Ilipoishia ” Alexander nikifa,, jamaniii Mimi nakufa leo wakati Bado sijamaliza kazi yangu,, Alexander nakufa jamaniii..
Alexander akabaki kucheka tu inamaana yeye anakufa wakati yeye alimuwekea juice hiyo hiyo na hakufa mbona alizidi maigizo huyu.
Endeleaย
SEHEMU YA KUMI NA TISAย
Minnie akawa kapitiwa na usingizi Alexander ikabidi akae akimtizama yaani hamuelewi Binti huyu ni lini ataweza kutulia ndani? Hakuwa na namna zaidi ya kuvuta shuka akimfunika na yeye alilala kando yake.
Asubuhi kunapambazuka leo White House aliitwa Mahakamani tayari kusaini kesi ya miaka ishirini kupita, kesi hii ilimshurutisha kuwa yeye ndie muuaji wa Miricka Deusdely tayari kesi hii ilifunguliwa upya na mshitaki alikuwa kamanda Mzobe, wote waliambatana na wanasheria wao tayari kwa kuanza kesi.
Huku kwa Alex siku hiyo alikuwa akiandaa nguo zake tayari kwenda kuwapokea wenzake kwa mission ya kufatilia majambazi sugu wanaonyanganya Mali za Raia.
Kwa Minnie ndio anasituka usingizini ikiwa ni Majira ya saa tatu anaamka anakuta Kuna kifungua kinywa mezani kimeandaliwa, akawa anatizama kama Alexander yupo hakuona mtu ikabidi ainuke kwanza nakuingia bafuni angalau apige maji Ile kamaliza tu kuoga alisikia Mlango unafunguliwa kuashilia Kuna mtu anaingia.
“” Nani tena huyu asiwe Alexander kafika wakati Mimi sijaandaa nguo.”
“” Minnie kipenzi! Ooh come on baby! Mbona hujanywa chai jamaniii? ” Leo na surprise.”
Alexander akaongea huku akiweka gauni kitandani..”” Na uhakika ukivaa gauni hili utapendeza.””
Minnie ndio akafungua Mlango akiwa kajitanda kanga kwenye mwili japo alikuwa na wasiwasi sana alijitahidi kujibana kutembea ni kama asionwe na Alexander lakini Alexander alikuwa akimtizama tu.
“” Wakati mwingine jiachie tu Mimi nishakuwa mmewako sahii nitakuwa nafanya majukumu kama Mme kuhusu unyumba nitasubili ridhaa yako.”
Minnie akahisi kama atakufa hizi siku za usoni kwa maneno ya Alexander ikabidi ajifiche nyuma ya kabati alipaka mafuta yake haraka haraka akivaa nguo lakini Alexander alimzuia.
“” Mrs Alexander nguo yako ipo kitandani Naomba uvae nguo hii.”
Minnie akawa ametoka nyuma ya kabati akiwa Bado kajifunga kanga kifuani aiitizame nguo yenyewe.
“” Njoo uchukue mbona unakuwa muoga wakati unaweza tkwenda bustanini peke yako na usihitaji msaada wowote vipi kama monster angekutokea hukoo..!!?”
“” Aaa! Usinitishe bhana nilienda kwa mambo yangu ila nataka Leo uniambie habari ya kule Bustanini tukiwa tumekaa tumetulia.”
Akifanya kusogea na kuchukua gauni.
“” Sawa! Hata Mimi nitahitaji ukweli mtupu kuhusu wewe nataka ninfahamu vizuri Bandit girl.”
“” Hilo tu usijali.”
Minnie alimaliza kuvaa nguo yake akawa anajitizama kwenye kioo kweli alipendeza sana. Alexander akawa anamtizama tu muda huo alikuwa akihangaika kufunga zipu ikabidi amsogelee akimfungua.
“” Leo tena nimetoka msaada wa kukufungia nahisi hili tukio limejirudia kama siku Ile ya party nilikusaidia.”
Minnie ikabidi amgeukie kumtizama kwanza.
“” Ooh Bwana Alexander! Kwahiyo wataka ujira? Naona fadhira zako zinahesabika kwangu.”
Alexander hakutaka kumjibu zaidi ya kumtizama nguo ilivyompendeza alimshika mkono na kumkalisha kwenye kiti huku walibaki kutizama nyuso zao kwenye kioo, Alexander ikabidi achukue chana Kisha alianza kumtengenezea nywele, Minnie akawa ametulia tu akimtizama kupitia kioo chake alivyo makini lakini Kuna kihali fulani alikuwa anahisi kwa mtu huyu hakuacha kuzungumza na moyo wake.
