Ilipoishia “Kama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke Mileleย Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, sikuย nikimaliza nitakuacha urudi kwenuโ Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwaย haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi.ย
โUnasema nini?โ niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini.ย
Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikuaย mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwambaย sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu. Endeleaย
SEHEMU YA SITA
Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nikiwa kitandani, kichwa kilikua kizito sana. Macho yanguย yalikua hayafunguki kirahisi kutokana na Uzito wa Kichwa changu baada ya kupoteza fahamuย zangu wakati uleย
Kwanza nilihakikisha pumzi zangu zinarejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kukumbukaย kilichokuwa kimetokea, chumbani hapakuwa na yeyote yule isipokua Mimi na maumivu yanguย ya Kichwa. Nilizivuta nguvu zangu hadi nikakaa kitako pale kitandani, nikawa nayasikia sasaย yale maumivu ya kuchanwa huku chini na wale Misukuleย
Chozi likanitoka kutokana na ule unyama wa yule Mzee Mwinyimkuu, nikahitaji kuelekeaย Bafuni kujikagua namna nilivyoumia maana misukule walinifanya kwa fujo tena kwa Mpigoย wote Watatu. Niliishusha miguu vizuri hadi Sakafuni, hapo nikahisi maumivu mengine makaliย mguu wa Kushotoย
โAggghโผโ niligugumia, nikapeleka macho yangu Mguu niliouhisi una maumivu, Mungu wanguย yule Mzee alinifanyia kitu kibaya sana. Alinikata kidole kimoja. Aiseeโผ nililia kwa uchunguย sana, sikuwa na kidole cha mwisho halafu damu ilikua imetapakaa mguuni, Hii siku nililiaย kuliko siku zote. Yaani nibakwe ma wale Misukule halafu nikatwe kidole kimoja hebu fikiria niย maumivu kiasi ganiย
Chozi lilinibubujika nikajikuta nikisemaย ย
โMama yangu nateseka Mwanao, nakufa huku Mimiโ Haki sikua na cha kufanya maana tayariย Nilishatiwa kilema. Nikajivuta hivyo hivyo hadi nikafika Bafuni, sikujua nianze kujikagua mguuย wangu au niukague Uchi wangu ambao ulikua ukiwaka moto kutokana na jasho lilivyokuaย
likipita. Nilivua kaniki nikaanza kuoga ili angalau nipate nguvu japo moyo ulijawa na ganziย sana.ย ย
Hiyo ilikua siku nyingine ya pili baada ya tukio la kubakwa na kukatwa kidole maana matukioย haya yote yalifanyika siku moja tena Usiku. Nilifungulia maji hadi mwisho maana palikua naย bomba la mvua, nikakaa sakafuni huku maji yakishuka mwilini kwa kasi sana. Nililia kuanziaย moyoni mwangu hadi mwili mzima. Likaja wazo la kutaka kuondoa uhai wangu maana matesoย niliyoyapata yalinikatisha tamaa ya kuendelea kuishiย
Wakati wazo hilo likiwa limekolea kichwani pangu nilihisi kumwona Mtu pale Bafuni,ย nilishutuka nikajivuta pembeni mahali ambapo yale maji yalikua hayanipigi tena, machoย yalinitoka kama fundi saa aliyepoteza nati. Mapigo ya moyo yalinidunda mithiri ya moyoย unataka kutoka ndani, Mtu yule hakuonekana kuwa Binadamu wa kawaida, alikua na nyweleย ndefu zinazo buruza hadi chini, alivalia gauni jeupe lenye damu. Kibaya zaidi alikua ni Mtoto waย kukadiriwa kuwa na Miaka 6 hadi 8 hivi.ย
