! Lakini Maada yetu inaendelea nipo nafatilia kuhusu Ile picha lakini bado sijapata majibu kwani wewe unafikiliaje kuhusu Ile picha? ”
“” Nawaza macho yangu kwanza! Sasa mission sioni,,, nitaikamilisha nikiwa hivi? nisaidie basi angalau nione kwanza ndipo nitakamilisha ratiba zangu halafu nataka majibu ya kazi yangu niliyokupatia, kama utachelewa kunipatia majibu utaniona kikwazo mbele yako kila mara.”
………. Itaendelea…………
USIKOSE SEHEMU YA 26.
Usomapo simulizi hii hakikisha hausambazi sehemu yoyote pasina ridhaa ya Mwandishi.
[17:50, 6/4/2024] Tinner: SIMULIZI: MINNIE KISASI CHANGU.ļø MTUNZI: TINNER ROBER. SEHEMU: Ā¶ 26Ā¶ 0746638941 Whtsp.
TULIPOISHIA……………..
Alexander ikabidi acheke huku akijiongelesha mwenyewe.
“” Eti Minnie…,,, ndo nimekosa namna hii hadi wanizonge familia nzima? Aaa!! Nahisi kuchoka tu! Lakini Maada yetu inaendelea nipo nafatilia kuhusu Ile picha lakini bado sijapata majibu kwani wewe unafikiliaje kuhusu Ile picha? ”
“” Nawaza macho yangu kwanza! Sasa mission sioni,,, nitaikamilisha nikiwa hivi? nisaidie basi angalau nione kwanza ndipo nitakamilisha ratiba zangu halafu nataka majibu ya kazi yangu niliyokupatia, kama utachelewa kunipatia majibu utaniona kikwazo mbele yako kila mara.”
ENDELEA……………………..
“” Ooh bandit girl! Mimi natamani kazi ulioianzisha uiache. Naona kabisa utahatarisha maisha yako na ya wengine pia.”
“” Sikutaka ushauri kwako, niitie Mama Miricka kwanza nataka nibadilishe nguo.”
“” Lakini Mimi Si mmeo..?”
“” Sizini na Mme wa mtu! Please niitie Mama Miricka.”
Alexander ikabidi amsikilize na kwenda kumuita mama Miricka.
Huku nje alionekana Alex kakaa huku akikagua picha za Nickson alizopost katika kurasa yake, aliona yupo na Minnie hapo ndio akaamini kweli wale ni ndugu akaona bora kumpigia simu, akawa kapokea.
“” Ee Kamanda Nick salama! Samahani kidogo ushajua Minnie alipo?”
Nickson akashituka kwanza anakumbuka Minnie alimwambia yupo sehemu salama pamoja na Baba’ke, na siku za nyuma alimwambia kuhusu Alex kama anamfahamu lakini akakatisha Ile Maada ya yeye hakupata muda wa kufatilia tena kutokana na majukumu yake ya kazi, akawa haelewi zaidi ikabidi amjibu.
“” Sijajua ni wapi walipo ila niliwasiliana nao wapo salama kwa kifupi nishawapata.”
“” Ooh! Unajua Nini…,, mdogo wako wewe anaishi kwetu na kingine mdogo wako kaolewa na mdogo wangu yaani ni mwanafamilia katika Denishoo au White House.”
Nickson akahisi kama pumnzi zinakata mahali alipokuwa amekaa ikabidi asimame kwanza yaani haamini.
“” Mh muu.. una ..Sema wewe hapo wakaa na Minnie…!?”
“” Ndio huamini.. !? Ambavyo huamini hata Mimi siamini na sielewi, labda ngoja nimpelekee simu japo utashituka kidogo make aliumia kidogo macho yake,, nakupigia video call muda si mrefu.””
Alex akapandisha mpaka kwenye chumba Cha Minnie Kisha akapiga simu video call huku akigonga mlango, muda huo Mama Miricka alikuwa akimsaidia Minnie kuvaa baada ya kumaliza ndio akaenda kufungua Mlango.
“” Aaa Baba Miriii karibu umekuja kumuona shemeji yako.”
Huku kwa Nickson alikuwa akitizama vizuri mazingira ya mle ndani baadae ndio anaonesha sura ya Minnie yaani hakuamini na sio kuamini tu alisikia akiambiwa Alex kaja kumuona shemeji yake inamaana Minnie ndie shemeji yake piwa.
“” Minnie ongea na Kaka’ko anataka kukusalimia, hii ni video call pia.”