“” Unaonekana kuwa romantic sanaa! Kama ulifanya hivi kwa Maina nahisi nyakati hizi kwake imekuwa kumbukumbu lakini vipi kuhusu Maina kweli…!?”
Minnie baada ya kutafakari vile ikabidi amgeukie amuulize lakini Alexander akawa kamrudishia kichwa chake aendelee kutizama kioo.
“” My bandit girl! Hebu tulia basi nifanye kazi yangu kwanza! Kuna kitu wataka kuniulizia?”
“” Yaah ni kuhusu Maina, Atakuwa kakumbuka sana huko aliko jitahidi Leo ukaonane nae.”
“” Mhu! Sereously..? Aaa Maina nahisi kwasasa natakiwa nikae mbali nae Ili nimtizame bandit girl, kama napojaribu kutoka hata kwa dakika Moja tu anakuwa kaharibu, vipi kama nitaenda kumuona si nitakuta ushachukua jembe upo kupalilia bustani na wakati sio kazi yako, Hapana… Malkia wangu atapauka.”
Minnie ikabidi acheke tu make alizidisha maneno na alimuita Malkia wake daah!?”
“” Oooh nahisi njaa Kwanza, nimetosha bhana kama ungenibana mkia wa farasi ingekuwa rahisi kuliko hata unavyohangaika, Sema nimependeza Ahsante Bwana Alexander.”
Aliongea na kuinuka Kisha alienda kukaa mezani na kuanza kunywa chai, Alexander nae ikabidi amfuate.
“” Ulisema utanijibu maswali yangu! Naweza uliza sasa?” Minnie akaongea akishusha kikombe Cha chai amsikilize.
“” Okay,, just continue..!””
“” Kule bustanini,,,, Kuna Eunice,, Kuna Nashon, halafu Kuna majina ya Mamangu nae kalala pale.. Sasa najiuliza wale ni kina nani ukitoa Miricka Deusdely… Nijibu hayo kwanza halafu nitauliza tenaa..!?”
“” Wewe mtoto wewe!! maswali Gani tena hayo ya wafu? Kwanini unataka ujue?”
“” Please Alexander uliniahidi kujibu maswali yangu nambie basi, si hata wewe utaniuliza na miminitakujibu..? “”
“” Basi nikuulize kwanza Mimi! Na swali Moja tu make hayo yako kama tutaongea yatafanya nisahau swali langu.”
Minnie akafikilia kwanza baadae akamjibu.
“” Okay nambie..”
“” Simama kwanza.”
“” Aaah vya kusimamishana tenaa?”
“” Yaah! Come on.”
Ikabidi Minnie asimame muda huo Alexander alimshika mkono akimsogeza kunako kioo, akawa hamuelewi lakini Alexander alifanya kusimama nyuma yake Kisha alimkumbatia akimtizama kupitia kioo akizungumza.
“” Unamuona Minnie wangu kule..?”
Minnie akafanya kutabasamu tu Bado hajamuelewa Mana’ke.
“” Ee huyo ni Mimi namuona.”
“” Huyo pembeni yake nae wamuona..?”
“‘ yaah namuona, Si Alexander nyuma yangu.”
“” Upo sahihi. Sasa hao watu wawili waliopo kwenye kioo,, mmojwapo ambae ni mwanaume… Kwasasa anampenda Minnie wa kwenye kioo japo huyu alienae hapa nyuma’ke ndio anampatia mashaka, Imekuwa ni muda anawaza ni namna gani anaweza mbadilisha akawa mwanamke anayetunza nyumba yake vizuri. Sijui unanielewa Minnie..?’
Aaa!!! Minnie alijikurupua mapema kwenye kumbatio lile ashajua ashaanza maneno yake tena, alifanya kuondoka lakini Alexander akamrudisha kwa kumshika Minnie mkono Kisha alimleta karibu yake.
“” Miniiii nipo sereous lakini! Nahisi kumpenda bandit girl! Najua hutanielewa sahii lakini ipo hivyo, sitataka kulazimisha unipende lakini sitaruhusu ukae mbali na Mimi hata baada ya kukamilisha mission yako kwa lolote lile litatokea sitatoa taraka. Kama hutanikubali Mimi nitaishi na wewe kama mke na Mme bandia.. sawa tu’ Ndoa tuliyoifunga naona kwangu ipo sahihi tu.”
Minnie hapa alibaki kachoka akimtizama Alexander asielewe, Alexander ikabidi amshike mkono akimsogeza kunako meza waendelee kunywa chai, Aaa… Minnie alishidwa hata kunywa chai akawa kasimama aondoke.
“” Minnie wapi wataka kwenda? ” Kama utashuka sebuleni… Familia nzima wanatusibili sisi.”
