Ilipoishia “Muhonzi akafanikiwa kukata kamba alivyofungwa, giza lilikua nene ndani ya Chumbaย alichohifadhiwa, akajaribu kuchungulia dirishani kwa mtindo wa kuruka sababu dirishaย lilikua juu sana lakini hakuambulia kuona chochote kile, akajaribu kuitaย
โKuna nani hapo nahitaji Majiโ aliita kwa makusudi huku akifahamu fika kua eneo hilo linaย ulinzi mkali kuhakikisha yeye hachomoki, akaita tena, ndipo aliposikia hatua za kiatu zikijaย upande wake, akarudi haraka kuketi sakafuni alipokua ameketi.ย
Mara taa ikiwashwa, kisha akatupiwa maji aliyoyataka. Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
โNitakunywaje sasa na umenifunga kamba?โ akauliza Muhonzi kwa ujanja huku akiwa tayariย ameshakata ile kamba, yule Mlinzi akamtazama sana Muhonziย
โNi kweli sasa nitakunywaje nina kiu sana Aaaaaahhhโ akazidi kusema Muhonzi hukuย akijibaraguza kama Mtu aliyefungwa mikono yake, yule Mlinzi ikamlazimu kufungua sasaย mlango wote kisha akaingia ndani ya chumba hicho, ndicho alichokua anakitaka Muhonzi.ย
Akaoneshwa Bunduki, kisha akaambiwaย
โHuwezi kufanya ujanja wowote, nitakupa majiโ alisema yule Mlinzi, akaiokota chupa yaย maji kisha akaifungua na kumsogezea Muhonzi ili amyweshe, hakujua kua alikuaย ameshafanya kosa kubwa sana, pale pale Muhonzi akamtandika ngumi nzito ya pua,ย
akamfwata kwa haraka na kumvunja shingo. Akaiyokota ile Bunduki kisha akaanza kutafutaย njia ya kutoka ndani ya Godauni.ย
Akatembea kwa taratibu kwa mahesabu mazito sana ili asije rudi mikononi mwa Zagamba,ย akasikia sauti ya TV, akajua fika kua Walinzi wengine walikua huko. Akasogea hadi eneoย hilo na kuwakuta walinzi wakiwa wanakunywa pombe na kuvuta sigara.ย
Hakutaka kusema nao, akatafuta kona nzuri akapita ili alifikie lango kuu la kutoka ndani yaย Godauni hiyo iliyojaa giza zito. Taratibu sana Muhonzi akalisukuma lango kisha akatoka njeย ya Godauni, muda ulivyozidi kwenda ndivyo ambavyo wale Walinzi walivyoshtuka baada yaย kuona mwenzao harudi, akatumwa mmoja wao kwenda kuangalia, akamkuta akiwaย ameshakufa. Msako wa kutafutwa kwa Muhonzi ukaaanza ndani ya lile Godauni, walipokujaย kugundua kua alishatoka ndani ya Godauni tayari Muhonzi alikua ameshafika mbali kabisa.ย
**ย
Baada ya kuchomoka mikononi mwa Watu wa Zagamba, akakimbilia kwenye jumba la siriย ambalo alikua akilitumia kufanyia kazi zake, kichwa chake kikiwa kinawaka moto kwanzaย alihitaji kujisafisha mwili mzima baada ya kukaa godauni kwa siku kadhaa.ย
Maji ya Baridi yakakubali kuuufanyia Utakaso wa kutosha mwili wa Muhonzi, akili ilipokaaย sawa akawa tayari kujua ni wapi alipo Elizabeth, bado aliamini kuwa alikua hai. Jambo laย kwanza alilolifanya baada ya kuketi na kuwasha mitambo yake ni kuanza kusaka mara yaย mwisho simu ya Elizabeth ilizimwa wapi.ย
โPicha ya Ndegeโ ndiyo sehemu pekee ambayo simu ya Elizabeth ilizimwa kwa mara yaย mwisho, aina ya simu aliyoitumia ilionekana lakini uzuri simu hiyo bado ilikua Hewani,ย Usiku ulikua mwingi, akajipumzisha kwanza Kitandani ili akiamka aendelee na upekuziย wake kwa njia ya Mtandao, masuala hayo ndiyo yaliyokoleza ukaribu wake na Elizabethย Mlacha.ย
**ย
Saa 3 Asubuhi, Tanzaniaย
Muuwaji wa kuaminika alikua akipata chai ya asubuhi sehemu fulani ya Tanzania, safariย yake ya Usiku mzima ilikomea kwenye moja ya Hoteli, alipumzika hapo ili afanye safari yaย kuelekea eneo nyeti la Black Site.ย
Baada ya kumaliza, aliingia kwenye gari kisha akaendelea na safari yake ya Masaa matatuย baada ya Chai, sasa aliushika Msitu mmoja, akaisweka gari eneo fulani, akachukua begi lakeย na kupandisha kilima kimoja. Alionekana ni Mtu anayejua anachokifanya, kazi aliyopewa naย Waziri Mkuu ni kuhakikisha anamchukua Elizabeth kutoka Mikononi mwa Walinzi wa Balckย Site.ย
Begi alilolibeba lilikua na silaha moja ya masafa marefu pamoja na Darubini, aliketi juu yaย kilele cha kilima hicho, huku macho yake akiyaelekeza eneo la umbali wa Kilomita Nane,ย hapo ndipo ilipo Black Site.
