Ilipoishia “Nilipoanza kuhisi muda unakwenda na hakuna mtu aliyetoka, nikampa dakika tatu kwamba lazima atakuwa anavaa ndiyo maana anachelewa:
โLabda alikuwa anajisaidia haja kubwa, maana wengine huwa wanavua nguo zote, lakini mimi nipo, siendi kokote,โ nilisema moyoni nikiwa bado nimesimama mlangoni kwangu.
Baada ya muda, nikasikia watu wakiongea chumbani kwao, nikashtuka, nilijikuta nikisema:
โHaa!โ
Haraka sana nilitupa macho mlangoni kuangalia kandambili, nikazikuta pea mbili, nikashangaa: ”
ENDELEA SEHEMU YA NNEย
โIna maana amenipita hapahapa au? Haiwezekani, asingeweza kunipita hata kama ingekuwaje?โ niliwaza. Nilitoka kuelekea chooni, nikakuta mlango uko wazi, nikachungulia ndani, hakukuwa na mtu, nikanyoosha mikoni, nikarudi ndani.
Nilifikia kwenye kochi sebuleni, nikahema kwa nguvu kwani niliamini nimo ndani ya miujiza mikubwa ya ndani ya nyumba ile.
โHivi ni kwa nini dalali alinidanganya hivi?โ nilijiuliza mwenyewe nikiamini kwamba, dalali aliyenipangisha nyumba ile alijua mchezo mzima ila alitaka kupata fedha tu ndiyo maana alinipangisha bila kunipa tahadhari.
Nilitoka sebuleni, nikaenda chumbani, kitandani nikakuta โtoilet paperโ ikiwa imekatwa sehemu. Mimi niliicha pembeni ya dirisha, lakini ikaonesha kuna mtu aliichukua na kunyofoa kidogo kisha badala ya kuirudishia palepale, yeye aliiacha kitandani.
Mbali na โtoilet paperโ pia kuna kikopo chenye vijiti vyenye pamba za masikio kilikuwa kwenye stuli jirani na kitanda, lakini kwa muda huo kilikuwa kimeanguka chini halafu vijiti vimebaki kama vitatu tu kwa maana kwamba, aliyeingia kuchukua โtoilet paperโ ndiye huyohuyo aliyechota vijiti vya pamba.
Nilianza kuhisi kuwa sikuwa kwenye nyumba salama, lakini kwa uthibitisho upi? Moyoni nikasema nitajua tu, mimi ndiyo mimi.
Nilikaa ndani kwangu hadi usiku ulipoingia, nikasema nibadili nguo kwa kuvaa bukta na singilendi halafu nitoke kwenda kula gengeni kwani siku hiyo sikuwa najisikia kupika chochote. Ni mara nyingi nilipenda kula gengeni.
Nilitoka, nikasimama mlangoni ili nifunge mlango wa chumbani, nilipoangalia chini, upande wa wenzangu nilikuta nje ya mlango wao pana vijiti vya pamba za masikioni vikiwa vimetumika, nikiwa katika mshango, mbele nikaona tishu ikiwa imefutiwa majimaji yenye rangi nyekundu kama damu.
Nilitembea kwa wasiwasi, nikatoka nje, sikufunga mlango kwa funguo, lakini niliubamiza tu, funguo nilikuwa nazo, nikaenda gengeni kula.
Pale kwenye genge ambapo si mbali sana na nyumbani, alikuja yule mama aliyeniuliza mimi ni mtu wa wapi, nilimsalimia, lakini kabla hajaitikia alishtuka kuniona.
โUpo kijana wangu?โ
โNipo mama, nimetoka kazini nimekuja kupata kidogo.โ
โPole sana, uoe sasa.โ
โHuo ndiyo mpango wangu mama.โ
โEe, uoe halafu mimi nitakupa vyumba viwili pale kwangu, nakuahidi.โ
โNashukuru sana mama. Naanza kujipanga.โ
โSawa, vipi wenzako lakini?โ
Nilisita kumjibu, nikabaki namwangalia tu, naye alibaini kwamba nimepata mshtuko na swali lake.
โVipi wapangaji wenzako, naamini utakuwa hujaonana nao?โ/
โNi kweli mama, tena hebu nakuomba kidogo,โ nilisema nikienda pembeni kidogo ili na yeye anifuate tukaongee.
โNiambie,โ alianza kusema.
Nilimuuliza kama kuna anachokijua chochote kile kuhusu wale wapangaji wenzangu. Alianza kwa kusema:
โKusema ule ukweli sina kwa undani, ila napenda kukwambia kwamba, unaishi na watu ambao unahitajika moyo wa ziada ili uweze kuendelea kuishi nao.
โPale mbali na wewe, pameshakaa wapangaji wengine saba, tena wote kama wewe, hawajaoa. Lakini kinachoshangaza ni kwamba, wanaondoka baada ya wiki mbili, mmoja aliondoka baada ya siku tatu tu.โ
โKwa hiyo hakuna hata mmoja aliyewahi kukwambia ameona nini kule ndani?โ
โHakuna.โ
โLo! Mimi mama mambo ninayoyaona yanatisha.โ
โKama mambo yapi, nisimulie kidogo.โ
Nilipotaka kuanza kumsimulia huyu mwanamke, ghafla alitokea msichana mmoja, mweupe, mrefu kiasi, amejazia sehemu mbalimbali za mwili, akaguna na kusema:
โKaka Humuli mambo vipi, za siku?โ
Nilipata kigugumizi kikubwa kumjibu mambo poa kwani sikumjua na sikuwa nakumbuka chochote kuhusu yeye, sura yake ilikataa kichwani mwangu.