Minnie akashituka akijisogeza vizuri kwenye sofa ni kama alihisi sofa ni ndogo kabanana,, ndipo akasikia sauti ya Nickison.
“” Miniii… Kwanini lakini Mdogo wangu unakuwa hivyo!! Yaani wewe hapo umeolewa na mdogo wake na Alex kwanini lakini unakuwa hivyo Minnie,,, hakika leo siku yangu imekuwa mbaya,, kwanini eti Minnie why’s? ”
Minnie alishidwa ajibu Nini zaidi ya kubabaika tu, Alex ikabidi amgeukie vizuri.
“” Minnie mwambie Kaka’ko wewe na Baba’ko mnanjama na familia yetu haiwezi kuwa salama yaani wewe utoke Mbeya uje Zanzibar halafu kwetu,, ilikuwaje mkafika hapa? Mbona sielewi lakini? Basi mwambie Kaka’ko unajua vile alikuwa akiwatafuta lakini?”
“” Mhu Kaka,,, nitakwambia,, nitafute private tutazungumza lakini I’m sorry kaka! Kila kitu kitakuwa sawa.”
“” Miniii sawa wapi? Mbona mnaniumiza hivyo! Kweli Leo mmenivunja moyo wewe pamoja na Baba na kwa hari hii mlivyofanya kunitenga Mimi sitawahesabu kama ni ndugu zangu nyie fanyeni maisha yenu tu! Au Bado mna kisasi tu angalia Sasa hivi macho yako wewe yamekuwa na shida nahisi yote ni kwasababu hukuwahi kumuelewa Kaka’ko anataka Nini na hivi mnavyoendesha maisha yenu Kuna siku nitakuwa kinyume na matakwa yenu,, na sitatoa msaada kwenu.”
“” Kakaaaa! Unaongea Nini lakini..? Mbona unakuwa hivyo why unanitenga yaani unaniepuka Mimi ndugu yako….!? Usimseme Baba vibaya yupo halari.
“” Nishakata huo undugu! Najua kisasi Cha damu ambavyo hulipwa kwa damu na vipi kuhusu maisha yenu nyie yatakuwa salama kweli? Naomba tuishie hapo.. sitataka mnishirikishe kitu chochote kuhusu nyie Mimi na nyie ndio bye bye.””
Muda huo Alexander nae alikuwa akisikiliza kasimama mlangoni muda mrefu baada ya simu kukatwa ndio akaingia.
Muda huo Minnie alilia kilio Cha kufa mtu ilikuwa ni ngumu kuamini maneno ya Kaka’ke kuwa kwasasa yeye hawahesabu kama wanafamilia alilia mpaka akashuka chini, Alexander ikabidi amuwahi alifanya kumuinua na kumkalisha tenaa, alimtizama Kaka’ke aliesababisha yote hakuvutiwa sana na jambo lile, Alex ikabidi awaache akiwa na maswali mengi Bado anauliza kwanini Minnie yupo pale?.
Alexander akafanya kumvutia kifuani akizidi kumtuliza lakini anashidwa asimamie upande upi ni amkumbatie Minnie kwa kumuonea huruma au aungane na Kaka’ke yaani Bwana shemeji kumuonya Minnie aache kisasi wakati anajua kabisa kaja kwenye nyumba yake kwa akili ya kisasi? Hakuwa na budi kumtuliza akae sawa mambo mengine yangefuata.
Huku kwa White house alionekana kushikilia picha ya Minnie pamoja na picha ya Alex akiitizama sana baadae alizungumza ni kama anaiuliza Ile picha.
“” Je, Ni haki hawa ndugu kufahamiana kuwa ni kaka na Dada au Siri hii iendelee kufichwa..!?”
Ghafla akasikia sauti nyuma yake alikuwa ni Mr Gelu.
“” Sio sasa mkuu.. !!!
Ikabidi amgeukie huku akichukua picha akizirudishia kwenye Album.
“” Kwanini sio Sasa…? Minnie na Alex ni watoto wa Mama mmoja, nimejitahidi kuficha Siri hii lakini naona siwatendei Haki! Mama’ke na Minnie nilibahatika kuzaa nae mtoto mmoja japo Mzee Mzobe alijua yule mtoto alipoteza maisha lakini anaishi na kwasasa Kawa mkubwa, na kingine katika eneo lake la kazianalofanyia…. anafanya kazi na ndugu yake yaani Nickson sema hawafahamiani tu, huoni nawatenga hawa ndugu?”