Akatoa Ramani ya jengo la Black Site, ramani hiyo ilichukuliwa Ikulu baada ya Waziri Mkuuย kuikamata Ikulu, muuwaji akatabasamu. Kisha akalala usawa mzuri na kuiweka Bunduki yaย Masafa marefu vizuri, akachukua Darubini na kuanza kulikagua jengo hilo kwa uzuri.ย
Akajifunika kofia nyeusi, kisha akairejesha Darubini ndani ya Begi, akaanza kuitumiaย Darubini iliyo kwenye Bunduki yake, macho na hisia zake akayaelekeza ilipo Black Site,ย eneo alilolala alikua akilitazama jengo hilo lenye vioo kwa uzuri sana.ย
Aliona na kuhesabu idadi ya Walinzi walio ndani ya Jengo ambao ni Makomandoo waย kuaminika aliokua akiwatumia Rais Lucas Mbelwa, alihitaji kuwamaliza kwanza. Ndani yaย jengo palikua na zaidi ya Makomandoo hamsini. Wote aliwapigia mahesabu, kisha akaikunjaย Bunduki yake na kuizamisha ndani ya Begi, akarudi chini ya Kilima na kuanza kutembeaย kwa kutumia barabara ya vumbi iliyokua ikielekea Black Site.ย
Muuwaji huyo, alipokaribia aligundua kwa haraka uwepo wa ulinzi maalum wa Nyayaย nyembamba za Umeme ambazo ndizo zilizokua zikilinda eneo hilo, alishajiandaa sababu siriย za ulinzi wa ndani na nje ya Jengo alikua amezipata.ย
Akachomoa kifaa kidogo chenye mfanano na Simu, kisha akauzima umeme huo ndani yaย sekunde ishiri akawa amezivuka nyaya hizo. Taratibu akakimbia na kujificha nyuma ya ukutaย wa jengo la Black Site, kuhusu idadi ya walinzi wa ndani ya Jengo hakua na wasiwasi naoย sababu alishawapigia mahesabu makali sana.ย
Akasimama hapo kwa mahesabu mazito, kisha akachungulia, jengo hilo lililokua na viooย vingi ambavyo vingefanya urahisi wa Muuwaji kujulikana kua amefika, akapiga hatua zaย haraka na kuuwahi ukuta wa pili, akajificha kisha akatoa kamba kutoka ndani ya Begi lake,ย akairusha kamba kuelekea juu, iliponasa akawa na zoezi moja tu la kuifuata paa ya jengoย hilo.ย
Kisha taratibu akatembea juu ya paa la jengo huku akiwa anapiga mahesabu yake vizuri,ย alikua na ramani nzima ya jengo hilo la Black Site, ilikua rahisi kwake kujua ni wapi atawekaย kambi hapo juu ya paa ya Jengo, akafika mahali ambapo palikua na pambo kubwa la saa,ย eneo hilo lilikua karibu na mlango Mkuu wa Kuingia ndani ya Jengo hilo, kando ya jengoย ndimo walimokua wakikaa makomandoo.ย
Kwake hao ndiyo kikwazo kikubwa kufanikisha kazi ya Kumchukua Elizabeth, akaiwekaย vizuri kofia yake kisha akalala kwa ustadi mzuri huku akilitazama jengo ambaloย Makomandoo walikua wakipatikana.ย
Akaishusha Bunduki yake ya Masafa marefu kutoka ndani ya Begi lake kisha, akaitega vizuriย kuelekea kwenye jengo, kichwani alikua na ramani yote. Kitu pekee alichohitaji kukifanyaย hapo ni kuufunga mlango wa Umeme ambao ndio uliokua ukitumika na Makomandoo hao,ย mwendo wa dakika ishirini awe tayari ameshamchukua Mateka wake kwani kupambana naย Makomandoo hao haikua kazi rahisi kwake.ย
Akafunga kiwambo cha kuzuia sauti, kisha akalenga kitasa cha Umeme ambachoย kingemfanya atenganishe kati ya Makomandoo na Walinzi wa kawaida wa Black Site,ย umbali wa jengo hilo ni zaidi ya Mita sabini.