Hakunionesha sura yake iliyofunikwa na nywele hizo ndefu nzito na zenye uchafu wa kutosha.ย Alisogea hadi nilipo kisha akayafunga yale maji halafu akanisogelea zaidi na kisha nilimsikiaย akisemaย
โKukata tamaa ni sawa na kuuza utu wako, usijione unapigana kwa ajili yako bali unapigana kwaย ajili ya wengi. Amka ukashinde vita ili kuwaweka huru walio wengi ndani ya nyumba hiiโย alisema yule Mtoto kwa sauti ya Kukaza sana, alikua ni Mtoto wa kike, mkononi alishikiliaย mdoli fulani wenye manyoya.ย
Kiukweli sikua na ujasiri wowote wa kuongea chochote mbele ya yle Mtoto nisiyemfahamu,ย halafu nilihisi huwenda ni mawazo yangu tu.ย ย
โNimesema amkaaaaaโผโ yule Mtoto alipaza sauti kali ya kutisha, hadi nilijikuta nikipiga yoweย la kutosha kwa hofu, niliziba masikio yangu na kufumba macho yangu, sikutaka kuendeleaย kuisikia sauti ya yule Mtoto wa ajabu, sijui alitokea wapi na kwanini aliyaongea yote yale.ย Nilipofumbua macho yangu nilikutana na Mzee Mwinyimkuu akiwa amesimama mbele yangu,ย kibaya zaidi nilikua uchi wa Mnyama, niliivuta ile kaniki na kuivaaย
โKwanini unapiga kelele?โ aliniuliza yule Mzee, nilimeza funda zito la mate nikiwa sakafuniย kule bafuni, huwa hapendi akikuuliza kitu halafu usimjibu kwa wakati.ย ย
โHapana Baba, labda..โ nilijikuta nikibabaika nisijuwe namjibu niniย
โNakuonya Binti, Maisha ya Wazazi wako yapo mikononi mwangu. Kama unataka waendeleeย kuishi basi fuata niyatakayo, kila utapofanya mapenzi na misukule nitakukata kidole kimoja chaย Mguu, hadi nitakapo maliza kuondoa vidole vyote vya miguu nitakuacha huru lakini kwa ahartiย la kukaa kimyaโ alisema yule Mzee, niliitikia kwa kichwa tu ili aondoke lakini sikuafiki etiย anikate vidole vyote vya Miguu yangu.
Alipoondoka ndipo nami nikapata unafuu wa kupumua vizuri, nikarudi chumbani mara moja,ย wazo la kujiuwa halikurudi tena kwa wakati huo, wazo likawa moja tu nitawezaje kuondoka bilaย wazazi wangu kudhurika? Halafu kingine nilichowaza ni kuhusu yule Mtoto kule Bafuni,ย aliyoyaongea yalikua maneno mazito ambayo nilihitaji kuyatafakari.ย
Ndiyo, sikupaswa kukata tamaa, sikupaswa kulia kila siku maana machozi yangu ni sawa naย machozi ya Samaki baharini huenda na maji mara zote.ย
Nilishinda na maumivu makali sana na nilipaswa kumpikia Mzee Mwinyimkuu na Misukuleย yake, siku hiyo aliniambia nipike Ugali mwingi na Maharage. Ningefanya nini, nilifanya hivyoย nikiwa natembea kwa maumivu makali sana hata hamu ya kula iliniisha.ย ย
Nikiwa jikoni mchana, nilisikia Mtu akibisha hodi. Sikujali sana sababu nilishaanza kukataย tamaa, fikiria naambiwa nikatwe vidole vyote ndio ataniacha huru, maana yake nitakuwa kilema.ย Nikamsikia akitembea kuelekea nje kumwangalia mgongaji, sijui walizungumza nini. Halafuย nikamsikia akiniitaย
Nilijikaza hadi nikafika Mlangoni, nikamkuta Akiwa na Mwanaume mmoja mnene mwenyeย kitambi na ndevu zilizozagaaย
โSaida Binti yangu, sogeaโ alisema Mzee Mwinyimkuu, aliongea kwa bashasha na tabasamu juuย halafu akaniita Binti yake, hadi nilishangaa nikasogeaย
โHuyu ni Mwenyekiti wa Mtaa. Msikilizeโ Alisema kisha yeye akasogea kwa nyuma ili mimiย ndiyo nifanye mazungumzo na Mwenyektii, sikujua anataka kusikia nini na kwanini niitweย Mimi.ย
