Ilipoishia “Kumbukumbu ya Desmond iliishia hapo, alitikisa kichwa chakeΒ kisha alielekea ofisini kwa Daktari wa Hospitali, DaktariΒ alipomuona Desmond alijuwa nini kimemleta, Desmond alianzaΒ kumshambulia Daktari huyo kwa manenoΒ
“Umeagiza Mke wangu apelekwe Wodi nyingine alafu MimiΒ nizuiliwe kumuona si ndiyo? Hivi unajuwa ulichokifanya?”Β Alisema Desmond kwa hasiraΒ
“Desmond hebu kaa kwanza tuongee, hili jambo siyo laΒ kulichukulia jazba, tulichofanya ni kupandisha darajaΒ matibabu ya Mkeo ili aweze kuamka haraka ” Alisema DaktariΒ huyo kwa upole sana . EndeleaΒ
SEHEMU YA SABA
“Kuamka haraka? Unajipa kazi ya Mungu si ndiyo? UnafikiriΒ Mimi sitaki Mke wangu aamke haraka? Nataka ila mlipaswaΒ kunishirikisha na sio sahihi kunizuia mimi kumuona MkeΒ wangu…Nitamuhamisha kwenye Hospitali hii haraka sana”Β Alisema DesmondΒ
“Desmond naomba unielewe, Mkeo utamuona lakini siyo kamaΒ zamani kutokana na aina ya matibabu ya sasa pia wodiΒ aliyopelekwa, nakuomba uwe mpole. Muhimu Ni afya ya MkeoΒ Desmond” Alisema Daktari lakini Desmond alizidi kuwa juuΒ
“Natoa siku mbili Mke wangu awe amerudishwa kwenye wodi yakeΒ aliyokuwa akikaa, vinginevyo nitamuhamisha hapa” AlisistizaΒ Desmond kisha aliondoka zake, lakini Daktari aliwaza sanaΒ ikiwa Desmond anampenda mke wake kwanini akatae asipatiweΒ matibabu kwenye wodi mpya? Kama gharama mbona wao niΒ Mabilionea wakubwa tuΒ
Alipata wazo la kumtafuta Lucia ambaye alitoa wazo la Mke waΒ Desmond kuhamishwa Wodi na kupewa huduma za daraja la juuuΒ zaidi, alimpigia simu akamwambia wakutane nyuma ya HospitaliΒ hiyo mahali ambapo palikuwa na Bustani.Β
Mara moja walikutana huko, Daktari akataka kujuwa niniΒ ambacho kilikuwa kikiendelea na kwanini Lucia alitoa wazoΒ lile, ilionekana kuwa ni swali gumu sana kwa Lucia kumjibuΒ Daktari huyo akamwambiaΒ
“Ni kwasababu ni Mgonjwa wangu ndiyo maana nilitaka apeweΒ matibabu ya haraka ili kumuamsha mapema” Alijibu akiwaΒ anatazama chini lakini akili ya uzee ya Dakatari MkuuΒ ilimwambia kuwa Lucia alikuwa na jambo lingine kabisaΒ
“Unajuwa fika kuwa unaniongopea Lucia…Niambie ukweli, LuciaΒ wewe ni kama Binti yangu wa kumzaa tena hata Mjukuu wangu,Β sura yako inaonesha dhahiri kuwa unnificha jambo…nyuma yaΒ pazia kuna nini?” Aliuliza tena Daktari huyo, alimpa nafasiΒ Lucia afikirie nini cha kufanya, mwishowe aliona ni boraΒ amfungukie daktari huyo, alimwambiaΒ
“Nina mashaka Desmond akawa siyo Mtu mzuri kwa Mke wakeΒ Mandy, juzi alikuja na mwasheria akamsainisha Mgonjwa kwaΒ alama za vidole, nilipouliza nilijibiwa kuwa sipaswiΒ kuingilia masuala ya kifamilia” Alieleza LuiciaΒ
“Una uhakika?”Β
“Nina uhakika na ndiyo sababu ya kukuonba Mkuu mgonjwaΒ ahamishwe daraja”
“Lakini inafikirisha sana sijui kuna nini nyuma yake. NdiyoΒ maana nilikuja kukuuliza sababu Desmond aliwaka sana baada yaΒ kujuwa kuwa hawezi kumuona Mke wake. Hapo ndipo wasiwasiΒ wangu ulipoanza….Kaendelee na kazi Luicia tutaongeaΒ baadaye” Alisema Mkuu huyo kisha alimtazama Lucia akitokomeaΒ eneo hilo akiwa ndani ya mavazi ya kihudumuΒ
Baada ya kupita masaa kadhaa, Desmond alimuarika MwanasheriΒ Joel kwenye moja ya Baa zenye hadhi, alihitaji kumuelezaΒ kuhusiana na jinsi mambo yalivyokuwaΒ