Minnie akamgeukia.
“” Kwanini watusubili? Kuna Nini kwanza?”
“” Wewe nisubili hapo.”
Alexander alimalizia kunywa chai huku akichukua tishu akifuta mikono yake Kisha alisogea kunako dressing table akapakaa mafuta kwenye mikono yake kukata harufu ya supu.
“” Basi twende.”
Minnie ikabidi aongozane nae taratibu huku Alexander akiwa kamshika mkono, walifika mpaka sebuleni wanashangaa kuona baadhi ya wanafamilia wapo wamewasubili kwa hamu. Bibi baada ya kumuona alimuwahi kumkumbatia.
“” Ahsante jamaniii mjukuu wangu anaona! Minnie unaniona vizuri lakini..?”
Minnie akamtizama kwanza Alexander akimkata jicho akimfikilia”” kumbe suprise yako ulitaka kunidhihilisha naona..? Ungeniuliza kwanza kama natakiwa nione sahii au baadae baadae..!?’
Hakili za Minnie bhana zilifurahisha tu ni kweli alitaka aone baadae na sio Sasa na wakati aliona..๐?”
Wanafamilia walifurahia pamoja wakiwa na furaha kabisa baadae alikuja Miricka nae akawahi kumkumbatia Mama’ke mdogo.
“” Mamaa umepona sahiii?”
Minnie ikabidi amnyanyue Ili amtizame vizuri.
“” Si unaona macho yangu..? Mi naona sahiii..! Leo nitakusomea hadithi nyingi Ili ujihakikishie naona.”
“” Sawa ma’mdogo Saangapi hiyo.?’
“” Mida mida tu.”
Miricka ikabidi ashuke akielekea chumbani kwake ni vile alifata vitabu.
Minnie akamtizama baadae kumbukumbu ya jana ikamjia kichwani… Pale amuone Alex kwenye Kaburi la Mama’ke yaani Miricka Deusdely.
“” Kwenye Kaburi Alex alikuwa akiomba Dua kwenye Kaburi la Miricka Deusdely halafu mwanae anaitwa Miricka inamaana jina hili lilitokana na Miricka Deusdely alielala, inamaana ni jina la kurithi..!!!!? ”
Hapo hapo akapanda juu na yeye akizidi kumuita shemeji yake (Alex) amuulize vizuri.
Mama Miricka ikabidi amfuate nyuma nyuma Kisha alimshika mkono.
“” Baba Miriii ametoka kwasasa yupo kambini hatutakuwa nae kwasasa karudi kazini.””
“” Hebu mpigie kwanza nataka nimuulize vizuri kwenye Kaburi la Miricka ni la nani yake? Kwa kifupi nataka kujua kuhusu Miricka Deusdely.”
Wanafamilia wote wakamshangaa yaani Minnie anataka kujua kuhusu kifo Cha Miricka Deusdely kiaje Ani?”
Bibi ikabidi amfuate Kisha alimshika mkono, Alexander nae akawa amesogea akafanya kumshika pia.
“” Kwanini unakuwa hivyo Minnie muda wote unafatilia habari hii wataka ugundue Nini nilikwambia wale ni wazazi wangu sitaki kusikia kauli zako unanichosha hizi habari zakuongelea marehemu.”
Alifanya kumshusha chini akimpeleka chumbani kwake akatulie.
“” Lakini Alexander si uniambie jamaniii, Yule Miricka Deusdely ni Mamangu Mimi tarehe na mwaka uliondikwa pale zote ni tarehe za Mamangu iweje anakuwa huku halafu huyo Alex alienda kuomba Dua pale, Mimi nataka anieleweshe tu kuwa yule pale ni nani kwake?”
Minnie akazidi kulalamika muda huo Alexander kasimama kampatia mgongo hajui azungumze nini anyamaze huyu mwanamke.
“” Minnie kuwa mpole basii mbona unatuchanganya hivyo! Ayaa alielala pale ni Mama’ke Alex, Na alifariki miaka ishirini kupita, Bado sijakujibu tu…?””
Minnie hakuamini kwani anakumbuka hata Mama’ke nae ni miaka ishirini kupita alifariki inamaana ndie Mama’ke? ikabidi asimame kwanza akielekea alipo Alexander.
“” Basi yule ni Mama’ngu pia! Kwanini Sasa yupo pale si niliacha Kaburi lake Mbeya?”
“” Mbeya tenaa? Wewe Mbeya ulienda kufanya Nini..?’
“” Kule ni Nyumbani inamaana huelewi..? ”
“” Nyumbani..!!? ” Sio tenaa Mwanza?”
‘” Mwanza ya wapi tenaa Mimi nyumbani Mbeya.”