Dakika moja na nusu ilimtosha kujihakikishia kua risasi atakayoiachia hapo itaenda kukataย mawasiliano ya jengo la Makomandoo na jengo la Black Site. Akavuta hewa nyingi kishaย akaiachia taratibu na kukaza mikono yake kisha kidole kikafanya kazi ya kusukuma risasiย ย
Haraka Alam ikalia kuashilia kua palikua na hitilafu mlangoni, hii ni baada ya Muuwaji huyuย kukita risasi mlangoni. Haraka walinzi wa Black site pamoja na Makomandoo walio ndani yaย jengo lililopigwa risasi wakawa kwenye taharuki nzito, akasubiria kwa sekunde kadhaa iliย Mlango wa Black Site ufunguliwe, alipousikua umefunguliwa akajirusha mithiri ya Nyaniย mzeeย
Akatua chini kama Buibui, haraka akaachia pigo takatifu la Risasi za mahesabu naย kusambaratisha walinzi watatu waliokua eneo la Mlango kisha akaingia ndani ya Jengo hilo.ย
Elizabeth aliposikia Alam ikilia kuashiria kuna tatizo alishaanza kuhisi ujio wa Mtu mbayaย ndani ya Jengo la Black Site, japo alikua amechoka sana lakini akaweza kumwambia Mlinziย kua amfungue kwani eneo hilo siyo salama kabisaย
โUsipofanya hivyo Utakufaโ akakazia Elizabeth huku akijitingisha kwa nguvu chacheย alizobakiwa nazo, yule Mlinzi hakutaka kumwelewa Elizabeth hadi pale aliposikia risasiย ikisikika karibu na Mlango wa chumba cha Mateso ambacho Elizabeth alikua amehifadhiwa.ย
โNifungue tafadhaliโ alisema Elizabeth, lakini akili ya yule Mlinzi ikajikuta imezubaaย kidogo, ghafla akapigwa risasi ya Kichwa, kisha Mlango ukafunguliwa, akaingia Muuwaji,ย akamtazama Elizabeth kisha akatoa tabasamu la kufanikisha kazi yake.ย
Hakutaka kupoteza muda akamzimisha kwa kumchoma sindano ya Usingizi, akamfungua naย kumweka begani, maiti za Walinzi zilikua za kutosha sakafuni, akatoka hadi nje ya Jengo laย Black Site wakati huo Makomandoo wakiwa wanahangaika namna ya kufungua ule Mlangoย wa Umeme ambao kwa kawaida hufunguka baada ya dakika ishirini endapo utapata Hitilafu.ย
Akauvuka uzio wa Umeme kisha akaanza kuzikata Kilomita kuelekea lilipo gari lake aanzeย safari ya kurejea Ikulu, mara zote alikua akiitazama saa yake kwa maana zikitimia dakikaย ishirini wale Makomandoo watatoka ndani ya jengo na kuanza kumsaka kila kona. Akaianzaย riadha baada ya kugundua kua alikua amebakisha dakika tatu kumalizika kwa ule mudaย aliokua ameupangilia kulifanya tukio la kuvamia Black Site.ย
Ndani ya jengo tayari makomandoo walishajiandaa kutoka huku wakisubiria muda muafakaย ambao Mlango huo wa umeme utakapokua umefunguka, Muuwaji alikua akikimbia naย Elizabeth aliyepoteza fahamu, akapandisha kilima kidogo lakini kwa Bahati mbaya akaterezaย na kujikuta akimtupa Elizabeth ambaye akavingirika na kutumbukia kwenye korongo, kwaย Bahati nzuri akanasa kwenye Mti.ย
โShit!!โ akasema Muuwaji, akaanza harakati za kutaka kumtoa Elizabeth, lakini kelele zaย Makomandoo zikasikika, akatazama saa yake na kuona tayari muda ulikuwa umekwisha naย tayari Makomandoo walikua wakija kwa kasi mahali ambapo Muuwaji alikua amesimama.ย
Kwanza akatafuta mahali na kujificha ili Makomandoo wasiweze kumwona, akaangalia risasiย zilizopo kwenye Bastola yake, kisha haraka akaenda mbali na eneo lile, akauzunguka mlimaย mmoja na kwenda kujificha huko kisha haraka akaitoa Bunduki yake kutoka ndani ya Begi.