“Kesi hii tukienda kichwa kichwa tunaweza jikuta tunafiaΒ jela…” alisema Desmond akiwa anagida unywaji, joel akaulizaΒ
“Kuna jambo jipya?”Β
“Kuhusu gari yangu niliyomuulia Sanga kutokukutwa Eneo laΒ tukio badala yake kukutwa gari nyingine kabisa ikiwa na mwiliΒ wa Sanga, tafsiri yake kuna Mtu wa tatu ambaye anaijuwa hiiΒ inshu, pili ni kuhamishwa kwa Mke wangu na kupelekwa kwenyeΒ wodi nyingine bila Mimi kupewa taarifa kisha nikazuiliwaΒ kwenda kumuona, ni ishara kuwa kuna bomu linaenda kulipuka”Β Alisema Desmond akiwa anamtazama Mwanasheria JoelΒ
“Uuuupss!! Hata mimi taarifa ya gari imenivuruga sana, huyoΒ Mtu wa tatu ni nani hasa? Na kwanini hadi leo hajapiga simuΒ wala kutoa taarifa polisi?” Aliuliza JoelΒ
“Nashindwa kuelewa, kila ninapoliwaza jambo hili naishiaΒ kukosa majibu ya kueleweka japo namtilia sana mashaka nesiΒ anayemuuguza Mke wangu, kuna bahasha amempa Mpenzi wanguΒ sijui kuna nini ndani yake napata ukichaa” Alisema DesmondΒ
“Desmond hii ni vita kubwa sana na mwisho wake hautokuwaΒ mzuri kama tunavyofikiria ni lazima tuwekeze nguvu na pesaΒ ili tumalize mizizi yote” Alisema JoelΒ
“Kesho kutwa ni siku ya kumvisha pete Noela, kama yule nesiΒ atakuja kwenye shughuli basi kila kitu kitaharibika, niΒ lazima tumzuie asije” Alisema DesmondΒ
“Hiyo kazi niachie Mimi nitahakikisha hafiki kwenye shughuliΒ lakini wewe unatakiwa kuhakikisha unamtafuta Mtu wa tatuΒ aliyeona ukiwa unamuuwa Sanga Baharini, huyo ni Mtu hatariΒ sana na huwenda anajuwa kuhusu kifo cha Mama Mandy kuwa mimiΒ na wewe ndiyo wauwaji” Alisema Joel kisha alinyanyuka,Β akachukua mkoba wake akapiga funda moja ya kinywaji akaiwekaΒ glasi kwa nguvu juu ya meza kisha akaondoka zake pale.
Jioni Lucia alimpigia simu Noela wakati huo akiwa anarejeaΒ nyumbani kwake akamuuliza kuhusu ile bahasha kama ameanzaΒ kuifanyia kazi lakini Noela alizidi kumsistizia kuwa niΒ lazima shughuli ya kuveshana pete ipite kwanza ndipo aifanyieΒ kazi, basi Lucia alikata simu akaelekea nyumbani kwao, akiwaΒ anaingia ndani aliiyona gari nyeusi ikiwa imesimama nje yaΒ nyumba yao, aliitazama lakini hakutia shaka kabisa, ndani yaΒ gari hiyo alikuwemo Mwanasheria Joel na kilichomleta paleΒ kilikuwa ni kuanza kazi ya kuhakikisha Lucia aendi kwenyeΒ hiyo shughuli, baada ya kufahamu anapoishi Lucia, MwanasheriaΒ Joel aliondoka zake.Β
Alimkuta Mama yake akiwa amelala, alikuwa mgonjwa hivyoΒ jukumu kubwa la Lucia lilikuwa ji kuhakikisha kuwa Mama yakeΒ anakuwa salama, Maisha yao yalikuwa duni na yeye ndiyeΒ tegemezi, alipitia huko chumbani na kumkuta Mama yake akiwaΒ amelala, alimfunika shuka kisha alitoka akaenda kuketiΒ sebleni.Β
Alitafakari mambo mengi sana ikiwemo alichozungumza naΒ Daktari Mkuu kisha alikumbuka alichokiweka kwenye bahashaΒ aliyompa Noela, aliweka picha ya Desmond na Mwanasheria JoelΒ kisha aliambatanisha na maelezo ya alichotaka Noela akifanye,Β alivuta pumzi zake kisha alijilaza kidogo pale pale Sebleni.Β