Alexander akachoka anakumbuka tangu Minnie aingie White House taarifa zake zilielezewa yeye na Baba’ke ni wenyeji wa Mwanza- Magu tena huko ndani ndani Mwatelesha na ndio Utambulisho wao na vipi tena kuhusu Mbeya hii imetoka wapi tenaa..?
Minnie wakati huo akizidi kuonesha bado kachanganyikiwa ni haelewi, Simu yake iliita ilibidi apokee lakini muda huo Alexander akaamua kutoka nje huenda kama ataulizwa na yeye angepata majibu! Alienda kumpigia simu White House aulizie vizuri kuhusu Minnie kwani ni mzawa wa wapi na kingine alitaka kuuliza kuhusu habari ya kifo Cha Miricka Deusdely yaani Mama’ke wakambo walihisiana vipi?
Wakati anapiga simu, Minnie nae alikuwa akiongea Ile simu aaliyopigiwa ilikuwa ni ya Kaka’ke.
“” Aaa kaka ni wewe? yaani leo umenipigia simu umesema upo Zanzibar?”
“” Miniii sijakupigia simu kwa shauku ya wewe kukurudia kama ndugu yangu ila natoa tahadhari,,, kama mnaendelea na u-Spy temu hii tukikutana katika kazi sitawatambua ni hilo tu.”
“” Kaka! Kwani upo wapi jamani kwanini tukutane katika kazi? ”
Nickison akawa amekata simu huku Minnie akabaki kwenye sitofahamu.
Huku kwa Alexander simu zake zilikuwa hazipokelewi ikabidi akate tu Haina maana tenaa, alitoka nje kuchukua gari amfuate Moja kwa Moja kazini kwake japo hakujua kama yupo mahakamani.
Huku Mahakamani White house alitoa ushahidi kumuonesha kuwa yeye hahusiki! Ilikuwa ni Flash ilimuonesha Yeye hakushika Bastola kumfyatua risasi Miricka Deusdely..
Kamanda Mzobe nae akatoa ushahidi wake nae alikuwa na flash ilionesha White House ( Denishoo) baada ya video yake kuisha ilionesha flash aliyokuwa nayo Kamanda Mzobe iliendeleza tukio lile lile ni Kamanda Denishoo alishikilia Bastola na flash hii ilikuwa upande wa Kamanda Mzobe
Wasimamizi wa kesi hii walihisi kuchoka ndipo Mwanasheria wa Kamanda Mzobe alisimama.
“” Ndugu mshitakiwa kwa ushahidi huu unaonesha wewe ndio umehusika na mauaji ya Miricka Deusdely,, mara ya kwanza ulisema wewe hauhusiki na mkononi haukushika bastola lakini kwa hapa tayari umeshika bastola na hapa inaonesha kabisa ulihusika na mauaji hayo.”
Mwanasheria wa Kamanda Denishoo( White House) nae akasimama.
“” Ndugu Mshitaki! Ushahidi huu wa kushika Bastola peke yake haujitoshelezi! Mtu yeyote pale angeshika Bastola Naomba rejea kwenye Crip yetu mara ya pili tuone kwa ukaribu,,, Unaona hapa… Kamanda Mzobe pia alikuja na vijana wake nao walikuwa na siraha lakini sio hivyo taharuki hii ilipotokea hata walinzi wa Kamanda Denishoo nao walifika wakiwa na Bastola Ili kumlinda Bosi wao!! Inamaana hii kushikilia Bastola iliashilia alipatiwa na walinzi wake Ili kuokoa maisha yake tu na sio ndio alifyatua risasi, Katika kusema hivi namaanisha Mteja wangu hahusiki kwenye kesi ya mauaji,, labda kwa ndugu Mshitaki hebu atupatie ushahidi unaoonesha Denishoo akiwa na Bastola na ameiruhusu risasi itoke.. kingine naweza Sema Kamanda Mzobe ndio anahusika maana Bastola yake ilikamatwa na ndani ya risasi zinazitakiwa kukaa risasi Saba na hii yake ilionesha risasi Moja imetumika na ushahidi tunao.”
Muda huo majaji walikuwa wakisikiliza kesi hii kwa umakini kabisa huku wakinipatia point kadhaa kwa mshitaki na mshitakiwa.
Wakati huo huo Alexander alikuwa amewasili eneo hilo baada ya kwenda ofsini akamkosa Baba’ke ilibidi apige simu kwa Bibi ndio akawa ameelekweza sehemu alipo.
Huku kwa Mwanasheria wa mshitakiwa Bwana Denishoo, alitoa ushahidi wa Bastola na kuiweka mezani na waliiangalia kweli risasi Moja ilitumika!! Ikabidi majaji wamgeukie Kamanda Mzobe.