โMajirani wanasema jana usiku na leo asubuhi zimesikika sauti za yowe kama vile kulikua naย tatizo. Nimemuuliza Baba yako anasema binti pekee uliye humu ni wewe, Je, Ulipiga yowe?โย aliniuliza Mwenyekiti, moyo ulinilipuka. Nikageuka kumtazama Mzee Mwinyimkuu,ย akanionesha ishara ya kunionya kwa kutumia macho yake. Basi nikarudisha macho kwaย Mwenyekiti, nikameza mate nikamjibuย
โSikupiga yowe na wala sijui chochote kile Kakaโย ย
โAu kuna Binti mwingine anaishi humu?โย
โHapana, naishi Mimi na Baba. Mume wangu amesafiriโ nilisema ili kuondoa ngoma juani japoย nilikua nautonesha moyo wangu kwa kiasi kikubwa sana.ย
โBasi samahani sana, pia Samahani Mzee Mwinyimkuu huwenda Majirani walisikia tofautiโย alisema Mwenyekiti lakini wakati anaongea akajikuta akipeleka macho yake kwenye Mguuย wangu akaona sina kidole, halafu kibaya zaidi kidonda kibichi. Yule Mzee hakunifunga chochoteย na wala hakukuwa na dawa yoyote ile hata Mimi ningetia ili pakaukeย
โKidole chako kimeenda wapi?โ akauliza, nikashtuka
โkidole?โ nikajikuta nikiuliza kwa mshituko nilioupata, laiti kama angelijuwa siyo kidole tu baliย hata huku chini nilichanwa na Misukule wa Mzee Mwinyimkuu sijui ingekuwaje.ย
โNdiyo ina maana hujui kama huna kidole, ona kinatoa maji majiโ alisema huku akianza kutiliaย shaka kuwa huwenda kelele walizo zisikia zilitokana na kukatwa kidole.ย
โMhโฆAaaah..โ kigugumizi kikanijaa maana sikujiandaa na swali hilo gumu.ย
โAna kisukari hivyo tulishauriwa akatwe kidoleโ alidakia Mzee Mwinyimkuu, yule Mwenyekitiย akashusha munkali wake, akaachia kicheko fulani na katabasamuย
โAaaah! Samahani tena jamani, si unajuwa ni jukumu langu kuhakikisha Wananchi wanguย wanakuwa salamaโ alisema.ย
โHakuna shida Mwenyekiti, karibu sana. Saida si umpe Mwenyekiti hata chai?โ aisee aliongeaย Mzee Mwinyimkuu kama vile ni Mtu mwema na kwamba tunaishi vizuri sana Mimi na yeyeย
โHapana nina majukumu mengine, basi Mimi naendaโ aliaga akaondoka zake, tukabakiaย mlangoni Mimi na Mzee Mwinyimkuu, akanikata jicho fulani la ukatili hadi nikachechemeaย kuelekea ndani mwenyewe. Akanifuata huko huko ndani kisha akanishika shingoni kwa nguvuย hadi nikawa nashindwa kupumua vizuriย
โNarudia Ole wako ujifanye una mdomo mrefu, hiyo hurka itakuponzaโ akasema halafuย akaniacha nakohoa kwa nguvu.ย
โ Siku nyingine ukipiga kelele zako ndio utakuwa mwisho wako humu ndani. Halafu kuna Kakaย yako anaitwa Hamidu?โ aliniuliza, nikaitikia kwa kutumia kichwaย
โAmepewa namba yangu na wazazi wako, amesema anapitia hapa kukuona anatokea Mbeyaย kisha ndio aende Dar. Sasa hakikisha hajui chochote kile hadi anaondoka, nina uhakikaย ametumwa kukuangalia unaishije sababu haupatikani kwenye simu wala Salehe hapatikaniโย Nilishtuka, sikutaka ndugu yangu yeyote yule aingie ndani ya ile nyumba ya kishetani.ย
Hamidu ni Kaka wa Mama Mdogo na Mkubwa hivyo ni Mtoto wa Dada yake Mama yangu.ย Kiukweli sikutaka Kaka Hamidu aje kwa sababu kuu mbiliย
Huyu Mzee siyo Mtu wa kumwamini, muda wowote anaweza akabadilika. Pili, kama itatokeaย Kaka Hamidu akatilia mashaka kuhusu Maisha yangu itakuwaje, si familia yangu itakuwaย kwenye matatizo? Tumbo liliniwaka moto yaani kila nilivyofikiria nilihisi kuhara, hata maumivuย ya kubakwa na kukatwa kidole hayakuweza kuyafikia maumivu ya kufikiria kuhusu ujio waย Kaka Hamidu.ย
