Ilipoishia “Jacklin Mwanangu sijapata pesa kama unaweza kusubiria hadiย jioni sawa” Alisema Mamaย
“Usijali Mama nitarudi tu” Nilisema, sikuwa na pesa ya nauliย ya kurudia nyumbani alafu mvua ilikuwa ikinyesha sana,ย kulikuwa na hali ya radi pia, nilifikiria kama Osmanย angelinikuta pale nje ingeleta picha mbaya zaidi, nilifikiriaย pia ile pesa niliyompa kwa hasira, nilijilaumu sana kwaย kiburi changu. Basi niliingia kwenye mvua, nilivua viatuย vyangu. Endeleaย
Kumbe yule Mdada msaidizi wa Osman alikuwa akiniangalia tu,ย alienda kumwambia Osman, nilitembea kwenye mvua nikiwaย natetemeka, kufika nyumbani kwetu kwa mguu ni zaidi ya masaaย matatu. Kwa jinsi mvua ilivyokuwa ikinyesha ilionesha waziย kuwa isingelinyamaza kwa muda huo, basi niliendelea kutembea.ย Osman alipopata taarifa kuwa natembea kwenye Mvua aliachaย kazi zake, alichukua Mwamvuli akaingia kwenye gari yakeย akaanza kunifukuziaย
Ilifika mahali baridi lilinizidia, nilitembea kwa maumivuย makali huku nikimfikiria sana Mosses, kwanini hakunitumiaย hiyo pesa? Kwanini alikuwa hapokei simu zangu, nilijikutaย nikilia njiani sababu moyo wangu nilimpa Mosses, niliulaumuย ย umasikini ambao Baba yangu alituachia, nilimlaumu Munguย kwanini alimchukua Baba wakati akiwa masikini?
Mara nilisikia Honi ya gari, niliipisha ipite lakiniย haikufanya hivyo, alikuwa ni Osman. Nilipogundua ni yeyeย niliondoa mikono yangu kifuani, nilitabasamu ili asione kamaย kutembea kwenye mvua kumetokana na kutokuwa na hela bali niย mazoezi tuu. Alishusha kioo akaniambiaย
“Ingia kwenye gari nikusogeze Jacklin” Alisema kwa busara naย hekima ya hali ya juu sana, pesa alizonazo Osman hakustahiliย kuninyenyekea namna ileย
“Hapana nafurahia maajabu ya Mungu” Nilisema huku nikiwaย napiga hatua huku Osman akiendesha taratibu.ย
“Hapana mvua ni kubwa sana Jacklin, twende nikupeleke kwenu”ย Alisema tena Osmanย
“Usijali Osman, nitachukua Tax mbele, nafurahia mvua kwanza”ย Nilisema nikiwa nimeshikilia viatu vyangu mkononi, Basi Osmanย alifunga kioo ili aondoke zake, kiukweli hali yangu haikuwaย nzuri, lile baridi lilinitesa sana, njaa ilikuwa ikinikwanguaย vibaya mno, nilijikuta nikianguka kwenye mvua.ย
โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขย
Nilipokuja kurudisha fahamu zangu nilijikuta nikiwaย Hospitali, Osman alikuwa amekaa kitandani, Mama yangu alikuwaย pembeni yanguย
“Mama!” Nilimuita Mamaย
“Jacklin Mwanangu, nesi Mwanangu ameamka” Alisema Mama,ย alinifanya nitabasamu sana, Upendo wa Mama ulikuwa Mkuu sanaย kwangu, niligeuza macho na kumtazama Osmanย
“Asante sana Osman” Nilisema nikiwa natabasamu japoย nilipoteza fahamu ila nilijuwa tu aliyenisaidia alikuwa niย Osman, kabla hajanijibu Chochote nesi alikuja kwa ajili yaย kuangalia hali yangu, Osman alimwambia Mamaย
“Naomba tuongee kidogo Mama” Basi Mama na Osman walitoka hukuย Daktari akiwa ananiangalia kwa makini na kiniuliza baadhi yaย Maswali ili kujuwa nilikuwa najisikiaje.ย
Osman alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo, alimuulizaย Mamaย
“Huyu ni Binti yako wa kumzaa?” Mama alitabasamu kishaย alimjibu Osman
“Ndiyo, ndiye Mtoto pekee ninayemtegemea, nakushukuru sanaย Baba japo sijakufahamu maana umenipigia tu simu na kunielezaย kuhusu hali ya Binti yangu, kwa jinsi nilivyokuwaย nimechanganikiwa wala sikuwa na muda wa kukuuliza” Alisemaย Mamaย
“Naitwa Osman, Mimi ndiye mmiliki wa kampuni ambayo Bintiย yako alikuja kuomba kazi” Alijitambulisha Osman kwa Mamaย yanguย
“Ooh! Asante sana Baba” Alisema Mamaย