“” Ndugu Mshitaki,, Mshitakiwa wako ana ushahidi huu hapa mbele ya mahakama! Una kitu Cha kujitetea zaidi au Mwanasheria wako atupatie majibu?”
Mwanasheria wa Kamanda Mzobe ikabidi atambe kwenye jukwaa lake.
“” Kwa ushahidi huu hauwezi ukamfunga mteja wangu kuwa ndio kahusika kwa mauaji, mtu anaweza chukua Bastola na akatoa risasi Moja Kisha akasimama na ushahidi kuwa risasi hiyo ndio ilimdhuru mtu lakini ikawa siyo Mimi naamini ushahidi huu ni wakutengeneza tu.”
Jaji akageukia tena kwa Mwanasheria wa Kamanda Denishoo.
“” Upande wa mshitakiwa unakanusha vipi maneno haya yakuthihirisha ni kweli amehusika?”
Ikabidi asimame kwanza huku akimtizama Mwanasheria mwenzake baadae aliitizama safi ya majaji akizungumza.
“” Ushahidi pia bado upo wakujitosheleza, Nilijua maswali haya yatakuwepo! Hebu Doctor Gwambae njoo utoe ushahidi.””
Kamanda Mzobe akaduwaa kwanza akaona kesi Mbona inazidi kuwa kubwa, kaifungua yeye lakini anaona ushahidi pekee hautoshi.
Doctor Gwambae akawa amefika akiwa na ushahidi, aliwapatia majaji faili kwanza wapitie Kisha aliongea.
“” Mnamo tarehe 06 June 2004 Bwana Denishoo alifika hospital akiwa na Bastola pamoja na sample ya damu iliyokuwa katika Bastola tulipima damu Ile iliyokuwa kwenye Bastola finger print zake zilionesha kabisa ni za Kamanda Mzobe! Na documents zote zipo hapa kuonesha ushahidi.”
Ikabidi wazipitie lakini hata hivyo muda ulikuwa umeenda mahakama iliomba iitishe kesi hiyo baada ya wiki mbili tena Ili Kamanda Mzobe aje na ushahidi unajitoleza ambao utaonesha kuwa hahusiki na mauaji make kesi tayari imeshamuangukia japo yeye ndio alienda kufungua faili upya la kesi hiyo… “” Ukisikia usifukue makabuli yaliyozikwa ndiyo huku Sasa” wahenga walikuwa na maana ya maneno haya.
Huku Alexander alikuwa akishuhudia vizuri kesi hiyo alihisi kumuonea huruma Minnie huku wanakoelekea siko kuzuri anaweza kumpoteza Baba’ke kwa kesi isiyokuwepo.
Hakutaka hata kuongea na Baba’ke tena zaidi ya kuelekea nyumbani akiwa na mawazo sana! Alifika chumbani anashangaa hamuoni Minnie ikabidi atoke nje kumtafuta alimuulizia kila mtu lakini hakupata majibu zaidi ya kuanza kumtafuta maeneo yote ndipo akajiongeza kwenda sehemu ya mazoezi akijaua Minnie yupo pale na kweli alikuwa maeneo Yale.
Muda huo Minnie alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa katika mashine ya kukimbia akizidi kuongeza MwendoKasi ni kama alikuwa kwenye mteremko mkali uliomzidia. Alexander alimtizama kisha alifanya kuzima mashine, Minnie ndio akahisi kizunguzungu akawa anasua-sua kuanguka Alexander akawahi kumshika Kisha alimnyanyua kumtoa pale akaenda kumkalisha kwenye bembea kwanza Kisha alimuuliza.
“” Ni sahihi kwa mnachokifanya leo Baba’ko kesi aliyoifungua naona kabisa inaenda kumzidia, okay! Si unataka uhuru kwasasa nakuruhusu ukatafute ushahidi wa kushinda kesi laah hivyo Baba’ko atafugwa tena! Kama utatoka nje itakuwa ni kwa ruhusa yangu nimekuruhusu nenda katafute ushahidi na kama mkishidwa basi mwambie Baba afute kesi Ili muishi kwa Amani.””
“‘ Maneno yako ni kama ya busara lakini siyataki wakati huu! Madam umeniruhusu nitoke nje Kila kitu kitakaa sawa na Baba’ko kama kahusika kwenye mauaji lazima awekwe ndani.””
Alexander alimtizama tu kisha aliimuacha pale aamue yeye kipi ni sahihi.