Akaielekeza eneo ambalo Elizabeth alikua ametumbukia, alikua akihema kutokana naย kukimbia kwa muda mrefu, Makomandoo wakalipita lile eneo kisha walipofika mbeleย walitawanyika ili kumsaka kwa uzuri adui yao baada ya kugundua adui yao hakuitumiaย Barabara ya vumbi bali alizama Msituni.ย
Muuwaji akautumia Mwanya huo kuuzunguka Mlima mdogo na kisha kutokea nyuma yaย Makomandoo kisha akapiganisha akili namna ambavyo anaweza kumchukua Elizabethย kutoka juu ya Mti ulio korongoni, mara akasikia mlio wa gari ukija kutokea Upande wa kuliaย ambapo ndiyo palikua na njia ya kutoka Black Site, haraka akajitupa Korongoni na kutuaย kwenye ule Mti ambao Elizabeth alinasia kisha kwa haraka akamsomba na kushuka nayeย chini ambako palikua Na Msitu wa kutosha.ย
Akajipigiza bega kwenye jiwe, kila mmoja akatua upande wake lakini hakuna Hataย Komandoo mmoja aliyeshtuka kua Adui yao alikua Korongoni, wenge zito likamzongaย Muuwaji akiwa anajitafuta, akayaruhusu macho yake kutulia, akamwona Elizabeth akiwaย mita kadhaa kutoka alipo yeye.ย
โAgggghhhโ akagugumia kwa maumivu makali huku akinyoosha bega lake, lililo jaa damu,ย kisha akajisomba na kumsogelea Elizabeth. Akasimama na kuvuta hewa ya kujituliza vyemaย halafu akaangaza juuย
Jua lilikua likiwaka, ndege wa Msituni walikua wakipiga kelele za hapa na pale, Purukushaniย eneo la juu zilikua za kutosha kisha akajishika kiuno chake na kujinyoosha vyema, hakuishiaย hapo akachana tisheti lake na kujifunga eneo la Bega, kisha akiwa amebakiwa na vest nyeusiย akajitwika Elizabeth, akaanza kuisaka njia ndani ya Msitu wenye giza.ย
Haikua rahisi kwake kujua alikua akielekea upande upi kwasababu alikua ameshapotezaย mwelekeo sahihi, akajikuta akisambaa Msituni kwa muda mrefu hadi pale Helkopta za Blackย site zilipoanza Msako kila kona ya Msitu.ย
**ย
Kelele za popo na sokwe zilianza kusikika ndani ya Msitu wa Magoroto, hatua kubwa zaย vishindo zilimfanya Benjamin Kingai aliye ndani ya pango atoke, kwanza alikutana naย Zandawe akiwa amevaa nguo za ngozi za wanyama. Pili alikua ameongozana na kundiย kubwa la Popo waliozingira eneo la juu ili kumpa kinvuli.ย
Tatu, alikua ameshikilia Mkuki aliouchomeka chini, vyote hivi vikamfanya Benjaminย ashangae, lakini tabasamu la kuchanua lilikua likiongezeka kwenye sura ya Malkia Zandawe.ย Taratibu Benjamin alisogea karibu na Zandawe na kumuuliza kwa utaratibuย
โKuna nini?โ alihoji kwa sauti ya chini ili adokezwe lakini Malkia Zandawe akajibu kwaย sauti.ย
โLeo ni siku ya Ukombozi Benjamin, siku ambayo unaenda kurudisha kila ulichokipotezaโย alisema kisha alikaa kimya, akamfanya Benjamin atupe swali jingineย
โUnamaanisha nini kusema kila nilichokipoteza?โ akauliza Benjamin Kingai, kisha akamezaย funda zito la mate huku kivuli cha wale popo ambao ndiyo jeshi la kuaminika la Malkiaย
Zandawe likiwa linamsaidia pia Benjamin kuikimbia mionzi ya jua ambayo ilianza kuaย Mikali.ย
โUmepoteza familia, umepoteza haki ya kuishi ndani ya Nchi yako, pia Mtoto na Mpenziย wako.โ Benjamin akatoa tabasamu lenye Maswali mengiย
โUnamaanisha……โ kabla hajamaliza kusema alikuja ndege mpelelezi wa Zandawe kishaย akatua chini na kusema kwa Lugha ya ndege kisha Zandawe akamjibu Benjaminย
โEneo uliloteswa imevamiwaโ alisema Kama vile Mtu aliyejua haswa anachosema, taarifaย zote alipewa na ndege wake mpelelezi, hii ilimshtua sana Benjamin akajawa na taharukiย