“” Ni sawa lakini….. Kama Minnie kaolewa na Alexander inamaanisha ni ndugu yake na wewe unaamini kuwa Minnie yupo kwaajili ya kisasi na kumuoza hapa ilikuwa ni kufatilia nyenendo zake pamoja na Baba’ke, hapa nawaza je wakipendana itakuwaje? Hawa ni ndugu.”
White house akacheka kwanza huku akijitizama kwenye kioo.
“” Ahahaa! Yaani wapendane juu ya kisasi ni ngumu nitatengeneza mazingira ya wao kuwa mbali hawawezi kuwa kitu kimoja,, kwanza ndio kazi inaanza hapa ukisikia tap Game ndio hapa! Kamanda Mzobe lazima aadhibiwe yeye ndio alisababisha kumkosa mkewangu kipenzi,, nilimpenda sana yule mwanamke lazima alipe.””
Muda huo Mlango ukafunguliwa ilikuwa ni sura ngeni kuonekana kwenye hii familia ya White House,, Alionekana ni Baba mmoja kapanda hewani huku mwili wake ukiwa umejazia kwa mazoezi alivalia koti kubwa na chini alivalia jinsi aliingia kwa mbwebwe akafanya kutundika koti lake kwenye kiti Kisha alikohoa huku akichukua bastola iliyokuwa katika koti lake akifanya kuitengeneza huku akijaribu kuikoki ni kama alikuwa akilenga shabaha kwa mtu.
“” Ohuuu!! Miaka mitano ya nyuma si kama miaka mitano ya mbele.”
Aliongea semi hiyo huku White house na Mr Gelu walimtizama Kisha wakacheka kwa sauti wakimsogelea na kumkumbatia.
“” Oooh kaka Denis! Afadhari umekubali kurudi tukamilishe mission hii kwa pamoja! Nilifikilia utachelewa kufika kumbe upo chap kama mshale.. Ahahaaaaa!”
White House akazidi kucheka lakini kaka alietambulishwa kama Denis alimsukuma kidogo akirudi nyuma.
“”” Aaa!! Sio hivyo Kaka’ngu hapa naenda kufanya kazi ngumu, ya kuua kiumbe Cha Mungu sio kawaida… Weka mpunga mezani kwanza.””
White House akashangaa inamaana Kaka’ke alitaka pesa kweli? Tangu lini Kawa mtu wa kufanya mission na kuomba pesa,,, Hapo hapo kicheko Cha Denis kikarejea tena alimcheka White House kisha akamkumbatia tenaaa.
“” Aaa mdogo wangu! Sio rahisi Mimi kuwa hivyo najua umeshangaa hebu weka mkeka mezani tuuchambue kwanza.”
Ikabidi wavute kiti na kukaa mezani Kisha White House alipiga simu kwa Dada wa chakula angalau waletewe vinywaji Ili wajadili vizuri.
Upande wa Kamanda Mzobe nae alikuwa kakutana na Mwanasheria wake wakiwa wamepata ushahidi wa kumfunga Bwana Denishoo, waliendelea kujadili.
“”” Kesi inatakiwa tuipeleke mahakamani! Kama Denishoo ataitishwa mahakamani Kuna ushahidi lazima upatikane katika maelezo yake! Kama hakumuua yeye basi ni miongoni mwa wanafamilia wake ndio wanahusika, ataenda kujieleza hata hivyo katika maongezi yake lazima atajichanganya tu.””
Ni siku tatu zilipita Alexander aliambatana na Minnie wakielekea hospitalini kama Daktari alivyowataka wafike baada ya siku tatu kwa uchunguzi zaidi.
Daktari ilibidi aingie kwenye chumba Cha Minnie alifanya kumfungua kitambaa Kisha alimwambia afungue macho taratibu kama anaona.
Alexander nae ikabidi aingie ndani amtizame vizuri mgonjwa wake ndipo alimuona Minnie kafungua macho japo macho yake yalikuwa hafifu sana.
“” Mhu Minnie unaniona..? Alexander akamuuliza kwa shauku kweli.
Minnie alitikisa kichwa tu kukataa haoni, Alexander akapoa Ghafla huku akimsogelea karibu.
“” Hauoni tenaa!! Minnie kwanini Sasa imekuwa hivi Mimi sikutaka uwe hivyo,, yaani Maina jamaniii sitakaa nimsamehe.”
Muda huo huo Simu yake ikaita unaambiwa usiempenda kaja,, Alikuwa ni Maina mwenyewe kapiga simu. Alexander akafanya kuitazama simu kwa hasira akapokea akitoka nje.