Haki, nguvu ziliniisha Mimi. Sikuwa na simu labda ningemueleza Kaka Hamidu asije ili kuokoaย uhai wake na wa wazazi Wangu. Jasho lilinivuja, moyo ulinienda kasi sana, kibaya zaidi Mzeeย Mwinyimkuu alinitaka niigize kuwa naishi Maisha ya furaha sana ili kuwatoa hofu ndugu zangu.ย
Nilifuta kwanza jasho langu kisha nilikubaliama na hali halisi kuwa ni lazima niwe muigizajiย mzuri zaidi ya Monalisa, nikarudi zangu chumbani nikiwa nachechemea kisha nikavalia baibuiย langu na mtandio, nikakaa mbele ya kioo ili nijiweke sawa. Nikajilazimisha kutabasamu ilihaliย moyoni ninalia, nilipohakikisha kuwa naweza kuigiza vizuri nilikaa kitandani nikiendeleaย kutafakari mambo mengine yaliyonijia akilini mwangu.ย
Mara baada ya muda mrefu kupita Mzee Mwinyimkuu alikuja chumbani, hakuwa na heshimaย wala adabu na Mimi aliingia kama anaingia chooni nami wala sikushtuka sababu niliyoyapitiaย yalianza kunipa ukomavu. Akanipa hela, halafu alikuwa akinipa hela mpya tupuย
โUkitoka hapo nje kuna Pikipiki, atakupeleka sokoni kisha atakurudisha. Muandalie Kaka yakoย chakula anachopendelea, nasistiza, makosa yoyote yale yatakugharimuโ mara zote anapoongeaย ananinyooshea kidole na kunikazia macho yake mekundu kama mvuta Bangi, nilipokea naย kuitikia kwa kichwa tu. Mdomo wangu ulijawa na uzito usio kawaida sababu nilizoea kukaaย kimya.ย
โTabasamuโ alininasa kibao na kunitaka nitabasamu, basi nikaachia tabasamu la hovyo hukuย chozi likinibubujika, Nyakati hizi niliona ni namna gani Mungu niliyehangaika kumuabuduย akiwa amenikalia kimya akiniangalia ninavyoteseka Mimi. Nilifuta chozi na kuchapa mwendoย nikiwa na kapu mkononi, moyo ulinijaa chuki. Niliyachukia Maisha yangu, nikajichukia mimiย mwenyewe na zaidi nilimchukia yule Mzee.ย ย
Nilitembea kwa kuchechemea halafu kichwa kilikua kinaniuma sana, nilipofika nje nikaigizaย kutembea vizuri lakini maumivu niliyokuwa nayapata hayakuwa ya kawaida. Basi, nilimuonaย Bodaboda akiwa amesimama na Pikipiki yake, nami nikaidandia bila hata kumsalimia kisha yuleย Bodaboda akaongoza kuelekea mbele kama Mtu anayejuwa nilikua naenda wapi.ย
Ilikua ni mara yangu ya kwanza naenda mbali na nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, sikuachaย kuhuzunika ndani yangu. Niliwatazama watu wakiwa wanafanya shughuli zao kwa uhuru kabisaย tofauti na Mimi mfungwa kwenye nyumba ya Misukule. Ilituchukua wastani wa nusu saa hiviย hadi kufika sokoni, palikua pamechangamka vya kutosha na palikua na kila aina ya Bidhaa.ย
Kaka Hamidu alikua mpenzi wa ndizi za Rosti na samaki wabichi, hela ilitosha kabisa kununuaย vyote. Nilihakikisha namuacha yule Bodaboda mbali ili nipate nafasi ya kuomba simu nimpigieย Mama yangu ili nipate namba za Kaka Hamidu kusudi nimzuie asije, mwanzo yule Bodabodaย alikua akinitupia jicho kama vile alipewa maagizo ya kunichunga lakini baadaye nilimpotezaย kwa makusudi kabisa.ย
โSamahani kaka naomba nitumie simu yako, ni muhimu sana niwasiliane na Mama yanguโย nilisema haraka haraka mbele ya Muuza Samaki wabichi, akanitazama bila kunielewa nahisiย alijawa na maswali mengi yasiyo na majibuย
โSimu yangu?โ aliniuliza kama Mtu asiyenielewa kabisa, chozi lilianza kunidondoka.