โVipi kuhusu Mtoto na….โย
โMpenzi wakoโ akadakika Zandawe kisha akasemaย
โInatupasa kwenda sasa hivi huko kujua kinagaubaga, huo uvamizi hatuna hakika unafanywaย kwa lengo gani, lakini yupo Msichana aliyetoroshwa hukoโ alisema Malikia Zandawe kishaย alisubiria jibu la Benjamin, kabla hajajibu chochote Benjamin akamtazama yule ndege kishaย akainama na kumwambia ndege huyoย
โAhsanteโ aliposimama akamuuliza Malikia Zandaweย
โTunafikaje huko?โย
Malikia Zandawe akatabasamu kisha akamjibu kwa kumwambia nifuate, aliposema alikuaย tayari amegeuka na kuanza kutembea huku wale Popo wakimfuata kwa juu, akamsogeza hadiย eneo la wazi ambalo lilikua halina Miti kabisa ila lilizungukwa na Msitu mkubwa waย Magoroto.ย
Katikati ya eneo hilo palikua na kitu kilichofunikwa Majani mengi makavu, Malkia Zandaweย akasogea hadi hapo kisha akaanza kuondoa yale Majani yaliyokuaa yamerundikana,ย Benjamin alipata Mshangao mkubwa baada ya kuona Helkopta ikiwa ndiyo iliyokuaย imefunikwa hapo.ย
Pale pale kabla hata hajamaliza kushangaa akaletwa Mtu mmoja aliyefungwa mdomo wake kwa kitambaa, aliletwa na Sokwe Mkubwa ambaye ni rafiki wa Malkia Zandawe, Mtu huyoย alikua na mavazi ya Urubani, alionekana wazi kua ndiye aliyekua rubani wa Helkopta hiyo.ย
โNitakuacha Huru ukinifikisha nitakapoโ alisema Malkia Zandawe kisha akamtoa kitambaaย eneo la Mdomo.ย ย
โSiyo Mtu mbaya, ila mmenifanya nimekua Mbaya kwasababu hamtaki kuuheshimu naย kufuata Misingi na mila za Msitu huuโ alisema Malikia Zandaweย
โNaomba tafadhali, mateso niliyopata yametosha kua funzo kwangu, naomba niendeย nitawaeleze ukweli kuhusu huu Msitu, naamani hakuna mwingine atakayetia mguu kwenyeย huu Msitu.โ Alisema yule rubani huku chozi likimbubujika, Malkia Zandawe akainama naย kumwambia
โNimeshakwambia kua sina ubaya na wewe, hamkutaka kusikiliza onyo langu, ukawe chanzoย cha wengine kuupa heshima huu Msituโ Alisema kisha aliposimama akamwambiaย
โNaamini hili litakua funzo kubwa kwenu, sikutaka kukuuwa kwa maana nilikua na Uwezoย wa kukufanyia ubaya kama niliowafanyia wengine walioingia ndani ya Msitu bila kufuataย utaratibu. Kuna viumbe vinaishi humu, vinahitaji utulivu n amani kama ambavyo nyinyi kilaย siku mnapiganiaโ alisema Malikia Zandawe, kidogo akaanza kulengwa na Mchozi.ย
Benjamin akamsogelea Malkia Zandawe na kumtuliza kwa kumshika bega, hata yule rubaniย wa Helkopta ya Kijeshi aliona wazi kua Binti huyo alikua akizungumza kwa hisia kali iliyomuumiza. Malkia Zandawe akafuta chozi lake kisha akamwambia ndege wake mweupeย aongoze njia, akamtaka na Benjamin aingie ndani ya Helkopta hiyo pamoja na sokwe wakeย ampendaye.ย
Kitendo cha ndege kuruka kiliwafanya na Popo kuzama Msituni zaidi kwa kukimbia kwaย spidi kali kisha Benjamin, rubani, Malkia Zandawe na Sokwe wakaingia ndani ya Helkoptaย hiyo tayari kuelekea ndani ya Black Site kuikomboa familia ya Benjamin Kingai. Dakikaย tano baadaye Helkopta ikawa angani ikimfuata ndege mkubwa mpelelezi aitwaye Gola.ย
Nini kitaendelea?ย
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
9 Comments
Hatareee, mambo ni ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
nice sasa kwel ubaya ubwela , ila prime minister๐๐
Wooow mambo yanzd kuwa mambo๐ฅ๐ฅ
Tuwekee na sehemu inayofata ya 27 leo saa 3 ๐
Konki
๐๐
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Admin kazi nzuri ๐๐
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