Ilipoishia “Muhonzi, kuna dili lakini ni dili la kifo, narudi Dar Mchana wa leoā alisema Elizabeth kwa kujiamini kabisa mara baada ya simu kupokelewa, kisha akaikata bila kusikiliza upande wa pili kwaniĀ Aliiona harufu ya Utajiri.
Mishale ya saa tano ilimkuta akiwa anamaliza kuweka nguo zake ndani ya Begi lake kubwa lenye Matairi, akalikokota akiwa anafunga zipu ya begi, akalivusha mlangoni kisha kwa haraka akashuka kwa kutumia lifti kuelekea chini, kichwa chake kilikua kinawaza kitita cha pesa atakachovuna, alijiamini anaweza kufanya kazi hiyo kwa mafanikio
EndeleaĀ
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Akiwa ndani ya Tax tayari safari ya kuelekea Uwanja wa ndege imeanza alijikuta akipata mashaka juu ya safari yake hiyo, haikua rahisi kumwamini Mtu aliyezungumza naye tu kwa njia ya simu, kazi yake ya Ujasusi wa siri ilimtengenezea maadui wengi.
Akaiacha Mwanza akiwa ndani ya ndege, kitu cha kwanza kufanya ndani ya ndege ilikua ni kuandika kila alichofikiria kuhusu Mtu aliyezungumza naye muda mchache uliopita, kisha akayaruhusu Macho yake kuuangalia ubunifu wa Mungu namna alivyoiumba anga nzuri inayovutia Mawingu mazito yalikua yametanda mfano wa Barafu, tayari ndege ilikua imeshaliacha anga la Mwanza.
Iliwachukua takribani zaidi ya dakika sitini kuanza kuona mandhari nzuri ya kupendeza wakati ndege ilipokua ikishuka kutoka anga ya juu.
Hali ya ukijani ulioiva ilimfanya anene kwa sauti kuu
Ā āMungu ameipendelea Tanzaniaā aliachia na tabasamu huku ndege ikizidi kushuka, sauti ya kuwataka wafunge mikanda yao iliposikika ilikua ni ishara kuwa ndege ilikua ikijiandaa kugusa Ardhi ya Jiji la Dar-es-salaam.
Elizabeth aliwasili Jijini Dar-es-salaam, eneo la maegesho palikua na gari iliyokua ikimsubiria, aliingia humo akakutana na Muhonzi.
Wote walikua vijana wenye kufanana umri, kisha safari ilianza kuelekea kwenye makazi yao āUmesema kuna kazi?ā aliuliza Muhonzi akiwa anaipita kwa kasi scania moja iliyobeba vifaa vya Ujenzi maeneo ya Sido
āTunatakiwa kufikiria zaidi kabla ya kuichukua hii kazi, ni kazi hatari sana Muhonzi, aliyetoa amedokeza kuwa ni kazi ya kuingia Ikulu na kuiba nyaraka za siriā alinena Elizabeth akiwa anaperuzi simu yake
āOooh Mungu wangu, hivi anafikiria sisi hatuyataki Maisha yetu? Elizabeth hii kitu siyo rahisi kama anavyofikiria bwanaā
āNdiyo hivyo Mzee Baba, hofu yangu unaweza kua mtego. Kwanza nimekuja kuonana na Mtu aliyenipigia simuā
Safari yao ndefu iliyojaa mazungumzo iliishia kwenye nyumba moja huko Ilala. Walijadili kwa kina sana wakafikia makubaliano ya kumpigia simu mhusika aliyetoa kazi hiyo na simu ilipokelewa haraka sana ilionekana kuwa Mhusika alikua akiisubiria simu hiyo
āTunaweza kuonana?ā alihoji Elizabeth huku akimtazama Muhonzi aliyejawa na mchecheto
āKesho saa 9 jioni tukutane Diamond Jubelee Upangaā akasema Mtu huyo kisha alikata simu.
āOooh fuc**, unamwamini?ā akahoji Muhonzi aliyevalia prova ya njano, pensi nyeusi na soksi ndefu, alikua akiranda randa
āTunapaswa kumwamini, amesema atatoa kitita kikubwa cha pesa tunayoitakaā
āKama ni mtego?ā
āHatuwezi kunasa kwenye mtego kirahisi, kwasasa wacha tumwaminiā
**
Usiku kucha walikesha kwenye mtandao kutafuta taarifa za mpigaji wa simu, walijaribu kuidukua namba ya Mpigaji ili iwe rahisi kwao kumtambua Mtoaji kazi kabla ya kukutana naye, dakika ziliyoyoma, kazi nzito waliifanya wakiwa kwenye chumba maalum walichokitengeneza kwa ajili ya kazi hiyo lakini waliambulia patupu.
Mpigaji wa simu alikua Mtu msiri sana kwa kiingereza wanaitwa āLow Profileā
Kukosa taarifa za Mtu huyo kuliongeza chachu ya kupenyeza hisia zao kua huwenda Mtu huyo naye ni Jasusi mbobevu ndiyo maana alizificha sana taarifa zake na haikua rahisi kumdukua.