โNdiyo kaka ni muhimu sana naomba niongee na Mama yangu japo dakika moja tu Mimiโย nilisema huku chozi likinibubujika. Bado yule Mkaka alikua amepigwa na Butwa halafu dakikaย zilikua zinakatika.ย ย
โWewe umetokea wapi?โ naye akaanza kunihoji badala ya kunisaidia, niliihitaji hii nafasiย kuokoa uhai wa Kaka Hamidu.ย
โKaka nisaidie kwanza mengine utayajuwa tu, samahani nipo chini ya Miguu yakoโ nikasemaย tena, halafu pale Buchani palikua na Wateja wengine wawili ambao waliweka umakini kwanguย kusikiliza, mmoja akadakiaย
โBro, si umsaidie huoni Mtu hadi analia bado unamuuliza maswali?Hebu chukua ya kwanguโย akasema Kaka aliyekuwa akisubiria kuhudumiwa, yaani maongezi yalichukua dakika tano zaย thamani ambazo zingenisaidia kumpata Mama kwanza kabla ya Kaka Hamidu. Akanipa simuย ย
yake nikaanza kujaza namba ya Mama yangu haraka na kwa pupa hadi nikawa nakosea kosea naย kurudia rudia huku mkono ukitetemeka sana hadi mwenye simu akaniambiaย
โNipe simu nikusaidieโ basi nikampa na kuanza kumtajia Namba. Kabla hata sijamalizia nambaย za mwisho nikaguswa begani, nikashtuka. Nikafuta chozi haraka, nilipogeuka nikakutana na yuleย Bodabodaย
โDada unafanya nini, muda unaenda?โ alisema, sikuwa na la kufanya pale wala sikutakaย kuendelea kuwasiliana na Mama yangu, nikatoa pesa nikampa muuza samaki, kila mmojaย akajawa na bumbuwazi la kufa Mtu. Sababu ghafla tu Mtu aliyekuwa analia na kuomba msaadaย nikawa na nguvu ya kusemaย
โKaka nipimie kilo moja nachelewa Mimiโ nilisema kama Mtu mwenye haraka, cha ajabuย hakuna hata aliyeongea tena pale isipokua kunitazama kwa mshangao, nikapimiwa samaki kishaย nikageuka na kuongozana na yule Bodaboda, nikageuka kumtazama yule Kaka aliyekuwa na niaย ya kunisaidia simu nikamtazama kwa huzuni huku chozi likianza kunibubujika. Nilikua kamaย nimemtumia Ujumbe kuwa nimeshikiliwa nahitaji msaada.ย ย
โNyie mmemuelewa yule Msichana?โ aliuliza yule Kaka akiwa pale Buchani, kila mmojaย alionesha kutonielewa mimi.ย
โUsikute anapitia magumu sana yule Msichana, siyo bure aombe simu halafu ghafla tu ajikausheย baada ya yule Mtu kujaโ akasema Muuza samaki. Yule Kaka akawaambiaย
โNgoja niwafuatilieโ aliongea kisha haraka akatoka pale kutufuatilia Mimi na yule Bodaboda.ย Binafsi niliamini asingeliweza kuelewa chochote lakini nahisi Malaika wake walimuonesha kituย juu yangu. Wakati huo Mzee Mwinyimkuu alikua akieelekea kituo cha Daladala kumpokea Kakaย Hamidu ambaye alimwambia kuwa anakaribia kufika.ย ย
Nilikuwa nimeshamaliza kununua mahitaji, nikapanda kwenye pikipiki bila kuzungumza na yuleย Bodaboda maana nilijuwa wapo timu moja na Mzee Mwinyimkuu hivyo sikutaka hata kuongeaย
chochote kile. Aliendesha kwa mwendo wa kasi sana kurudi nyumbani, sikuogopa mwendo wakeย sababu nilijiona kama Mfu anayeishi. Nyuma yetu yule Kaka alikua akitufuatilia na Pikipiki,ย Mimi wala sikujua hata yule Bodaboda hakujua kama kuna Mtu anatufuatilia hadi tunafikaย nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuuย
Yule Bodaboda alisimama na kunisindikiza kwa macho hadi naingia ndani, lakini nami sikusitaย kumfuatilia maana nilipoangalia mlangoni sikuviona viatu vya Mzee Mwinyimkuu hivyo nikawaย na uhakika kuwa alikua ametoka, nikabana mlangoni na kumchungulia yule Bodabodaย
Wasiwasi wangu ulikuwa wa kweli, akapiga simu na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwaย amenifikisha nyumbani halafu akasuburia kwa dakika kadhaa ndipo akaondoka, nilihema kwaย nguvu kisha nikaegemea ukuta kwanza ili kumiminisha chozi langu ambalo lilikua likibisha hodiย kila sekunde iendayo kwa Mungu, siyo tu kububujisha chozi bali nililia sana Mimi Saida.ย
Nilipomaliza kulia nilielekea jikoni ili kuandaa chakula cha Kaka Hamidu, Mzee Mwinyimkuuย alikua mwenye kujiamini sana sababu aliyaweka dhamana Maisha yangu kwa ajili ya Wazaziย wangu. Nikaanza kupika kwa ajili ya Kaka Hamidu.ย