“” Nini wewe unanipigia simu,, umesababisha matatizo huku halafu unanipigia simu ,, Minnie kwasasa haoni mazima richa ya matibabu hakuna kilichoendelea.” Wafikili naweza tabasamu kwa simu zako yaanii ni afadhari tu usiwe wanipigia simu.” Akafanya kukata.
Daktari huku aliendelea kumkagua Minnie vizuri huku akimuwekea dawa ya maji kwenye macho yake lakini alishituka kidogo akahisi Minnie anaongopa.
“” Ni kweli hauoni au unatuigizia..!? Mbona mboni yako naangalia ipo vizuri tu! Kama unadanganya nitakuchoma sindano na dawa nyingi nitakuwekea nikizani bado unashida nikawa nimeua macho mazima.”
Minnie akafanya kumshika mkono kumzuia asiendelee kuweka dawa Kisha akatabasamu.
“” Nilipona toka jana! Kwani niliweza kufungua kitambaa nikawa nimeona unajua ilikuwa ni ngumu kuamini Mimi sioni ilibidi nifanye zoezi la kuona mapema kama itashindikana Mimi kuona basi tenaa ningeangalia utaratibu mwingine, hapa naona ila mwambie Mwangalizi wangu bado macho yangu hayajawa na uwezo nitakuwa naona taratibu,, vinginevyo hata hivyo sioni vizuri saaanaa!”
Daktari akacheka tu akajua Minnie ni mjanja mjanja sana. Akafanya kumuminya masikio kwanza.
“” We mtundu sana halafu huyo Mwangalizi unayemuita hivyo yeye anakuita “mkewangu “.
Alexander akawa kaingia akimuwahi Minnie alimtizama usoni akifanya kukagua macho kwa makini.
“” Unaniona lakini hata hii tshirts nyekundu huoni hata wekundu fulani kama damu hivi huoni, hebu vuta taswira ya damu inavokuwa ndio nimevaa hivyo.”
“” Mimi naona kijivu, inafanania na weusi kidogo.
Alexander akahisi kuchoka inamaana aliona kijivu na weusi wakati alivaa nguo yakung’aa kabisa si bora hata angetaja rangi zenye mng’ao angalau hata piki, orange, purple angalau ingetia matumaini lakini hii nyeusi akahisi ni bado yupo vile vile hakuna hata kilichoendelea, ikabidi amgeukie Dokta.
“” Daktari fanya utaratibu wa operation hii itasaidia yeye kuona angalau nitimize ahadi yake tu.”
Daktari akamtizama Minnie lakini Minnie macho yake yalisema kabisa asizungumze kitu chochote akakiuka makubaliano yake.
“” Aaa Bwana Alexander! Nimempatia dawa atakuwa akitumia taratibu tu ataanza kuona, usijali hari aliyonayo nikwakuwa muda mrefu alikuwa na kitambaa na kingine ni zile dawa ndio zinafanya kazi ndiomaana anaona majivu-jivu.”
“” Sawa! Twende Minnie.”
Alimshika mkono huku akibebelea dawa walizopatiwa na Daktari kwa Minnie ndio alitakiwa kufanya namna ya kutokuzitumia labda hio ya maji ndio alifaa kuitumia.
Walifika mpaka white house wakawa wamewaeleza hari ya Minnie kwasasa, wote waliumia lakini hawakusita kumuombea Dua Ili awe salama.
Alexander alimchukua Mkewe na kumpeleka chumbani Kisha aliomba apumnzike kwanza, yeye akawa ameingia bafuni kuoga.
Minnie ikabidi achukue simu yake angalau aitumie Ile kaichukua tu anashangaa Alexander katoka bafuni na tauro alikuja kuchukua sabuni ndipo anamuona Minnie kashika simu ikabidi amuwahi.
“” Usitumie simu macho yako Bado yanasumbua! Huu mwanga wa simu utakuumiza sanaa!”
Minnie ikabidi arudishe simu huku akijilaumu sana, kwanini alifaa kuigiza hivyo wakati atahitaji simu ya mawasiliano? akajiona ni mjinga sana ana kweli alipaswa kujicheka mwenyewe.
Alexander akawa kaichukua simu na kuiweka mezani Minnie akawa anamtizama tu, baadae akawa amerudi bafuni akamfikilia kwanza muda anaoutumia bafuni akajua ni kama Dakika kumi alishuka haraka haraka kitandani Kisha alichukua simu na kumtumia ujumbe Baba’ke kuhusu Afya yake kisha alimwambia kuhusu Denison na jinsi anavyoigiza haoni akawa ametuma ujumbe ule alimuomba atamtafuta akipata nafasi Kisha simu akairudisha chapu baada ya kufuta message.