Muda kidogo Minnie alikuwa ndani tayari kajiandaa kutoka nje akatafute ushahidi pamoja na Baba’ke, alivalia suruali yake vizuri pamoja na tisheti huku miguuni akivaa raba! Muda huo Alexander alikuwa akimtizama tu vile anahangaika kubana nywele zake Kisha alitupia kofia na hapa Alexander ndio akamjua vizuri Minnie alifaa kuwa Spy girl kwa mavazi yale, kabla hajatoka alifanya kumuita akimfuata.
“” Ulisahau Simu! Kama utapata shida yeyote Naomba nipigie tafadhari! Kingine subili nikutoe ndani kupitia mlango wa nyuma , kwa haya mavazi yako kama Bibi atakuona utamuumiza sana.””
Minnie hakuwa na namna zaidi ya kumfuata nyuma nyuma! Baadae alimfikisha hadi Mlango wa nyuma na Mlango huu ulikuwa ni mdogo sana uliashilia ni wa dharura tu akawa kamtoa Minnie lakini Alexander hakutamani kabisa aende aliishia kumnyoshea mkono tu akimhitaji.
Minnie hakutaka kusubili hapo hapo aliita tax tayari kuelekea nyumbani kwa Baba’ke.
Upande mwingine Alikuwa ni Alex kakutana na Makamanda wenzake yaani Amri, soudy, Nickison na wengineo huku wakiwa na jenelali mkuu wa jeshi akiwapatia ramani ya kuingia kwenye mjengo mkubwa uliokuwa ukimilikiwa na waziri wa kilimo na ndie alikuwa akimiliki kikosi kikubwa Cha majambazi hawa, hutaamini kwenye mjengo huu ndipo Minnie alipokelewa na Baba’ke kwa muda wote waje Zanzibar na hapa ndio nyumbani kwao Abdul…..
Kwa Minnie alikuwa tayari kafika nyumbani kwao wakijadili kupata ushahidi huku Mwanasheria wao alikuwepo na yeye akichangia maada! Minnie alijitahidi kuchangia lakini aliona mchango wake unagonga mwamba akaona bora akawaandalie chakula tu.
Muda huo Abdul nae akawa amefika baada ya kupata taarifa kutoka kwa Baba’ke aliingia ndani ndipo anamkuta Kamanda Mzobe yupo na Mwanasheria pale aliwasalimia pale Kisha aliulizia Minnie alipo akawa ameelekweza yupo jikoni alifika na kumkumbatia kwa nyuma huku akimsaidia kugeuza mboga.
“” Mh Alexander.. umekuja Tena huku?”
Abdul akashituka kwanza inamaana yeye aliitwa Alexander tenaa? Ndipo akamuongelesha.
“” Miniii!! Naona unamuwaza Mwana wa Adui yako..?”
Minnie ndio akajishitukia kwanza ni kweli alihisi uwepo wa Alexander lakini alikuwa Abdul, akaamua kupotezea kwanza.
“” Noo najua atanifuata unajua nimetoroka kule nikawaza kaja kuniganda tenaa?”
“”” Basiii upo na Mimi hakutaharibika kitu! Vipi unapika na ugali amaa?’
“” Ugali tu,, wali nahofia kupika mbichi unajua ni siku nyingi sijaingia jikoni! Yasije fika kwa Mwanasheria,, utasikia Binti wa Mzobe hajui kupika,, kwamaana hiyo lazima wafugwe maisha.””
Abdul alicheka tu lakini akagundua Minnie hayupo sawa, kwa Minnie alikuwa akikumbuka maneno ya Alexander alivyomwambia wafute kesi kama watakuwa hawana ushahidi tosha, Ili waishi kwa amani. Akafikilia sana lakini alijipa ujasiri Kisha alimuuliza Abdul.
“” Hivi unafikili kwanini White House kamkandamizia kesi Baba? Yaani ushahidi wake hauna nguvu mbele ya mahakama na wakati aliyehusika ni white house?””
Abdul ikabidi amsogelee Kisha alikaa kwenye Moja ya sehemu ya jikoni kulijengwa kama ngazi akawa anamtizama Minnie.
“” Haya yanayoendelea ni kwakuwa white house ana nguvu sana kuliko nyie.””
Muda huo Alexander akawa kampigia simu Minnie akawa kapokea.
“” Vipi upo salama lakini? Kama kunashida nambie nije halafu ukitaka kurudi nyumbani nambie nikupitie twende wote hata hivyo nipo mjini mara Moja.”
“” Huku ni salama tu! Basi nitakujulisha.”
Kwa Alexander aliamua kutoka nyumbani angalau akatembee kidogo upweke ulikuwa mkubwa ndani baada ya Minnie kuondoka ikabidi na yeye akajipumnzishe sehemu kwanza.
