HATIMAYE Bodi ya Ligi wametangaza Ratiba ya Msimu wa Ligi Kuu 2024/25 ambayo itaanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 16 kwa mchezo mmoja pekee, huku Simba wakifungua Ligi tarehe 18 dhidi ya Tabaora Utd.
Simba SC watafungua msimu wao pale KMC Complex, ambapo inaelezwa kuwa wamechagua kutumia uwanja wa KMC Complex pale Mwenge kwa michezo yake ya nyumbani , lakini mechi kubwa zote zitapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Bingwa Mtetezi wa Ligi kuu ya NBC Yanga SC, wataanza kuusaka Ubingwa wa 4 mfululizo kule mkoani Kagera katika Dimba la Kaitaba, kisha watarejea Azam Complex ambapo watapatumia kama Uwanja wa nyumbani pia kwa msimu huu kwa sehemu kubwa ya mechi zao.
Azam FC wao wataanzia kwa Mej.Jen. Isamhuyo vs JKT Tanzania.
MECHI 10 ZA AWALI ZA SIMBA SC 2024/25
Simba vs Tabora Utd
Simba vs Fountain Gate
Tz Prisons vs Simba
Azam FC vs Simba
Simba vs Namungo
Dodoma Jiji vs Simba
Simba vs Coastal Union
Simba vs Yanga Okt 19
Mashujaa FC vs Simba
Simba vs JKT Tanzania.
MECHI 10 ZA AWALI ZA YANGA SC 2024/25
Kagera Sugar vs Yanga
KenGold FC vs Yanga
Yanga vs JKT Tanzania
Yanga vs Mashujaa FC
Singida BS vs Yanga
Yanga vs KMC FC.
Yanga vs Pamba Jiji
Simba vs Yanga
Yanga vs Tabora Utd
Coastal Union vs Yanga
Mechi kubwa inayotazamwa na wengi ni ya Simba na Yanga ambayo itapigwa Oktoba 19, ikiwa ni mechi ya 8 tangu kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC.
11 Comments
Simba wakifungwa mech mbil za mwanzo napumzika kuwa shabiki mwaka wote🙌
Hahaha 😂 anza sas mtani pumzika kuanzia sas hv
Kama itaonekana basi simba inafungwa Tena kwa kikosi Cha simba basi mm na mpira ndio basiii siwezi kwenda yanga ila Bora niache kushabikia tu💯
Simba chama langu
Simba vs Azam
Simba vs Namungo Game nzur zakutazma
Mshabiki yeyote ambaye hana maslahi natimu, haichangii timu walk hajulikani kwa kiongoz yeyote wa timu kuanzia ngazi ya juu mpaka matawi. Ukihama nisawa na mzazi aliemzaa mtoto kisha mtoto huyo akawa kichaa na akasema huyu sio mwanangu kwasababu ni kichaa.
Yanga bingwa
Naiman na simba ya msimu huu
Wana Simba SC waendelee kupiga mazoezi ya kutafta muunganiko wa timu maana hata uwanja wa nyumbani tulochagua unaonekana wa ugenini ni bora azam complex stadium..so wachezaji wajitume maradufu ubingwa ni wetu mwaka huu ni wa kufoc.
Simba SC nguvu moja ubingwa nauona ni kuchanga karata za ligi vzr tu
Hahaha 😂 anza sas mtani pumzika kuanzia sas hv