“Sasa Mama! Pamoja kwamba hali ya Binti yako unaiyona ipoย sawa lakini kuna tatizo kubwa sana katika mwili wake,ย inaoneka figo zake zote mbili hazifanyi kazi ipasavyo,ย inatakiwa kubadilishwa, kama zitapatikana mbili au moja iliyoย imara sana” Alisema Osman, Mama alishindwa hata kusimamaย aliomba akae kwanza, akiwa kama Mama alichanganikiwa sanaย kusikia nina tatizo la figo zanguย
“Unasemaje?” Aliuliza Mama akiwa anakaribia kuanza kuliaย
“Ndiyo maana Mama nimekuita hapa iliniweze kuzungumza na weweย kuhusu hali ya Jacklin, ana siku 30 za kufanyiwa matibabu”ย alisema Osmanย
“Sasa mimi na umasikini huu nitaweza vipi Baba yangu? Munguย kwanini ananipa mtihani mzito kiasi hiki niimemkosea niniย Mimi?” Alisema Mama akiwa analia, Osman aliketi na kumwambiaย Mamaย
“Mimi nina safari ya kwenda Dubai kesho, gharama zoteย nitazifanya. Mnapaswa kutafuta Mtu wa kumtolea figo Jacklin”ย Alisema Osman, angalau Mama alifuta mchozi wakeย
“Nitakuunganisha na daktari Bingwa wa hii Hospitali,ย mtasaidiana itakapopatikana hata moja imsaidie Binti yako”ย Alisema Osman, Mama alimtazama Osman akamwambiaย
“Wewe ni Binadamu mwenye moyo wa peke yako Mwanangu, Munguย azidi kukubariki kwenye kila hatua” Alisema Mamaย
“Ila Mama naomba hili liwe siri yako, Jacklin hapaswi kujuwaย kama ana tatizo la figo sababu akijuwa inaweza leta shidaย zaidi” Alisema Osman, walipomaliza kuzungunza walirudiย wodini, walinikuta nikiwa ninafakamia vyakula maana njaaย niliyokuwa nikiisikia haikuwa ya kawaida, sura zaoย hazikuonesha dalili ya tatizo lolote lileย
“Jacklin!” Aliniita Mama kisha aliketi kitandani
“Kama kuna Binadamu ana roho nzuri katika hii Dunia basi huyuย Kijana ni namba moja, namshukuru kwa kuokoa Maisha yako”ย Alisema Mama kisha alitabasamu, kumbe Osman alikuwaย amewasiliana na Mosses na kumwambia kuwa nilikuwa nina umwaย sababu namba ya Mosses nilisave kama Mume wangu, alikuja mudaย huo, alinikumbatia na kunipiga busu mbele ya Mama na Osman,ย Mama alishangaa sana sabahu alikuwa hamfahamu Mossesย
“Mama!! Huyu anaitwa Mosses, ni..ni…ni” nilishindwaย kumtambulisha Mosses mbele ya Mama na Osman, Basi muda huoย huo Osman aliaga na kuondoka zakeย
“Mama huyu ni Mchumba wangu anaitwa Mosses…..Mosses huyu niย Mama yangu” Nilijitahidi hadi kumtambulisha Mosses kwa Mamaย yangu, japo niliona Mama hakufurahia ila alijikaza tuย
“Oooh!! Sawa, basi mpate muda wa kuongea Mimi naenda kwaย daktari” Alisema Mama, kumbe alikuwa anataka kumuwahi Osmanย nje, kweli alimkimbilia Osman kabla hata hajapanda kwenyeย gari akamuita, alipomfikia alimwambia Osmanย
“Baba upo sawa?” Aliuliza Mamaย
“Ndiyo Mama nipo sawa, naenda kuendelea na kazi” Alisemaย Osman, ila Mama alihisi kuna jambo lipo ndani ya Osman kwaย jinsi alivyoaga pale wodini.ย
“Nakuomba Mwanamgu, msaidie Jacklin apone na Mungu atakulipaย zaidi” Alisema Mama, Osman alimsogelea Mama akamwambiaย
“Ni jukumu nililokuahidi Mama, Mwanao atarudi kuwa sawa tuย wala usijali, hii hapa ni kadi yangu ya Biashara” alimpatiaย Mama kadi yenye mawasiliano yake, Osman aliingia kwenye gariย yake na kuondoka.ย
Mosses alikuwa ndiyo Mwanaume niliyempenda sana katika Maishaย yangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu, nilimuulizaย
“Kwanini ulikuwa haupokei simu yangu?”ย
“Samahani Mke wangu, unajuwa muda ule nilipatwa na dharuraย nikaenda kumuona Mdogo wangu alikuwa ana tatizo” Alisemaย Mossesย
“Ooh pole sana, anaendeleaje”ย
“Yupo sawa, hivi huyu jamaa aliyekuwa amekaa hapa ni nani?ย Mbona baada ya kukupiga busu aliaga?” Aliuliza Mosses
“Mmmh! Jamani Mosses, ni rafiki tu, ndiye aliyenisaidia”ย nilimjibu Mosses, kitu kilichokuwa kikinivutia zaidi kwaย Mosses ni wivu wake kwangu, yaani nisisimame na Mwanaume auย kuongea nayeย