Wakati amekaa pale alishangaa Kuna Dada anafika pale akiwa kavalia gauni fupi liloshika mwili wake vizuri, aliweka mkoba wake mezani huku akikaa kwa kujitupia mpaka Alexander akamuwahi kwa kuzungumza.
“” Maina Nini tenaa hivyo,, utaumia basii.”
“” Unajali kuhusu Mimi! Na vipi kuhusu kiumbe nilichonacho tumboni?””
Alexander akashangaa kwanza ikabidi asogeze kiti akiegama mezani amuulize vizuri.
“” Kiumbe…!!? Kiumbe Gani hicho?”
Maina akajibetua kidogo akimtizama Alexander kwa jicho la uchu Kisha akalamba midomo yake.
“” Unakumbuka mara ya mwisho tukutane..? Kwa mihemko yako hizi siku za karibuni unaitwa Baba!”
“” Hapana haiwezikani! Mbona swala hili tushalizungumza mapema! Mimi kwasasa nimeanza maisha mengine kwasasa nipo na mkewangu Minnie.”
Maina alicheka kwanza huku akirudia kutaja jina la Minnie.
“” Ooh Minnie! Minnie! kwasasa unamhesabu ndio mkeo lakini unajua hivi karibuni wataenda kuozea jela ikishindikana kwa kesi walioianzisha basi Kwa ubandit.”
“” Sina uhakika na ubandit wa Minnie japo napenda kumuita vile! Simaanishi kama anaweza kuwa hivo.”
“” Sawa hata hivyo nilikuja kukuhabarisha tu kuwa Mimi na wewe hatuwezi kuachana kizembe namna hiyo ulipo nipo, kingine kaangalie usalama wa mkeo kwanza sahii tu utasikia yupo jela.”
Huku kwa Minnie baada ya kumaliza kupika ikabidi watoke na Abdul angalau kutembea hata hivyo kamisi mitaaa ilibidi waende Moja kwa Moja kwao Abdul angalau akacheze na wenzake.
Alexander maneno ya Maina yalimuingia sana ikabidi aende nyumbani kwa Kamanda Mzobe haraka aulizie habari ya Minnie lakini akiambiwa ametoka na Abdul akawa ameomba kuelekezwa alipo hata hivyo bado ni Mme tu anapaswa kufatilia habari za mkewake.
Alifika mpaka kunako jengo kubwa akajitambulisha Kisha alielekeza Minnie alipo! Minnie akawa amepata taarifa akawa amekuja kumpokea Alexander.
“”” Yaani Alexander unaniganda kweli! Sasa huku umefata Nini..?
Minnie akazidi kulalamika huku wakisogea kunako bench wakawa wamekaa.
“” Mbona unalalamika sana inamaana hutaki uwepo wangu kisa upo na Abdul, Kitu ambacho sitaki kukisikia ni wewe kuwa karibu na Abdul.”
Minnie akahisi kikohozi Cha Ghafla, Alexander akawa anamtizama tu alijua kabisa maneno yake ndio yalimpatia kikohozi.
“” Basi hebu juamini! Nimesikia Kuna shida ndiomaana nikaja.”
“” Wewe umejuaje Kuna shida, au Baba’ko ndio kaleta shida?”
Alexander akawaza aseme kakutana na Maina na ndie kamwambia vile ikabidi akaushe tu.
“” Aaa namaanisha ni hisia nilizonazo kwako ndio zimenileta hapa.”
Muda huo Abdul akafika alijua kabisa Alexander yupo pale make Minnie alimuaga kuwa anaenda onana nae.
“” Aaa Bwana Alexander! Naona Sasa umefika kwenye himaya yangu! Okay karibu angalau tupate vinywaji. Ingia ndani.”
Alexander akamwangalia Minnie aliempatia ishara waongozane ndani.
Walifika sebuleni wakawa wamekaa kupata chakula! Na muda huo huo Baba’ke Abdul akawa amefika .
“” Aaa Alexander karibu naona umetutembelea Leo! Karibu nyumbani.”
Alexander akasimama kumpatia mkono ni vile walifahamiana, Abdul na Minnie wakabaki kutizamana.
“” Minnie leo umekuja na mmeo!!? Jambo jema hili sio Kila siku unakuja mwenyewe hapa na wakati najua uliolewa halafu unatembea mwenyewe mwenyewe sio vizuri.””
Minnie akahisi mtetemo kwenye tumbo lake kitendo Cha yeye kufahamiana na Alexander kilimchanganya make tayari washaanza zungumzia na maswala ya kazini.
Abdul alibaki kumtizama Minnie wote wanatazamana tu, Kwa Abdul alibaki kuumia anajua kabisa mahusiano yake na Minnie hakumshirikisha Baba’ke hapo ndio akajua amepoteza, akapata hasira akaondoka.