Usiku ulipoingia, nyumbani kwa akina Noela na Mama yakeΒ kulikuwa na shamra shamra sababu tukio la kuvishana peteΒ lilikuwa limekaribia, baadhi ya ndugu walikuwa wamefika pale,Β sura ya Noela ilizidi kunawiri kwa tabasamu bila kujuwa kuwaΒ kulikuwa na vita kubwa iliyokuwa inapiganwa chini kwa chini,Β Upande wa kule Hospitali matibabu yaliendelea kwa Mandy,Β kukawa na tumaini kidogo lakini Desmond hakuambiwa chochoteΒ kile sababu Tayari daktari Mkuu na Nesi Lucia walikuwa naΒ ajenda ya siri kuhusu uhai wa Mke wa Desmond aliyeitwa Mandy.Β
Siku iliyofuata baada ya muda wa kazi kuisha, Lucia alimuombaΒ Noela waonane mara moja, walionana mgahawani majira yaΒ Mchana, ombi la Lucia likawa lile lile lakini NoelaΒ alimsistizia kuwa hadi Shughuli ipite.Β
“Lucia ni kesho kutwa tu navishwa pete, kama nilivyokwambiaΒ sitawekeza fokasi kubwa kwenye kazi yako sababu nina shughuliΒ iache ipite kisha nitarudi kazidi na nitaanza na kazi yako”Β Alisema NoelaΒ
“Sawa Noela lakini ni muhimu sana ukafungua ile Bahasha”Β Alisitiza sana Lucia
“Sawa nitafanya hivyo kwa ajili yako, nitahakikisha unafauluΒ katika hilo jambo unalonipa kulifanya” Alisema NoelaΒ
“Umesema ni kesho kutwa ndiyo unavishwa pete, nitajitahidiΒ ili nimuone shemeji yangu….kama sikosei ulisema anaitwaΒ Joshua”Β
“Una kumbukumbu kama zamani, ndiyo anaitwa Joshua. Uje Lucia,Β ni muhimu sana” Alisema Noela, waliachana baada ya kuwaΒ wamezungumza vya kutosha. Aliporudi nyumbani Noela aliketiΒ akajiuliza ni kwanini Lucia anasistiza sana afungue hiyoΒ Bahasha.Β
Basi alielekea kwenye kisanduku chake cha kuhifahdia nyarakaΒ mbalimbali za kazi, ndimo alimohifadhi ile BahashaΒ inayotafutwa na Desmond, aliitoa kisha aliishikilia akiwaΒ ameketi chini kando ya sanduku hiloΒ
“Mmh kuna nini humu mbona Lucia anasistiza sana nifungue?”Β Alijisemea Noela ndani ya moyo wake, mwisho aliona ni boraΒ aifungue ili kuondoa ile lawama aliyokuwa akipewa na LuciaΒ kuwa anapuuzia kazi yakeΒ
Alichana kwa juu kisha karatasi zikawa zinaonekana kwa juu,Β akavuta karatasi moja lakini wakati anaivuta akaidondoshaΒ picha ya Desmond Mwanaume ambaye anamjuwa kama Joshua naΒ ndiye Mtu anayetakiwa amfwatilie na kujuwa ukweli wa mamboΒ yaliyojificha na ndiye Mwanaume anayeenda kuvishana nayeΒ pete, bahati nzuri picha iliangukia kwa kujifunika, nyumaΒ hakukuwa na maandishi yoyote yale.Β
Aliiokota picha hiyo ikiwa imejifunika vile vile, moyoΒ ulianza kumdunda hata kabla hajaona picha hiyo, alijishangaaΒ sana lakini kabla hajaigeuza Mama yake aliingia chumbaniΒ akamuona Binti yake akiwa katika hali ile ya waiswasi.Β
Alimpokonya ile bahasha na picha kisha akavirudisha kwenyeΒ ile Bahasha bila hata kuiangalia picha hiyo ya Desmond,Β akaweka Bahasha kwenye sanduku hilo alilokuwa ameliacha waziΒ kisha alilifunga.Β
“Noela huu siyo wakati wa wewe kufanya kazi, mara nyingi kaziΒ zako zinakuumiza kichwa na kukufanya ukose raha. Huna haja yaΒ kuwa katika hali hiyo cha Msingi ni kuweka akili kwenye tukioΒ la kesho kutwa la kuvishwa pete na Mwanaume unayempenda”Β Β
Alisema Mama Noela kisha alimnyanyua Mtoto wakeΒ
“Unaenda kuwa Mke wa Joshua, ni jambo ulilolipigania kwa mudaΒ mrefu hebu lipe kipaumbele, kazi zako utaendelea nazo baadaΒ ya shughuli kupita sawa?”