Waligida Kahawa wakiwa wanatazamana Usiku huo, mtazamano wao uliwafanya wasogeleane na kuanza kunyonyana ndimi zao taratibu huku wakitoa Miguno ya Hapa na pale Kasi yao iliongezeka huku wakiwa wanapapasana na kunyonyana ndimi zao, sekunde chache Muhonzi alikua tayari ameshaitoa pensi ya Elizabeth na kuanza kazi ya kikubwa.Ā
shughuli ya kivumbi na jasho ikawachukua zaidi ya dakika 15 kabla ya wote kuwa hoi huku akili zikiwakaa sawa na kuanza kumtafakari Mtu aliyewapa kazi ya kuiba faili Ikulu. Usingizi mnono uliwachukua pale pale
**
Siku iliyofwata waliamka na wazo moja tu, kuonana na Mtu aliyetoa kazi hiyo ya hatari, iliwapasa kusubiria hadi mishale ya mchana kisha walianza safari ya kuelekea Upanga
āMuhonzi niangalieā alisema Elizabeth,
Ni yeye ndiye aliyepaswa kuzama ndani ili kuonana na huyo Mtu, akaelekezwa sehemu ya siri ndani ya jengo hilo, alipoingia tu alijikuta akiyapeleka macho yake kwenye meza moja iliyo mbele yake, hapo alimwona Mtu mmoja
aliyevalia kofia nyeusi, aliificha sura yake haswa.
Namna alivyo ikampa uhakika Elizabeth kua ndiye anayepaswa kuzungumza naye, taratibu kwa mwendo wa Machale alisogea na kugonga meza. Yule Mtu aliyanyua uso wake, alikua ni Mwenyekiti wa chama cha Upinzani cha TUYTAĀ
āKeti hapoā alisema, taratibu Elizabeth aliketi hapo, alishaona dalili zote kuwa jambo hilo halikua utani, Mtu huyo alidhamiria kuzipata hizo nyaraka za siri, Wakati Elizabeth anaketi alisindikizwa na maneno kadhaa ya kumwondoa wasiwasi
āKwanini unazihitaji?ā aliuliza Elizabeth akiwa amemtolea macho mwenyeketi huyo wa TUYTA aitwaye Zagamba Edward, mara sauti kutoka nyuma ya Elizabeth ilisikika ikisema
āKwasababu imetosha kwake na anahitaji kulipa kwa ubaya wake, mateso na dhulma, ubaya na ubabe, wizi na utawala uliojaa kadhia nyingi ambazo zimenifanya nitoke upande wakeā ilikua ni sauti ya Mke wa Rais Mbelwa, Mke wa Rais aliketi huku akishuhudia mshangao mkubwa kwa Elizabeth
āNajua una maswali Mengi Binti, kwanini nimeichagua njia ya kumuasi Rais, kwasababu Mbelwa amekalia kiti cha Urais hali ya kuwa hatoshi, yeye ni Rais Mchafu aliyevuka mipaka.
Mtu anayeweza kumpa ujauzito mdogo wangu kisha akamuuwa, haitoshi ameigeuza Ikulu kuwa genge la Mauwaji ya watesi wake, Rais anayepanga njama mbaya dhidi ya Taifa hili, huyu hapaswi kukalia kiti cha Uraisā alisema Mke wa Rais kisha alimshika Bega Elizabeth
āMadam tumeshafikaā ilikua ni sauti iliyomzindua Elizabeth Ä·utoka katika fikra nzito ya namna alivyokutana na Mke wa Rais hadi kupanga njama za wizi ndani ya Ikulu. Mbele yake aliona Hoteli maalum ambayo Rais Mbelwa alihitaji Elizabeth akae hapo kisiri kwa siku mbili kabla ya kuondoka kuelekea mafichoni Uskochi kukwepa jicho la Usalama wa Taifa ambao walipanga kummaliza.Ā
Nini kitaendelea? Usikose sehemu ya 14 ya MSALA ndani ya SEASON 2Ā
Je, Benjamin anaokolewa au anakielekea kifo?
Hatma ya Mzee Kimaro na Elizabeth itakuaje?
AHSANTE!! Kwa kua nami katika season ya kwanza ya Riwaya ya MSALA.
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMĀ Ā
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAĀ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAĀ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIĀ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
10 Comments
Nzur ila fupi ongeza huu utamu
Mbona umetuma ya kumi na nne alafu kule juu umeandika kumi na tatu
Tunaisubiri siku nzima alafu mnatuletea simulizi fupi kiasihiki aah inaboa bwana
Ila ninzuri sana
Kaka Mkubwa Pokea Maua yako
Kaka ujitahidi usichukue mda mrefu sana kuileta epsode nyingine
Nzuri lakin fupi sana Bora zitoke ata mbili kwa siku unakaa kutwa nzima alafu ukutafupi ivi
Admin atuzingatiage bc,, ongeza tu stor marefu
Kongoreee unaupiga mwingi
Urefu uongezwe au mbili per day