Alexander alibaki kumtizama chini chini Kisha alicheka akajua tayari kamuondoa hapa na yeye angebaki na Minnie tu.
Muda huo Baba’ke Abdul alimchukua Alexander wakizidi kuzungumza huku Minnie nae akiwafuata nyuma nyuma.
“” Unajua Alexander umebahatika sana kumpata Minnie ni mwanamke muelewa sana, anajituma, mchapakazi,, Naomba umtunze Binti yangu. Kingine chumba chenu hiki hapa Leo lazima mpunzike hapa! ”
Minnie akawahi kushangaa huku akimtizama Alexander usoni yaaani Baba’ke Abdul alisema wapumzike pamoja.
Muda huo Baba Abdul alikuwa tayari kaondoka ikabidi wazame katika chumba Chao walichokaribishwa.
Alexander alifanya kuufunga Mlango Kisha alisogea na kukaa karibu na Minnie muda huo alikuwa kakaa kitandani tu, Alexander akafanya kulala.
“” Minnie unafikilia Nini wakati huu! Naamini Baba’ko atakuwa salama.”
Minnie hakujibu zaidi yakuingia bafuni ajimwangie maji haraka Kisha alikuja kulala kingine alikuwa kashamzoea Alexander ni kama Kaka tu!
Alexander nae ikabidi aingie bafuni Kisha alikuja kulala huku akimtizama Minnie.
“” Baba umemuaga lakini kuwa tunalala huku?”
“” Anajua,,, Sema hajui kama Na wewe unalala huku?”
Alexander akacheka kwanza huku akimtizama Minnie usoni.
“” Sawa kwani Mimi kulala na mkewangu ni tatizo?”
Minnie ikabidi ageuke ukutani make Alexander kaanza matamasha yake.
Alexander nae ikabidi avute shuka akijifunika.
“” Alexander uliwasha feni ya Nini wakati nje Kuna hari ya mvua?”
Ikabidi Alexander azime Kisha alimtizama mkewe nywele zilivokuwa zimemwagika kichwani, alizishika na kuanza kuzifunga mabutu. Minnie akawa amemgeukia.
“” Alex unafanya Nini lakini..!?”
Alexander hakumjibu aliendelea kuzifunga mpaka akamaliza kuzifunga.
“” Hapa utalala vizuri lakini Mimi Alexander sio Alex tenaa?”
Minnie akazidi kumtizama tu, Alexander nae alimtizama vile vile Kisha alinyanyua mkono wake akimpapasa nyusi zake asiishe kumsifia.
“” Macho yako mazuri sana.”
Minnie akatabasamu tu huku akiutoa mkono lakini Alexander muda huo mkono wake mmoja ulikuwa ukitembea kiunoni kwa Minnie.
Minnie akawa ametulia tu huku hisia zikianza kumpanda taratibu! Baadae nae alipata muda wa kunyanyua mkono wake kumpatia ushirikiano.
“” Minnie! Nakupenda sana,, Naomba kwenye maisha yetu yaliyosalia tuishie wote.”
Minnie akabaki kumtizama tu tayari ashazidiwa Mahaba ya Alexander.
Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni mrefu kwa Wanandoa hawa kuungana pamoja, Alexander hakuamini kabisa kwamba mwanamke aliekuwa akiishi nae kumbe alikuwa anagrade za juu kwenye ufahamu wa hisia zake kwanini Sasa alienda kwa Maina muda huo Hadi amsababishie Minnie matatizo?
Nini Kitaendelea?ย Usikose SEHEMU YA ISHIRINI YA KISASI CHANGU
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoย kijiweni.co.tzย unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiย editor@kijiweni.co.tzย ย ย
KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU KISASI CHANGU
14 Comments
Inogire โบ๏ธ
Aaahn admin leo umetisha sana big up ๐๐๐ naomba na minnie nae apate mimba basi chap chap ๐๐
kuba babaaaaaaaaake oya oya oya tayari kimeumana huko
Admin big up leo๐
Leo admin unastahiri maua hayawi hayawi sasa yamekuwa ๐ฅฐ
Oya Yani natamani ata uitume yote ilio Baki Yani imekuwa Tam Tam kinooma
Mini apate mimbaaaaaaa
๐ฅ๐ฅ๐๐พ
Kumekuchaa๐๐๐
Hapo sasa sawa ๐๐๐๐
Sema hapo mwishoni imenoga sana ๐
๐ฅ
Umetisha mzee
Kumekuchaaa kumekuchaaa alaf mbona kama inaelekea mwishonii hvii mbona ndo inanoga