“Sawa Mama” alijibu Noela kisha alitoa tabasamu, laiti kamaΒ angelikuwa ameiyona ile picha basi mambo yote yangelikuwaΒ yameharibika maana angesoma kilichoandikwa na Lucia, angekutaΒ siri ya jina la Desmond kisha tuhuma nzito.Β
“Haya twende” Alisema Mama Noela kisha alitoka na Binti yakeΒ lakini akili ya Noela ilijikuta ikianza kuwaza ile Bahasha yaΒ Lucia.Β
Naaam!! Desmond hakupotea Hospitalini sababu alijuwa fikaΒ kuwa kwa huduma anazopewa Mke wake anaweza akaamka mudaΒ wowote hivyo alihitaji kummaliza japo alizuiliwa kumuona,Β alimtafuta Nesi Lucia akamwambia anahitaji kumuona Mke wake.Β
“Lucia mnanitendea vibaya sana kwa kutoniruhusu nimuone MkeΒ wangu, wewe unajuwa ni jinsi gani nampenda Mke wangu naΒ nimekuwa hapa kila siku kuhakikisha afya ya Mke wangu inakaaΒ sawa” Alisema Desmond wakiwa wamesimama, hakujuwa kama LuciaΒ tayari alimuhisi vibayaΒ
“Sasa kipi bora Desmond, umuone Mke wako kila siku akiwaΒ katika hali ileile au usimuone ili afya yake ikae sawa ndaniΒ ya muda mfupi? kumbuka Mkeo amekuwa hapa kwa zaidi ya mieziΒ mitano, hadhi ya maisha yenu hakupaswa kuwa kwenye ile wodiΒ wewe hukulioma hilo?” Alisema Lucia huku kila mmoja waoΒ akipigana vita ndani kwa ndani, Desmond alipokuwa akimtazamaΒ Lucia alikuwa akijiambia kuwa lucia ndiye Mtu wa tatuΒ anayejuwa kila kitu huku Lucia akijisemea ndani ya moyo wakeΒ kuwa ukweli utajulikana DesmondΒ
“Hilo ni sawa lakini kwanini maamuzi haya yamekuja ghafla tuΒ tena bila kunishirikisha Mimi? Hamjui ni kiasi gani nimeumiaΒ mimi Lucia, nampenda Mke wangu Mandy” alisema Desmond akiwaΒ anatokwa na mchoziΒ
“Huna sababu ya kulia Desmond, ungekuwa unampenda Mke wakoΒ usingemsainisha hati ya Makabidhiano ya Mali ukiwa naΒ Mwanasheria” Alisema Lucia, Desmond akashtuka sasa kuwa LuciaΒ ndiye aliyetoa hilo wazo la kuhamishwa kwa Mke wake baada yaΒ ile siku kumsainisha Mandy mbele yakeΒ
“Anhaaa kwahiyo wewe ndiye uliyetoa wazo la Mke wanguΒ kuhamishwa?” aliuliza Desmond akiwa anafuta chozi kishaΒ aliweka tabasamu la kikatili, ile hali ya majonzi aliiondoaΒ baada ya kugundua kuwa anaongea na Mtu ambaye alikuwaΒ ameushtukia mchezo mzima.Β
“Lucia hukupaswa kujiingiza huku kabisa kwasababu hujuiΒ ilianzaje wala inaenda kuishaje, umefanya kosa kubwa litakaloΒ
kugharimu. Mama yako ni Mgonjwa, ni bora uweke Mawazo yoteΒ kwa Mama yako kuliko kuweka kwa Mtu ambaye atakujaΒ kukugharimu” Alisema Desmond kwa sauti iliyokaza yenyeΒ kumaanisha, Lucia alicheka chini chini kisha akamwambiaΒ DesmondΒ
“Mwanzo nilikuwa nikikupenda sababu niliamini una mapenziΒ mazito sana kwa Mke wako lakini baadaye nilikuchukia baada yaΒ kugundua kuwa wewe ni miongoni mwa waliosababisha yeye akawaΒ pale, nakuhakikishia Desmond, igizo unalofanya ukweliΒ utajulikana Mkeo akiamka” Alisema Lucia kisha alianzaΒ kuondoka lakini Desmond alimshika mkono akamwambiaΒ
