Ilipoishia “Hapo hapo akapiga simu moja kule Mbudya kua ameshammaliza Rais Mbelwa, mwili wake ukavutwa hadi eneo la chini ambako alikua akitesa na Kuuwa Watu, huku ndiko alikomfungia Mke wake kama mateka. Sasa mpango ulio mbele ni kuhakikisha anapatikana Elizabeth, Nchi ikawa chini ya Waziri Mkuu ambaye baada ya Kifo cha Rais Mbelwa alielekea ikulu na kuanza kutoa Maagizo ya nini kifanyike. Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINI
Mchaka Mchaka, ndege tunduni.
Helkopta sita zilizotoka Black site ziliwasili mpakani mwa Kiluvya na Picha ya ndege tayari kuanza Msako wa kumpata Elizabeth. Wakashushwa makomandoo arobaini na tano kutoka Black Site, nguvu kazi ikawa kuwasaka Mzee Kimaro na Elizabeth ambao walikua wakikata nyika baada ya kuchomoka pangoni.
Hali ya Uzee ya Mzee Kimaro ilianza kuifanya safari ya kukimbia iwe ngumu, aliishiwa nguvu lakini Elizabeth alimsaidia ili watafute Mahali wajifiche, nyuma yao wanajeshi na Makomandoo walikua wakizidi kuwaandama
โElizabeth, niache hapa Mama. Wewe okoa Maisha yako, Mimi siwezi kusonga mbeleโ alisema Mzee Kimaro akiwa ameanguka Chini, juu Helkopa ilikua ikisogea eneo hilo ambalo lilikua giza, lakini kadili Chopa ilivyozidi kusogea ndivyo mwanga ulivyozidi kuongezeka
โSiwezi kukuacha Mzee Kimaro, huwezi kufia hapaโ alisema Elizabeth akijitahidi kumwinua lakini Mzee Kimaro alikua tayari ameshakata tamaa ya kwenda mbele, Elizabeth alipoangalia nyuma aliona namna wanajeshi walivyozidi kusogea, akajitahidi tena kumnyanyua lakini tayari Helkopta ilikua juu ikiwamulika taa, wakawa wameonekana.
Ikabidi amfiche mzee Kimaro nyuma ya Jiwe, naye akajibanza lakini tayari taarifa ilishasambaa kwa Wanajeshi walio chini kua Elizabeth alikua mita chache kutoka wao walipo, njia pekee ya kujiokoa hapo ilikua ni kuhakikisha ananzisha Ambushi vinginevyo watanaswa kirahisi sana.
โUsipoteze muda na nguvu zako, kimbia uende mbaliโ Mzee Kimaro alizidi kuongea, sauti ya chopa ikawafanya washindwe kusikilizana, mara mashambulizi kutoka juu ya Helkopta yalianza, Elizabeth hakukaa kimya alijibu Mashambulizi hayo akisaidiwa na Mzee Kimaro
Waliishambulia Helkopta bila mafanikio, huku Mashambulizi ya chini kutoka kwa wale Wanajeshi yalikua yakianza, risasi walizobakiwa nazo zilikua chache mno, isingelikua rahisi kwao kuendelea na mapambano, Mzee Kimaro akachana shati lake jeupe na kulitundika kwenye kipande cha Mti kisha akanyoosha juu kua wanajisalimisha, wazo hili halikumfurahisha sana Elizabeth
โUnafanya nini Mzee?โ alihamaki lakini Mzee Kimaro alimpa ishara ya Kichwa kuwa kama wataendelea na vita basi watafia hapo kama kuku kutokana na uchache wao pia risasi ziliwaishia, chozi lilimbubujika Elizabeth Mlacha, aliangusha kilio cha nguvu huku ile Chopa ikiwa ipo juu yao, eneo zima likawa mwanga, wanajeshi na Makomandoo walio chini wakalizingira eneo lote huku walio juu ya Helkopta wakiwasiliana na walio chini kua ni
kweli walijisalimisha.
Roho ya Elizabeth ilifukuta kwa maumivu Makali sana, hapo alipaswa kufanya kazi mbili, moja ni kumwokoa MUHONZI Kutoka mikononi mwa mwenyekiti wa chama cha Upinzani na pili alipaswa kutoisalimisha ile flash Muhimu aliyoificha kwenye chupi yake.
Dakika Moja walizungukwa kila upande โMikono juuโ ilisema sauti komavu iliyojaa hasira, ilikua ni sauti ya Brigedia Antony, kila upande walizungukwa na kikosi kazi, Hatimaye Elizabeth aliamini ameshafikia mwisho baada ya siku Tatu za Hekaheka nzito. MWISHO WA SEASON TWO
Usikose Season 3, ya mwisho kabisa. Kujua kama Elizabeth alipona kwenye Msala huu
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
14 Comments
Dah ni ya โค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅ Tunaomba sizio 3 kwa hamu u
Admin unatuma short story hata raha huna ..sku ingine unapitiliza siku mzimaaa ..kama unatangaza๐ฆฅ๐ mpira bas achia story af ndo uende kwneye mpiraaaaaa…..๐ฉ๐ฉ๐ฉ๐ฉ๐ฎ๐ฎ๐ฎ๐ฎ๐ฎ๐ฎ๐ฎ
๐๐
๐คฃEliza atapona jeshi la msituni linakuja hapooo likiongozwa na malkia na mkuu wa majeshi Sokwe๐คฃPia Na Waziri wa Ulinzi Benjamin Chauwoga๐
Una mawazo makaliii ww ๐๐
Popo lazima waje kwaajili ya kumuokoa ๐๐๐. Mtunzi umetisha kweli ๐
Well done.. umecheza kama Pele lakini unatukata stim kafupi sana
Well done …ila fupi sana admn unakata stm
Ningekuwa Director ningeomba kufanya filamu Kwa huu mzigo MSALA all in all hadithi ni tamu balaaaaa
Adimni ntakuloga ๐๐๐
Lovely
Aiii ,simulizi ya kisisimua n kana nachek movie tena zaid ya..๐
Huu utunzi director fanya mpango wa bongo movie kaliii… usanii upo ๐ฅ๐ฅ
๐ค
Story hatar ila inachelewa adi unaenda kupoteza ladha sasa