Alexander akawa ametoka bafuni alienda kufunga Mlango Kisha alitoa tauro nakuanza kupaka mafuta alijua Minnie hamuoni.
“”” Haaaa mambo gani haya,, Alexander nakuona bhana! Minnie akaongea kimya kimya akipiga jicho huku akijifunika shuka.”
“” Minnie itabidi useme mapema kama macho yako hayaoni kabisa Bora useme ukafanyiwe upasuaji, najua unaogopa.”
Alexander aliongea huku akivaa nguo zake, Minnie muda huo hakujibu zaidi ya kujifanya kasinzia.
“” Ooh Minnie usingizi tayari! ”
Alexander akaongea huku akimsogelea Minnie amkague vizuri alijua kabisa kasinzia nae alifanya kulala akizidi kumtizama.
Minnie alijua kabisa Alexander yupo karibu yake akawa anasali kimya kimya.
“” Alexander Mimi naona bhana usinisogelee kiasi hicho unafikili sioni! Wewe huogopi?”
Alexander akafanya kunyanyua mkono wake akishika macho ya Minnie yaliyofumbika alifanya kuyapapasa tu huku akizungumza.
“” Kwani macho yako yanauma pia? Najua unaumia sana wewe kuwa hivi ila utapona tu! ”
“”” Aaa jamaniii,,, sijui nigeuke hapa au nifungue macho ajue nimeamka.”
Hakili za Minnie bhana alizijua yeye.
Alitaka kufungua macho lakini alishangaa busu linatua kwenye paji la uso wake baadae Alexander alizungumza.
“” I’m sorry Minnie! Kuna utofauti nauona katika macho yangu! Lakini ni kama sijajua au labda nimeanza kukupenda?
Hapo Minnie alijikuta anafungua macho Ghafla tobaa! Mkosi Gani huu kwake.
“”” A a a Ale…. upo hapa!!? ”
Alexander akacheka tu alijua kashituka lakini aliamini hakumsikia.
“” Nilikuwa natazama macho yako nijue ugonjwa upo wapi? Halafu ushaanza itana vibaya ujue.”
“”” Yote ni Kwakuwa sioni ndio unanifanyia hivi ee..!?”
“” So hivyo,. Vipi walete chakula.”
“” Sina hamu ya kula.”
“” Sawa Mimi ngoja niwaone ndugu zangu hapa halafu nataka niende kazini kwetu, sitachelewa kurudi kama Kuna tatizo haraka Kuna kengele nitakuachia utachukua na kuiminya watakusikia tu, lakini nitawachia maelekezo muda wote watakuja kukuangalia.”
“” Sawa Haina shida, hata hivyo nahisi usingizi nikiamka tu… “Uwepo.”
Alexander akatabasamu tu Kisha akamtizama jinsi alivyotoa macho kumuangalia akafikilia.
“” Tazama yake ni kama ananiona lakini haoni tenaa, natamani kama ungenitizama kumaanisha.”
Minnie yupo anampimia tu na alijua kumuigizia vizuri, Alexander akawa ameondoka Ile kuondoka tu Minnie akaenda kurudisha Mlango na funguo Kisha akachukua simu yake akimtafuta Nickson kwakumtumia ujumbe.
“” Kaka Mzima lakini, Naomba unisamehe lakini hii Ndoa ndio Baba aliniomba Mimi nifanye hivyo Ili nikae karibu na adui yetu tuweze kumfunga! Naomba unisamehe kaka hii yote nikwaajili ya kisasi tu.”
Alituma akisubili majibu lakini wapi baadae akatuma tena ujumbe.
“” Kaka macho yangu yamepona tayari! Basi ukitoka kazini nipigie tuongee.””
Muda huo Nickson alikuwa akizisoma vizuri message mwisho kabisa aliamua kumbrock.
Minnie ndio akampigia simu akaona namba yake ipo brocked akachoka akaanza kuongea mwenyewe lakini muda huo Mama Miricka alikuwa akija kwenye kile chumba Alimsikia Minnie akizungumza.
“” Kaka jamani pokea simu ndio umenibrock? Mimi nilitaka kukwambia naona kwasasa lakini ndio hivyo Tena hujibu message zangu.”
Mama Miricka akasikia vizuri hakuamini ndipo akamtumia ujumbe Alexander.