“Anhaa! Sasa sitaki hayo mazoea na huyo jamaa sawa?” Alisemaย
“Mmmh! Sawa” Nilimjibu, Mama aliporudi alitukuta tukiwaย tumemaliza mazungumzo, basi alimuita Mosses pembeni naย kumueleza kilichokuwa kikinisibu sababu alikuwa Mtu wangu waย karibu sana.ย
Mosses alipoambiwa hivi kuwa nina tatizo la Figo alimuulizaย Mamaย
“Mama unajuwa matibabu ya Figo yana gharama kubwa sana naย kama hivyo umesema yanahitajika ndani ya siku 30 tu,ย itakuwaje?ย
“Sasa unafikiria nitafanya nini Kijana? Japo yupoย aliyejitokeza kugharamia matibabu ila hatuwezi kumuachia yeyeย kila kitu ndiyo maana nimekueleza na wewe ili nione kwaย upande wako utajitoa vipi maana Jacklin ni wako wewe” Mamaย alisema, maneno ya Mama yalijaa uchunguzi sanaย
“Mama naomba siku moja ya kutafakari kisha nitakupa mrejeshoย wa nini ambacho mimi nitafanya, ila nakuahidi kuwa tupoย pamoja” Alisema Mosses, basi siku hiyo niliruhusiwa kurudiย nyumbani ila nilikuwa nahisi maumivu kiasi fulani kwenyeย mbavu zangu, jinsi Mama alivyokuwa akinifanyia kila kituย ilinitia shaka sana nilimwambiaย
“Mama Mimi nipo sawa huna haja ya kunifanyia kila kitu” “Nafanya sababu nakupenda Jacklin” alisema Mamaย
“Najuwa kuwa unanipenda lakini nilianguka sababu ya baridi tuย Mama hakuna kingine, nipo sawa” Mama hakusema chochote kileย kuhusu tatizo nililokuwa nalo la figo, siku iliyofuata Osmanย alienda Dubai kama alivyomwambia Mama.ย
Usiku wa siku hiyo, kilikuwa kipindi cha mvua hivyo kulikuwaย na baridi sana, Mama alikuja na kuniambia kuwa Osman alikuwaย ameshaondoka, ilinishangaza sana namna ambavyo Osman na Mamaย awalikuwa karibu kiasi hicho hadi kuanza kujuwa kuhusu safariย ย
za Osman, nilicheka kwanzaย
“Mmh! Mama nawe, yote hayo umeyajuaje? “
“Si kaniambia mwenyewe jana kule Hospitali, alafu Jacklinย ngoja nikuulize swali, unamuonaje Osman?”ย
“Mh! Mama hebu liweke vizuri hilo Swali, namuonaje kivipiย tena?”ย
“Hujausoma Moyo wake? Hujahisi kitu ndani ya moyo wa yuleย Kijana?”ย
“Sasa Mama naanzaje kuusoma moyo wa Mtu ambaye sina ukaribuย naye? Alafu hata kama akiwa na kitu moyoni mwake mimi tayariย nina Mtu wangu..”ย
“Sijamaanisha eti uwe naye hapana ila nimekuuliza tuuย Jacklin, anaonekana ana upendo sana yule Kijana” Mamaย aliendelea kusema mafumbo ila niliijuwa nia yakeย
“Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiย hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoย nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”ย
“Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaย na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaย kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya Mossesย kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaย kuchukua namba kwenye simu yangu.ย ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tatu Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
15 Comments
Dooohhh ๐ฅดhuyu moses apotelee mbali bhn abaki Osman๐
๐๐๐kivumbi
Hii inanikumbusha kuna tamthiliya moja ya mfadhili …kiswahil Advance level
Mm limoses nshaanza kuliona n jau …awe n Osman tu
Lus unapenda ela wew๐
sidhani kama moses atapatikana tena kwenye simu
Huyo Moses ayeyukiee juani
Ef 5 tu alizima itakuwa kuchangia Figo๐ ๐ ๐ ๐
Dada wa wap uyu mbona achangamkii fursa
Aah uhondo huu natamani usiishe hongera Kwa kaz mzuri ๐
Ongeza kidogo urefu wa liwaya mtunzi tunaenjoy sana.. ๐๐ฟ
I SEE MFADHILI ON ONE AND TWO๐๐
Mwandishi ungekuwa mcheza mpr.. bc tungekuita pele..
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Osman anaenda kuchukuwa mzigo kupitia ushawishi wa mama