“Una masaa 24 ya kutoka katika hili Lucia, Uwe na siku njema”Β Alisema Desmond kisha kila mmoja alielekea alipopakusudia,Β lakini Maneno aliyoyazungumza Lucia yalimtia ukichaa sanaΒ Desmond akiwa kwenye gari aliwasiliana na Joel akamwambiaΒ Wamuuwe Lucia kabla ya tukio la kuvishwa pete kwa Noela.Β
Siku hiyo Lucia alizidi kuchanganikiwa sana, aliporudiΒ nyumbani kwao alichukua simu yake ambayo wakati anaongea naΒ Desmond alimrekodi ili aweze kuongeza ushahidi wa kumpaΒ Noela, alimtumia sauti hiyo ya mazungumzo Noela kishaΒ akampigia simu ili amuelekeze lakini Noela hakupokea simu,Β maandalizi ya Tukio la kuvishwa pete yalikuwa yamepamba motoΒ sana hivyo hakuwa na muda wa kukaa na simu.Β
Siku hiyo iliisha, siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku yaΒ kuvishwa pete kwa Noela, maandalizi yote yalifanyika paleΒ pale nyumbani kwao sababu hawakutaka Watu wengi, gharama zoteΒ alizifanya Desmond. Usiku wa tukio Lucia alijiandaa, akamuagaΒ Mama yake akamwambiaΒ
“Mama naenda kwenye sherehe ya rafiki yangu, sitochelewaΒ kurudi. Nakupenda sana Mama yangu” AlisemaΒ
“Nakupenda pia Binti yangu, usijali nenda Mama nitakuwaΒ salama. ” alisema Mama yake Lucia, waliagana hapo kisha LuciaΒ alitoka. Alisimama Nje akimsubiria Mtu wa PikipikiΒ aliyewasiliana naye kuwa aende kumchukua hapo na kumpelekaΒ nyumbani kwa akina Noela, alisimama kwa muda mrefu nje,Β alipoona muda unazidi kwenda alianza kutembea taratibu iliΒ kama atakutana na Pikipiki aitumie, Ulikuwa ni usiku wa saaΒ mbili, baadaye likaja gari moja na kusimama mbele yake, LuciaΒ alijiuliza ni nani aliyesimama mbele yake.Β
Kioo kilishushwa akaonekana Mwanaume mmojaΒ
“Samahani Dada unaenda wapi?” Aliuliza huyo Mwanaume
“Naenda mahali kwani vipi?” aliuliza Lucia maana alikuwaΒ amechukia kwasababu bodaboda wake alikuwa amendanganya kuwaΒ hayupo mbali kumbe yupo mbaliΒ
“Sio vema Mtoto wa kike akatembea kwa mguu usiku huu,Β naelekea barabara ya sita sijui wewe” Alisema Mwanaume huyo,Β Lucia alifikiria akaona ajishushe tu kwa huyo Mwanaume maanaΒ yeye alikuwa akielekea Barabara ya nne.Β
“Naelekea Barabara ya Nne” Alijibu LuciaΒ
“Basi twende nikusindikize” Alisema Mwanaume huyo, LuciaΒ aliingia kwenye gari, safari ilianza kuelekea nyumbani kwaoΒ Noela, wakiwa Barabarani mwanaume huyo alionekana kumtongozaΒ Lucia lakini Lucia hakuonekana kumkubali kisha alimwambiaΒ
“Kama umenipa msaada ili unitongoze naomba unishushe MimiΒ siyo Mwanamke wa hivyo” Alisema Lucia akionekana kuchukizwa..Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NANE
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & PainΒ
Β Β
6 Comments
Aaashhhhh haitosh admin ongeza kidog jaman nataka kujuwa tu Lucia Alicia au hakufikaaaπͺπππ
Mhh uyo anae mtongoza asije akawa muuwaji mhhππ
Joel huyooo
Mh iyo gari iyoπ₯Ίπ₯Ίπ₯
Kaz ipo
Mmmh
Mambo yamepamba π₯ na yanaenda kuwa sio mambo tena bali ni balaa π₯π₯
Asante Mwandishi kwa niaba ya Admini kwa Simulizi yenye mafunzo na mazingatio makubwa
More Love from Kenya β€οΈ