“” Shem afadhari Minnie anaona nimemsikia akizungumza na mtu kuwa anaona sahii! Basi ngoja nisimsumbue anaweza kufanya mambo yake mwenyewe.”
Minnie hakujua kama Siri yake imevuja baada ya kumkosa Kaka’ke ilibidi alale tu hana mtu wa kuongea nae sahii.
Huku kwa Alexander baada kupata ujumbe alimwambia shemeji yake asiwambie familia ila wao watawafanyia suprise ila mpaka wazungumze kwanza.
“” Sasa nataka nicheze na akili za Minnie kama hataniambia anaona basi nitamfanyia vitimbwi vya ajabu mpaka akili mwenyewe anaona! Huwa namjua Bandit wangu anakuwaga na akili nyingi na ukute ni siku nyingi anaona ila kaniigizia tu, au na muda ule kitandani ashituke huenda alikuwa akiniona ee..!!? Ngoja nipite hospitali kwanza Daktari atanipa majibu.
Huku Minnie alikuwa kamaliza kuoga ashajiandaa vizuri alikaa kwenye sofa akijua muda si mrefu Alexander angefika, na kweli Alexander akawa kafika.
“” Ooh Minnie! Wajionaje khari kipenzi Changu..””
Minnie akatulia huku akimtizama Alexander anavyovua shati mbele yake.
“” Wewe vipi huko kazini mambo yamekaa sawa kweli..? Akajihami kuuliza vile huenda Alexander angeishia kuvua shati tu.”
Alimsogelea karibu akakaa pembeni yake akiwa kifua wazi, kumbuka muda huo Alexander ashaambiwa Minnie anaona.
“” Leo umependeza sana ni nani aliekuvalisha hivi..!? Ni mrembo kweli. Akaongea huku akimtizama usoni.
Minnie akafanya kukwepesha macho pembeni ni kama Kuna kitu alitafuta.
“” Ooh Minnie! Unahisi kuniogopa hata hunioni? Inaonekana unahisia Kali kwangu.”
“” Mimi huyu… Hahaaa Yani Mwana wa Mzobe nakuwa na hisia na Mwana wa Denishoo A.K.A Mwana wa White House ni ngumu bhana..!”
“” Ila Abdul ndio sahihi? Lakini Mimi ndio nimekuoa jifunze kuwa na hisia na mimi.”
“” Aaa Ale bhana Leo imekuwaje wewe Naomba niache bhana, maneno mengi kama umelabishwa asali na Maina, au mtoko wa Leo ulikuwa hot sana…!?”
Alexander ikabidi acheke tu huku akisimama na kuingia bafuni akiongea mwenyewe.
“” Nataka wewe ndio ukili waona kama usipokili nitakufanyia vitimbwi vingi mpaka utakaposema, najua unapenda ubandit muda wote hata kwa hiki unataka uniigizie tenaa Ili ufanye u-Spy wako.”
+++++++++
Ni upande wa pili kwa Nickson siku hiyo alikuwa ofsini kwake akiangalia picha ya Baba’ke pamoja na Minnie hata hivyo anawamisi Sana Sema njia waliyopita kwake imekuwa ni ngumu kuipitia Ukiangalia ni mtu anahesuka na kuhakikisha usalama wa Raia na mali zake isingekuwa rahisi yeye kujiingiza kwenye kisasi Cha Baba’ke.
Wakati amekaa Amri alikuja kumuita anahitajika akaonane na kamishina mkuu wa jeshi, baada ya kufika ilibidi akae kusikiliza hata hivyo walikuwa wapo wanne walioitwa pale.
“” Kamanda Amri, Sudy, Nickson Kuna mission ya kufanya mtaenda kuungana na Alex mtafatitilia kikundi Cha majambazi na mission hii mtaenda ungana na Kamanda Gamaya ndio anahusika na hii kesi kwahiyo kesho jiandaeni mtabeba mizigo yenu tayari kwa safari ya kwenda mpakani Zanzibar.
“” Ndio Kamanda! ” Wakaitikia kwa pamoja.
Nickson ikabidi arudi kwenye chumba chake akiwa na mawazo sana! Anajiuliza hiyo Mission… Zanzibar,, ,,,yaani alipo Minnie ndio wao wataenda kufatilia mission hiyo akawa haelewi kabisa.
Huku kwa White house alipokea simu kutoka kwa Kamanda fulani akimjulisha habari kuhusu kesi yake wakawa wamechukua kama nusu saa wakizungumza.
“” Sawa Kila kitu kitakaa sawa! ” Ndio mazungumzo yao yakaishia hapo.