โWewe ni nani kwani?โ nilimuuliza.
Akaachia tabasamu kwa mbali, uzuri wake ukaongezeka.
โHa! Humuli, hunikumbuki mimi, kweli?โ
โSikukumbuki hata kidogo.โ
โSasa we binti, kama wewe ndiyo unamkumbuka si umkumbushe mlionana wapi?โ yule mwanamke alisema kwa sauti ya mshangao.
Lakini yule msichana mrembo alimwangalia yule mwanamke kwa macho yaliyojaa hasiraโฆ
โMama uhusiki.โ
โNajua, lakini unapoteza muda kwa kuzungushazungusha wakati kumbe wewe unamkumbuka, yeye umeshajua hakukumbuki na amekwambia tayari.โ
Nilishangaa kumwona yule msichana akibetua kichwa kama aliyekuwa akiweka vizuri nywele zake, ghafla yule mwanamke niliyekuwa naye akajishika kichwa na kulalamika kinamuuma sana.
โJamani kichwa! Kichwa jamani, daa!โ
โVipi mama, imekuwaje kwani?โ nilimuuliza.
โKichwa Humuli, kinavuta ghafla! Uwiii.โ
Nilianza kuogopa, nilihisi naangukiwa na msala maana akifa pale na watu waliona nikienda naye pembeni si nitahojiwa mimi?
โKwani mama una kawaida ya kuumwa kichwa?โ nilimuuliza nikimsogelea ambapo yeye sasa alikuwa ameinama.
โSina, ndiyo nashangaa hapa.โ
Niliona hakuna dawa nyingine zaidi ya kumpeleka kwake ili nikaungane na familia yake kumpeleka hospitali. Lakini kabla ya kufanya hivyo niliinua macho ili nimwambie yule dada anisaidie na kama anataka kunikumbusha, hayo yangefanyika baadaye.
Ile naanaza kusema anti huku nikiwa nimeinua macho, nilishangaa kutomwona yule msichana pale.
โKhaa!โ nilijikuta nikisema hivyo.
โMama twende nyumbani ili tukupeleke hospitali na watoto wako.โ
โHa! Mbona kimeachia,โ alisema akionekana kushangaa na kuniangalia, alikuwa amepanua kinywa.
โKweli?โ
โEee, niko mzima kabisa.โ
โAu?โ nilitaka kusema neno lakini zikulimaliza, nikahisi ulimi unakuwa mzito si kwa kushikwa bali kwa matakwa yangu.
โHumuli.โ
โNaam.โ
โNi kweli yule binti humjui?โ
โSimjui mama.โ
โKuna mawili hapo, humjui au humkumbuki.โ
โVyote mama, simkumbuki na pia simjui.โ
โLakini wewe si alikutaja kwa jina?โ
โMwenyewe nilishangaa sana.โ
โBasi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana,โ alisema yule mwanamke huku akiondoka zake kuelekea kwake.
Nilimtazama, lakini baadaye nilirudi kwenye kibanda cha chipsi.
โMzee nakuona na miss jini,โ muuza chipsi mmoja alisema.
โYupi, yule mwanamke?โ
โHapana, yule msichana.โ
โMi simjui, kwani anaishi wapi? Maana kasema ananijua, ameniita na jina.โ
ย โKhaa! Kumbe wewe kama sisi. Huyu dada anaishi mitaa hiihii, lakini hakuna hata mmoja anayejua nyumba anayoishi!
โKuna jamaa mmoja anaitwa Maleke, Maleke aliwahi kumfuatilia kwa nyuma lakini alishindwa kujua aliingia nyumba gani!โ
โMh! Au jini?โ niliuliza kwa mshtuko mkubwa.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tanoย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
Una Enjoy Nyumba Ya Majini? Mtumie ADMIN Ahsante
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoย kijiweni.co.tzย unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiย editor@kijiweni.co.tzย ย
16 Comments
Very nice
๐๐๐๐ mamb n motooo
uwakika
Admin weee
Nzuri
Mambo ni moto ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅmwandishi unajuwa
Ndo kumekucha Sasa uwhhhh!!!! Zingatia neno MIS JINI
Ongeza vitisho admin ili iendane na tittle Apo bado haitishi๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Mmmmh m shaanza kuogopa aaan usiku siigus hii hadith ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Jaman story mzuri Sana
Naam Naam patamu sanaaa
Hahahaha yaan Utamu siku zote huwa unaishia kati kati daaa๐๐๐๐๐ admin huna baya
๐ท๐ท๐น๐น๐บ๐ฅ admin chukua maua yako hakika unatukosha haswa
Mungu wangu
Amaizing
Admini nakubali kazi zako lakini napenda kukwambia hili igizo lisha igizwa na kurushwa sinema zetu… Ila kazi iendelee