***ย
Kumbe yule Kaka alikua amejificha mahali akiangalia kilichokua kinaendelea, alikua na uhakikaย kabisa kuwa nilikuwa kwenye mateso mazito, baada tu ya yule Bodaboda kuondoka basiย akamfukuzia kwanza yule Bodaboda hadi Kijiweni. Akasimamisha pikipiki yake kando kishaย akavuka barabara hadi alipo yule Bodaboda.ย
Akamwita pembeni na kuanza kuzungumza naye, kitu cha kwanza alichomuulizaย
โSamahani Bro, hunijui, wala sikujui lakini kuna jambo nataka kukuuliza. Kwanzaย unanikumbuka?โ akauliza, yule Mkaka alikuwa mweupe halafu alikua na rafudhi ya Kichaga.ย Umri wake kwa makadilio ni kama miaka 33 hivi, kwangu ni mkubwa sana hata kwa Salehe pia.ย ย
Yule Bodaboda akamtazama kwa umakini lakini hakumkumbuka kwa haraka โSikufahamu bro, unashida gani na Mimi?โย ย
โNaitwa Abuu, nilikuona pale Bucha ya Samaki kule Mjini. Ulikua umemfuata Msichana mmojaย hivi ukaondoka nayeโ alipomuuliza hivi tu yule Bodaboda akaanza kutafuta majibuย
โAnhaaโผ inawezekana, sasa unataka nini?โย
โYule Msichana aliniomba simu awasiliane na Mama yake, sasa hakufanikiwa ndiyo wewe ukajaย ila kwa namna nilivyomuona anaonekana yupo kwenye changamoto kubwa sana na anahitajiย msaada, unalifahamu hilo?โ Si unajua Wachaga hawakwepeshi maneno yao, alimchapa mojaย kwa moja na kumwacha Bodaboda akiwa anatafakari sana
โKaka unajua yule ni Mke wa Mtu, mimi kazi yangu ni kumpeleka sokoni tu. Hayo mengineย mimi siyajui na wala sifuatilii kabisaa, sasa kama unataka kufuatilia ndoa za Watu haya, ilaย nakutahadharisha sana. Hii ni Rukwaโ alisema kwa kujiamini sana.ย
Abuu alikosa cha kuongea zaidi akamshukuru tu yule Bodaboda lakini kichwani alikua naย maswali mengi sana, Basi yule Bodaboda alikua akitumika kweli na Mzee Mwinyimkuu hivyoย baada ya Abuu kuondoka akampigia simu Mzee Mwinyimkuu na kumueleza aliyoyasema Abuuย kuhusu safari ya Sokoni, Abuu akawa amejiweka matatizoni bila kujua alikua akifuatilia jamboย la hatari kiasi gani, wakamtazama Abuu kama kikwazo hivyo wakawa na mpango juu yake.ย
Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot.ย Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vileย vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yanguย niteseke.ย
Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuonaย Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikuaย nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawaย anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguoย akampa Mzee Mwinyimkuu.ย
Comments zikiwa nyingi naachia ya saba leoleo hapa
Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA SITA YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xxย
19 Comments
Wacha ni comment kabla sijasoma maana nipo hapa nasubri game ya liverpool muda wa comment ntakosa ila asante ka mkubwa๐๐๐ช๐ช
Daah….
Heee๐
Makubwa yanamkuta Saida jamani
Maskini oooh
Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na maumivu na mazingatio maishani.
Asante Admin โค๏ธ
Kaka Mkubwa
Kwa burudani โค๏ธ๐
Aisee!!!! inagusa sana itapendeza kama ukiachia sehemu inayo fuata ili kujua mwisho wake itakuwajeโ๏ธโ๏ธโ๏ธ
๐ admin zawadi yaki iyoooo
Hatariii dada kauchapa
Duh kazi ipo
Heee๐
Makubwa yanamkuta Saida jamani
Maskini oooh
Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na maumivu na mazingatio maishani.
Asante Admin โค๏ธ
Kaka Mkubwa
Kwa burudani โค๏ธ๐
Duh.inasikitisha sana jaman kama namuona anachokipitia Saida
Et tabasam la hovyo jamni
Hatari snaaaa
Hahahah dah mbn kama squad game ๐ฎ
Hatima ya saida sijui itakuaje๐ญ
Kaka amidu anafungua mlango
Naona km Bado MUNGU yupo n ww Saida . Ni Wakati tu hujfika japo kweli unteseka . Ngoja tuone pengine kaka yako atakuwa anasali .
Aseee maisha ni Giza dingii tumuombe sana mungu
So amazing
Achia sehem inayo fuata
Jamani mwendelezo tafathali