Baadae alikuja Mr Gelu akitoa taarifa na yeye ni kuhusu biashara aliyoenda kuisimamia, Kisha White House akamuomba watoke wote na muda huo ilikuwa ni Majira ya usiku.
Upande mwingine ni kwa Alex Majira hayo hayo alipata muda wa kwenda bustanini kuzuru kabulini kwa Mama’ke kama kawaida yake, Alimkuta Mlinzi akisinzia ikabidi amshitue kwa kumuingizia njiti sikioni alishituka sana halafu Alex akabaki kucheka tu.
“” Oyaa acha kulala bhana! Utaibiwa.. Ngoja niingie bustanini kwanza.”
“” Aaa samahani mkuu! Nisamehe kwanza si unajua usingizi..?”
“” Usijali bhana.”
Muda huo huo Chumbani kwa Minnie alikuwa kalala huku akimtizama Alexander ambae anafatilia mpira kakaa kwenye sofa na pembeni kulikuwa kunae kinywaji Minnie akawa anamtizama vizuri kama atakunywa kile kinywaji baadae ndio anamuona Alexander kashika Glass akanywa Minnie akahisi kucheka kwanza kwa furaha Kisha alianza kumhesabia dakika tano, muda sio mrefu Alexander akahisi usingizi akaamua kuzima TV Kisha alikuja kujitupia kitandani akimtazama Minnie ambae anaonekana kusinzia alichofanya alimkumbatia akiamini Minnie kapitiwa usingizi.
“”‘ Sasa huyu jamaniii mbona ananiigizia muone alivyonishika .” Minnie akaongea taratibu asisikike lakini Alexander akazidi kumkumbatia huku akimtizama usoni.
“” Sawa nasikia usingizi mzito sio ndio uniache humu ndani?”
Minnie akashituka kwanza inamaana alijua anamuacha akaona ni wenge tu. Alijituliza kwa muda baada ya kuona kasinzia alijitoa kimya kimya Kisha alifungua mlango taratibu akinyata kutoka nje, na hapa alikuwa akielekea bustanini kama kawaida yake.
Alifanikiwa kutoka mpaka nje akawa amefika eneo la bustanini alimtizama Mlinzi ambae kakaa kwenye mti kaegama akawaza namna ya kupita pale alichoamua alitupa jiwe upande wa pili Mlinzi akawa ameshituka kuangalia kule hapo hapo Minnie alimpita kama mshale akielekea kwenye bustani hiyo ambayo alikuwa akiiona kwa mbali leo hii ndio alifanikiwa kufika kwenye Ile bustani alianza kukagua ndipo anaona katika bustani hiyo Kuna makaburi manne alianza kuyatizama vizuri Moja baada ya jingine, la kwanza aliona ni kama la mtu mzima alizaliwa 1977(47) na Kaburi hili lilikuwa la Utambulisho wa majina ya mwanamke yaani Eunice N kyela , na Kaburi jingine lilikuwa na Utambulisho wa majina ya kiume Nashon Denishoo mwaka wa kuzaliwa 1995(29), Kaburi jingine hakuona vizuri maandishi yake kutoka na mwanga hafifu na jingine ndipo anashangaa kuona Kuna mtu akasituka kwanza akajua ni mzuka amaa, alitaka kupiga kelele lakini akawa amesikia maneno ya mtu huyo akizungumza.
“” Mama Leo mwanao Nimekukumbuka sana! Nimekuja hapa kukuaga naenda kufanya mission ya hatari Naomba baraka zako ziambatane na mimi!”
Minnie akafanya kusogea karibu akizidi kusikiliza sauti vizuri ndio anasikia ni sauti ya Alex akashangaa ni yeye tena alikuja kuomba Dua kwenye Kaburi la Mama’ke akawa amesogea karibu ndipo alipata kulisoma vizuri liliandikwa Miricka Deusdely, kuzaliwa 04. 12. 1976 akawa kashituka kwanza akirudia kusoma mara mbili mbili ndipo anaona majina Yale Yale alivyoyasoma mwanzo ni sahihi alivyoyarudia akahisi kuchoka kwani majina Yale yalifanana na ya Mama’ke mzazi na yeye alipoteza maisha ilikuwaje Tena yakawa huku hata tarehe za kuzaliwa zifanane?
Alibaki ametulia pale akiwa amechoka, muda huo Alex alimaliza kufanya ibaada yake akifanya kunawa na kutoka pale akitumia simu yake kumulika Ili apate mwanga, Minnie alibaki akimtizama tu baada ya kuondoka na yeye alisogea pale Ili ajihakikishie kweli alikuwa ni Mama’ke hata picha yake iliandikwa pale.
Alitoka pale akiwa na hasira akijua White House alimuua kweli Mama’ke na aliamua kuweka kumbukumbu za mwili huo kwenye himaya yake, na kitu kingine alichokiwaza hata miili iliyolala pale napo alifanya vilevile kuwaua. Alitoka bustanini akiwa na kisasi kikubwa moyoni nafisi yake ikivuja jasho.
Alifika mpaka chumbani kwake alimkuta Alexander Bado kalala alifanya kukaa kwanza akimtizama vizuri usoni anamaswali mengi ya kumuuliza amjibu, alijikuta akitamani kumuuliza kwa hasira aliyonayo hakusita kuchukua maji kidogo akimnyunyuzia usoni. Alexander ndio akamuaka akiwa na wenge kweli.
“” Wee Minnie… Nini lakini…!?”
Minnie alimsogelea na kumkaba Shingoni wakizidi kuvutana kitandani Minnie akiwa kawaka hasira.
“” Hivi Baba’ko wewe kaua watu wangapi? Sio Miricka tu hata Eunice , Nashon nae aliuwawa kwanini lakini Baba’ko ni shetani namna hiyo?”
“” Wewe spy girl umechanganyikiwa eee? Au kwakuwa unaona? Nilitegemea ujiziilishe mwenyewe waona na sasa umeweka wazi Kila kitu,, kingine acha kumzungumzia vibaya Mamangu, pia acha kumzungumzia vibaya Kaka’ngu, halafu naomba uwaache wapumzike kwa Amani.””
“” Mama’ko..!? Mama’ko yupi sasa! Halafu au Mamangu mimi ndio wamzungumzia? Acha pia kumzungumzia vibaya Mamangu.”
Alexander akashusha pumnzi kwanza Kisha alimvuta Minnie karibu amhoji vizuri.
“” Ulienda kufanya ubandit tenaa! Nilijua tu waona ukaona uichukulie nafasi ya upovu kwa matakwa yako, lini lakini Minnie utaacha u-Spy? Kwanini usitulie na mimi jamaniii!”
“” Sitaki kuchanganywa na familia ya wauaji, Naomba uniache.”
Alexander alimshika kisha alimkaba alimsogeza Hadi mezani kunako Ile Glass ya kinywaji kumbe alikunywa kidogo akawa kabakisha na aligundua kabisa Minnie alimuwekea vidonge vya usingizi, alimnywesha kwa nguvu Minnie akajitahidi kufurukuta kwakuwa ni mwanaume alishidwa kumhimidi akawa mpole akawa amekunywa juice yote.
“” Alexander nikifa,, jamaniii Mimi nakufa leo wakati Bado sijamaliza kazi yangu,, Alexander nakufa jamaniii..š
Alexander akabaki kucheka tu inamaana yeye anakufa wakati yeye alimuwekea juice hiyo hiyo na hakufa mbona alizidi maigizo huyu.
Nini Kitaendelea?Ā Usikose SEHEMU YA KUMI NA TISA YA KISASI CHANGU
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMĀ Ā
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAĀ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAĀ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIĀ
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoĀ kijiweni.co.tzĀ unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiĀ editor@kijiweni.co.tzĀ Ā Ā
KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU
18 Comments
Admin kwann unatuungiaa na story ya nyuma…n ngumu kutfta seem iliobaki ..
Isichelewee tenaa tenaaa
Admin unarejea stroy ht sio ndefu
Hujatutendea hak Admin, bas tuongezee sehem ya 19
Leo umepuyanga boss
Kunaulazima Gani wa kuunganisha story iliopita na inayoendelea admin unatukosea Sanaa
Admin umejivuruga unachanganya madawa
mhu story nzuri sema usichanganye na vilivopita
Mbna unachanganya na ya nyuma jaman
Imechanganywa sanaa shida nini
Oy admin unazingua mzee iyo kuchanganya changanya ndo nini sasa
19???
Story tamu lakin unatucheleweshea Hadi inapoteza Radha
Kwel lkn
Admin unarejea inaonekn ndefu kumbe ni fupi sann
Yaan nimetumia nusu dk 15 kutafuta nilipo ishia oooh mung
Admin unaboa kwa kweli.
Ni mm tuu au Kuna mwingine kaona kama admin anarudi kitu kile kile ambacho tumesha kisoma???